Leo nimeonana na The Boss……………..!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,379
Kumbe ni suriama aliyechanganya damu ya Kiholanzi na Kitanzania. Mama yake ni M-TZ na baba ni Mholanzi. Wakati anaripoti hapa kazini kwetu kama CEO wetu mpya akitokea nchini Uingereza yalipo makao makuu ya kampuni yetu nilikuwa nimesafiri kikazi na leo hii niliporipoti kazini ndio nimetambulishwa kwake rasmi. Nilipata muda wa kubadilishana naye mawazo kwa muda mfupi………..Kwa bahati mbaya hajui Kiswahili vizuri, lakini nimemuahidi kumfundisha lugha hiyo. Huyu atakuwa ndiye The Boss wetu mpya aliyekuja kuchukuwa nafasi ya Boss wetu aliyemaliza muda wake.................................
 
Hahahaha mwambie kuna kitu inaitwa jf,ajiunge.
Nitaharibu kazi..........Sitaki hapa ofisini kwangu wajue mimi ni memba humu JF..............
Kuna siku HR wetu aliniuliza kama ninaijua JF, niliruka kimanga ................ nikamuuliza hiyo ni software gani?
 
khe mzizi usijeleta uzi hapa wa kutedwa na suriama inavyoosha uneshamzikia au uongo?
Keshanambia ana mchumbake huko Uingereza.............. Atakuwa anamtembelea kila mwaka kipindi cha Krismas.........
 
Keshanambia ana mchumbake huko Uingereza.............. Atakuwa anamtembelea kila mwaka kipindi cha Krismas.......

acha njanja yako fimbo yambali haiui nyoka af upime kwa maana hao mashori wa majuu hawaaminiki tusije tukapoteza kijana.
 
Asi don't nini we do
it bwana tena badili na ofisi kashanisumbua kweli kila saa anakuja
kukuulizia hadi nashindwa kufanya shughuli zangu hapo utakuwa umempa ban
ya ofisi
Sikuwezi kwa nahau..........!
 
Nitaharibu kazi..........Sitaki hapa ofisini kwangu wajue mimi ni memba humu JF..............
Kuna siku HR wetu aliniuliza kama ninaijua JF, niliruka kimanga ................ nikamuuliza hiyo ni software gani?

Ni software inayomtatiza Gertrude lwakatare!
 
Keshanambia ana mchumbake huko Uingereza.............. Atakuwa anamtembelea kila mwaka kipindi cha Krismas.........
Na ratiba ya kurudi hm ikibadilika tu namwambia mama kuhusu huyo Suriama wako!
Maana wewe mzee hata hueleweki!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom