Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,810
- 15,398
Kumbe ni suriama aliyechanganya damu ya Kiholanzi na Kitanzania. Mama yake ni M-TZ na baba ni Mholanzi. Wakati anaripoti hapa kazini kwetu kama CEO wetu mpya akitokea nchini Uingereza yalipo makao makuu ya kampuni yetu nilikuwa nimesafiri kikazi na leo hii niliporipoti kazini ndio nimetambulishwa kwake rasmi. Nilipata muda wa kubadilishana naye mawazo kwa muda mfupi………..Kwa bahati mbaya hajui Kiswahili vizuri, lakini nimemuahidi kumfundisha lugha hiyo. Huyu atakuwa ndiye The Boss wetu mpya aliyekuja kuchukuwa nafasi ya Boss wetu aliyemaliza muda wake.................................