Leo nina furaha ya ajabu, nimevuna 14 wa CCM

Leo nina furaha ya ajabu, nimevuna 14 wa CCM

Abel Ndundulu

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2015
Posts
847
Reaction score
389
Leo nina furaha ya ajabu.Nimefanikiwa kuwashawishi rafiki zangu 14 ambao walikuwa wanatarajia kumpigia kura JPM ili waweze kumpigia kura Edward Ngoyai Lowassa pamoja na madiwani na wabunge wa vyama vya UKAWA.

Mkakati wangu ni kwamba mpaka kufika tarehe 25/10/2015 niwe nimewashawishi wapumbavu na malofa wenzangu wapatao 224 kwa wastani wa watu 14 kila siku.

Naamini kwa mkakati huu tutaiweka pembeni CCM tunayoipenda ili ikajitafakari ikirudi ije upya.Kumbuka mimi ni Mwana CCM kindakindaki ambaye sijaridhishwa kabisa na mwenendo wa chama changu kukabiliana na Ujinga,maradhi,umaskini na rushwa.

Mwana CCM mwenzangu,kama unaipenda CCM amua sasa kuiweka pembeni ikafanyiwe marekebisho muhimu na ya Kimsingi.Gari bovu halifai barabarani.Litasababisha ajali mbaya isiyosahaulika.

Tuifanyie overhaul kwa miaka mitano MUNGU akipenda irudi ikiwa mpya.Je unaungana na mimi?Kama ndiyo gonga LIKE.

Kama hapana potezea!!
 
Weka ushaidi,usije kuwa anajitekenya mwenyewe na kuchekwa kwa hiyo elfu 5 uliyopewaa??
 
Hongera sana .nami jana nimembadilisha mzee mmoja mbishi sana mwenyewe kafurah kanisifia sana kwa kumfunua ubongo wake.
 
Unafanya kaz nzur tatzo hawatuelewi kuwa tukiitoa ccm madarakan hakutakuwa na chama chenye mamlaka na watz kwahyo maamuz yatarud kwetu watz nani tumuweke nani tumtoe.... Huu ni ukomboz baada ya miaka 54
 
Hongera sana .nami jana nimembadilisha mzee mmoja mbishi sana mwenyewe kafurah kanisifia sana kwa kumfunua ubongo wake.

Nimefanikiwa kupata wawili leo,Rais Mtarajiwa alikuwa sanya,Ni rahisi sana tafakari hotuba ya MH Lowasa,hawajawhi kubadili maneneo hayo ameongea kutoka rohoni,ni kweli imani huzaa imani,na sisi tumemwamini kwamba elimu,Elimu,Elimu ni mkombozi kwa maskini,Hii nimeipenda sana maana elimu ndio msingi wa maisha,lengo letu nipate watu 100,amabao tunajua ni wana CCM,wajiunge na familia ya mabadiliko
 
Hili bandiko lako linanikumbusha mtu mmoja niliyesikia kuwa ni gamba lakini mkewe ni #teammabadiliko, kaona hamna jinsi hivyo kaficha kichinjio ili mama atakapostuka labda tarehe 24 usiku asikipate.
Nami ngoja niingie mtaani kwa busara mpya kutafuta japo hata mmoja. Nadhani jimbo la Vunjo sasa hivi wakaazi wake wako wazi zaidi kujiunga na mabadiliko!
 
Hongera mkuu,mimi wabibi wawili wa CCM kindakindaki wanapigia UKAWA!!!
 
kila mtu akufanikiwa kumshawishi walau mtu mmoja tu ushindi wa kishindo lazima
 
Oyoooooooooooo wela welaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Pole sana, nikusikitishe tu ni bora uache kushangilia, maana mimi hapa nilipo nimepasuka kwa furaha, leo nimevuna watu 536 wenye kadi za kupigia kura na ambao walishaamua kumpigia kura Lowasa.

Sasa fanya mahesabu yako, niliowapata mimi, toa wako, utajua ccm imepata faida bei gani.

Biashara mahesabu sio mbwembwe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom