Myahudi Jr II
JF-Expert Member
- Jan 7, 2016
- 7,005
- 9,264
Leo ni Jumanne, tena asubuhi na mapema ila lazima salamu hizi nizitoe kwakweli. Wewe Officer (Capatain), mabega yako yamepambwa vizuri na nyota 3 kwenye kila bega zenye rangi ya dhahabu zing'aazo kama nyota ya Asubuhi iangazapo ulimwengu.
Tabasamu lako lililoacha meno meupe nje yaliyopangika vizuri, nilipokusalimu, "Habari yako dada" ukajibu huku ukiniangalia kwa kuzingatia sana.
Nyusi zako zilizochanwa vizuri sana utadhani zimetindwa zinazolinda macho yako meupe ya gololi yenye kope murua kama manyoya ya kifaranga mwenye siku 5
Haya yoote yamekua ndoto baada ya kushuka kwenye vidole vyako na kukuta pete nzuri ya rangi ya dhahabu kwenye kidole chako.
Ukapanda Rava 4 yenye rangi ya silva, ukiwa dereva ukampakia mjamaa mmoja alievalia T-shirt yenye mistari ya yangi nyekundu hivi
Ulikua umesuka msuko flani hivi, nywele zote umezileta katikati.