Leo nimeona uongo wa mchungaji Bushiri

Leo nimeona uongo wa mchungaji Bushiri

Ukitaka kujua utapeli wake angalia prophetic channel at least mwaka mmoja hivi. Mimi nimemfuatilia tangu 2013 yaani ametapeli wengi sana badala ya kuwaacha waende jehanam yeye anawafundisha siri za mbinguni, anaudhi sana.
Mwingine tapeli ni Ontario yaani anafichua siri za jinsi ya kutajirika wakati asili yetu ni umaskini, umaskini upo kwenye damu yeye anataka tuachane nao, Ontario huyu.
Nimebaki nacheeeeka.....!!!!! Hope watakuelewa ulicho andika hapa.
 
mkuu hivi yule razalo mla makombo pale nyumbani kwa tajiri hakuwa mtoto wa Mungu? naomba unijuze kidogo hapa
Lazaro alikuwa mtoto wa Mungu. Mungu huwapenda wote akina Lazaro na akina Zakayo wenye uwezo wa kuwagawia watu mara nne ya mali zao.
Yesu alikuwa anafundisha kuwa Jilindeni na choyo maana uzima wa mtu haumo ktk wingi wa vitu alivyonavyo. Utaona kuwa yule tajiri alikula kwa anasa na mlangoni pake yupo Maskini Lazaro lakini hakuweza kumsaidia. Lakini mfano huo haukumaanisha kuwa watoto wa Mungu wa ukweli lazima wawe maskini. Huyu tajiri Alimpa makombo Lazaro eti ndo msaada kwa maskini. Hilo Mungu halipendi kabisa.

Kujua kuwa Mungu hapendi umaskini
1. Alimwambia Ibrahimu Mwanzo 22:17. (Katika kubariki nitakubariki na alimbariki hasa)
2. Mungu Alimbariki Isaka mtoto wa Ibrahimu hadi Wafilisti wakamuonea wivu Mwanzo 26:12-14
3. Waisraeli walitoka Misri na utajiri mwingi. Kutoka 12:35-36
4.Ayubu alikuwa tajiri na hakumuacha Mungu hadi Mungu alijivunia. Ayubu 1
5. Wanafunzi wa Yesu walimiliki mali. Matendo 4:32-36.
Ingekuwa utajiri ni dhambi basi Biblia ingejaa maskini. Ibrahim, Isaka, Yakobo, Yusuph, Daniel, Musa,Eliya, Daudi, Solomoni, Ayubu n.k hawakuwa maskini.

Mbinguni wataenda wote maskini na matajiri. Mtu akitaka kwenda akiwa maskini basi utampata na ataenda nao hivohivo. Anayeutaka utajiri hivohivo.

Kipimo cha mtumishi wa Mungu si mali alizonazo mtu.
mkuu hivi yule razalo mla makombo pale nyumbani kwa tajiri hakuwa mtoto wa Mungu? naomba unijuze kidogo hapa
 
Huyu cha mtoto kuna nabii mungu wake anajua lugha moja tu na ana wafuasi kibao halafu mnamshangaa huyu.
 
Niliwahi kuona kideo youtube akiwa exposed yaani aliumbuka ila alifanya kila njoa kutaka kulazimisha aliyemuumbua hanazo huko juu..
 
HABARI NGOA NIANZE NA SIFA ZAKE
View attachment 673732

1. Alishawahi tembea angani
2. Ana uwezo wa kuongeza account yako ya bank na ikajaa pesa
3. Na kadhalika ila hana ushuhuda zaidi wa hapo tu kanisani na bila uthibitisho

Huwa nawaambia hawa wachugaji sio watu wamejaza makanisa na kujifanya wanafanya miujiza kumbe ni akili tu wanacheza na watu na ni biashara huwa wanafanya juu chini kuakikisha watu i mean waumini waamini kama kweli Mungu ana tenda ila kwa hii video nilio iona twitter huyu wanamuita bushiri nime mdharau sana sio kidogo hebu tazama huyu bashiri wa nigeria ambae ana wafuasi wakutosha na anajaza kanisa huwa naiuliza swali kwanini ni sisi africa tu tuna roho nyepesi na ya kutukuza hadi kufikia kuacha kuuomba mungu na kubaki kuweka imani kwa hawa watu 100% hii video niya twitter bonyeza uone maana nimejaribu ku download imee nizengua.

kumbuka mimi sija mponda ila nime chukia uongo wake kufundishwa njia za mbinguni hata wewe una weza ukiwa mwenyewe ila kinacho niuma ni watu ku nyenyekea kwakwe kuitisha pesa ukitaka kumuona nakadhalika sasa kama hii video anaonyesha anafanya miujiza kumbe hamna kitu na watu wana amini ni nini sasa hii

Hawa ni wezi tena hawajifichi. Wanaiba mbele ya macho ya serikali. Ni waongo na wauwaji. Wanawadanganya watu kutowa sadaka na kuwapa ahadi za uwongo huku wakijitajirisha. Hii imekuwa biashara kubwa Afrika ya kuwaumiza watu. Serikali lazima ichunguze hawa watu. Huwezi kuwa mtu wa MUNGU kuchukuwa pesa kwa masikini na kujinunulia majumba na magari Wakati waumini wako wanalala njaa. Dini hizi za uwongo zinachipuwa kama uyoga pori wenye sumo. Hawa watu wanatuibia mala mbili, wanawaibia wanaumini wao na wanaiibia serikali kwa kutolipa kodi.
 
Mchungaji anapiga picha kuonyesha mjengo wake na magari anayomiliki. Labda anachunga bata mzinga.
 
Kuna prophet mmoja hapo anajiita prophet shila.
Hata jana kaweka video insta anahesabu mihela.
 
mwacheni ale maisha wajinga ndio waliwao!
na mimi mwanangu akitimiza miaka mi5 namnunulia Bugatti kama sio Boeing kabisa!
 
HABARI NGOA NIANZE NA SIFA ZAKE
View attachment 673732

1. Alishawahi tembea angani
2. Ana uwezo wa kuongeza account yako ya bank na ikajaa pesa
3. Na kadhalika ila hana ushuhuda zaidi wa hapo tu kanisani na bila uthibitisho

Huwa nawaambia hawa wachugaji sio watu wamejaza makanisa na kujifanya wanafanya miujiza kumbe ni akili tu wanacheza na watu na ni biashara huwa wanafanya juu chini kuakikisha watu i mean waumini waamini kama kweli Mungu ana tenda ila kwa hii video nilio iona twitter huyu wanamuita bushiri nime mdharau sana sio kidogo hebu tazama huyu bashiri wa nigeria ambae ana wafuasi wakutosha na anajaza kanisa huwa naiuliza swali kwanini ni sisi africa tu tuna roho nyepesi na ya kutukuza hadi kufikia kuacha kuuomba mungu na kubaki kuweka imani kwa hawa watu 100% hii video niya twitter bonyeza uone maana nimejaribu ku download imee nizengua.

kumbuka mimi sija mponda ila nime chukia uongo wake kufundishwa njia za mbinguni hata wewe una weza ukiwa mwenyewe ila kinacho niuma ni watu ku nyenyekea kwakwe kuitisha pesa ukitaka kumuona nakadhalika sasa kama hii video anaonyesha anafanya miujiza kumbe hamna kitu na watu wana amini ni nini sasa hii

Kwan mkuu hukujua kama hawa watu nimatapeli?
 
Kwan mkuu hukujua kama hawa watu nimatapeli?
nilikuwa najiulizaaga tu kuwa hawa watu ni nguvu gani wanatumia hadi wanafanya miujiza sasa katika pita pita zangu ndo nika mkutaa huyoo mchungaji nikamfatilia kumbe ni muongo kupindukia halafu uongo wa hadharani. sasa ndo nimegundua kuwa wanacheza na akili za watu na sio miujiza wala nini
 
Wajinga ndowaliwaoo mkuu
 
Wajinga hawaishi labda bahari ikauke

Ova
 
Aliedownload hiyo naomba anitumie tafadhari
 
Siyo mnigeria huko SA na Nigeria na kwingineko kuna makanisani yake tu Yeye ni MMALAWI
 
Back
Top Bottom