Leo nimebaguliwa na Wahindi

Status
Not open for further replies.

Ni kweli maneno yako Mkuu. Nimeshuhudia ofisini kuna Mzungu alikuwa na allergy na perfume yoyote. Ofisi Yake ipo sealed kabisa. Kuongea nae ni kwa simu tu. Na hata hivyo, kutwa alikuwa anacheua. Allergy ni mateso sana.
 
Last edited by a moderator:
Idd amin aliona mbali.! Watu wakamlaaani....sasa wengi wanamkubali kwa hilo.mbaya halisi na wema hakosi.!
Mambo mengine sio ya kutegemea serikali maana kama mtu anawadharau wananchi wa kawaida jua kuwa hata serikali pia anaidharau.
 

Sio wote wanapenda kupiga story safarini. Mimi navaa mask yangu ili nisipige story na Mtu kwenye ndege. Napenda kulala kwenye ndege sio kuongea. Pia sina tabia ya kumkimbilia Mbongo nikisikia Kiswahili safarini au hata kwenye nchi za watu. Siwezi kujua issue yake. Kujuana kijirani sawa lakini sio kindani. Napenda maisha binafsi.
 
ungewauliza kati ya muhindi na muafrika nani ananuka?
 
Inasikitisha na kuhuzunisha kama bado hadi leo kuna vitendo vya kishenzi kama hivyo.
 
Sio wahindi wote wanabagua ....Katika dini ya Kihindu kuna jamii au daraja la watu flani special wanaitwa BRAHIMINS ...daraja la juu kabisa. Hawatakiwa kugusana na mtu yeyote asiye brahimin hata kama ni muhindi. Akifanya hivo anapata dhambi kubwa hata kivuli chako kikimgusa anakuwa amechafuka anatakiwa akaoge ...hawa ni untachable. Wapo hapo mtaa wa kisutu magorofani kibao tu. Ukienda India ndousiseme utayaona mengi, hata kuona wanaoawana wao kwa wao. Wanasali hekalu lao hawachangamani.
 
Na sio wahindi wote niwahindu ....wahindu ni asilimia 80%, kuna Mabudha, Christians, Muslims na dini ya Sikh (Masingasinga) hawa wote wanna hoyo 20% iliyobaki. Kubaguliwa inauma sana nadhani walioko huko nje wanakuelewa unavosema umebaguliwa
 
Tatizo mmezowea kuiba....na wahindi wako makini kulinda mali zao, ndo maana mnawatukana sana

We nae!!! Sasa uwizi unahusiana nini na ubaguzi. Mwizi mwizi na mbaguzi mbaguzi wewe vipi? Sometimes wanaibiwa coz hawana ukarumu.
 

Jambo lililotokea siyo ishu ya kuwa sensitive na harufu, ishu kitendo cha dharau ya moja kwa moja kwa watu weusi, nimejaribu kuelezea vizuri scenario mzima lakini watu wataki kusoma maelezo yote, wanasoma kidogo mwisho wanamaliza kwa kuponda na kuniuliza maswali ambayo tayari nishaelewa kwenye posti yangu ya msingi. Ebu jaribu kupitia nilichoandika halafu utaelewa scenario iliyotokea.
 
Ndio hapo sasa binadamu haandikwi usoni "Mind your own business" wengine hujibu na hao wahindi si ajabu wangeweza kujibu "Hii elevator huwa ina harufu mbaya na kali hivyo kila tukipanda hubana pua" badala ya kuanza kujishuku kwamba wahindi wale wamebana pua kwa sababu Waafrika wananuka.

Sio wote.Mimi ningebana pua ukaanza kuniuliza kwa nini nimebana pua na sikujui ningekujibu kifupi tu,CAN YOU MIND YOUR OWN BUSINESS?
 
Nachukia sana tabia za baadhi ya wahindi,kwanza wanapenda sana upendeleo na rushwa, iwe hosp ama sehemu yeyote yenye kutoa huduma,wao watapenda wapewe kwanza,hawataki kupanga foleni, pili ... ni wabaguzi hatari,kwa tabia hizi nawachukia sana hasa wenye tabia hizo
 


huyo ungesemaje??? kaziba pua???? kila mtu ana maamuzi yake......acha umbulula
 

kuna ambacho kiliwakera
huenda hali ya hewa ilichafuliwa haaaah!!
 
Nilisoma maelezo yako mwanzo mpaka mwisho lakini uliponipa changamoto ya kusoma tena, nikarudia tena mwanzo hadi mwisho lakini sijaona scenario yoyote inayothibitisha maelezo yako!

Kwanza umesema humo kwenye lift alishuka dada mmoja ambae alikuwa amevaa vizuri sana, haya hapa maelezo yako:
...kipindi naingia kwenye lift kuna mdada wa kibongo (alikuwa amevaa vizuri tu) alikuwa anashuka na humo ndani walikuwa wahindi wawili wanawake wamebana pua.
Kumbe, huyo dada aliyekuwa amevaa vizuri sana, wakati anashuka humo ndani kwenye lift kulikuwa na wahindi wameziba pua! Ndo maana nikakuuliza, unajuaje kwamba hapakuwa na mtu aliyekuwa amejifukisha manukato yaliyowapa shida? Kama kulikuwa na dada aliyevaa vizuri sana sitarajii dada kama huyo akose kujipulizia pafyumu na kama nilivyosema, kuna watu wana aleji hata manukato ambayo wewe unaona yananukia vizuri! Tokyo40 kwenye post #145 ametoa ushuhuda wake kuhusu mzungu wa ofisini kwao. Binafsi, kuna zile sabuni zinaitwa Detol ( am not sure kama bado zipo coz' sitaki hata kuzikia!). Zile sabuni mie nikiongea lazima nipate ugonjwa wa mafua... nina aleji nazo vibaya mno!
 
Last edited by a moderator:

Tatizo ni kwamba kipindi yule dada waliotoka naye safari moja(up floor), aliposhuka tu nawao wakachia pua zao,dada anashuka na sisi tunapanda tena,ghafla wale wahindi wakabana tena pua!!! Sasa inawezekana vipi ndani ya sekunde ambazo hazidi hata 5, wanuse harufu ya watu wengine tena hapo hapo hyo harufu iwe kali sana,kiasi ambacho wameshindwa hata kuvumilia. kuachia pua baada ya dada kushuka,maana yake ile kero ilikuwa imeisha. Kubana pua ghafla maana yake ile kero imerudi tena.!!!
 
Last edited by a moderator:
baadhi ya wahindi huwa wana mafua yasiyoisha, labda walishika pua ili kizua wasiwaambukize nyie,
 
anti sina uhakika na hoja ya huyu jamaa Huck sababu ubaguzi wa wahindi ni blaaa
SISI WAAFRIKA NI WAJINGA SANA. WAZUNGU NA WATU WENGINE WANATUBAGUA KUTOKANA NA RANGI YETU, LAKINI SISI TUNABAGUANA KUTOKANA NA MAKABILA YETU NA SEHEMU TUNAZOTOKA, IMAGINE KILA KABILA AFRIKA LINGEKUA NA KA NCHI YAKE TUNGEKUA NA VINCHI VINGAPI NA TUNGEKUA TUNAPIGANA KILA SIKU ZAIDI YA SASA HIVI.

wachaga acheni ubAGUZI SISI WOTE NI WAAFRIKA, SISI SOTE NI WATANZANIA
 

Ha ha ha ha ha yeleuwiii pole yako wamekutuma mbege nini?ukioa uchagani we ni mnyapara unatakiwa kufanya kazi sasa acha kabisa
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…