Leo ni siku ya nafuu kwa wafungwa vijana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Leo ni siku ya nafuu kwa wafungwa vijana

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Mchaka Mchaka, May 1, 2011.

 1. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #1
  May 1, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Gereza la kazaroho,
  S.L.P.1107,
  MAREKEBISHO,
  .
  Wapendwa wazazi wangu,

  Leo ni siku ya nafuu kwa wafungwa vijana. Nimepewa robo saa ili niwakumbukeni kwa barua. Nami bila ajizi, nachukua fursa hii kwanza kuwaamkieni.

  Pili, napenda niwape muhtasari wa jinsi nilivyo jimezesha kwenye kinywa hiki chenye ulimi wa moto, najinsi hali ilivyo kwenye maskani haya.


  Bila shaka wapendwa wazazi mnaikumbuka vyema ile siku ya mechi ya kandanda baina ya shule yetu na shule iliyopo nje ya mji, shule ambayo haifahamiki hata kwa jina.

  Basi nikweli ndicho kiini, ati sisi watoto wa kitovu cha mji tushindwe na watu tulio waonesha hata njia yakwendea shuleni kwao. Sisi vigogo katika mambo ya aina-aina, licha ya mchezo kama soka.

  Hapo wazazi si mimi tu pamoja na wenzangu wengi tulipandwa na jazba, japo hapakua na muafaka tangu awali wakutenda tulivyo tenda. Ni mbaya, Mwenyezi Mungu atu hurumie. Tulipiga tuliua.


  Wazazi wangu bila shaka nitumiapo neno "vigogo" natumia neno mwafaka, si majigambo kamwe. Wewe mpendwa baba yangu unakumbuka siku nilipo taja 'pesa' ulinichotea bila kuhesabu.

  Nilisema zina takiwa 'Tuisheni' lakini zilizo fika huko zilifika, zingine zilinipatia unga waku bwia na misokoto ya kuvuta. Isitoshe zingine zilinisaidia kuwanasa mapatna kwenye disko, hata walio mkaribia mama kwa umri.

  Hukumbuki siku moja baba ulisema mbele ya pesa hapana kisicho tii amri? Uliniambia hata cheti kizuri cha elimu ya sekondari haki kaidi pesa.

  Baba nilidhani haya ndio mapenzi ya mzazi kumbe nilikua nachemshiwa mzizi wa sumu! Nguvu za mzizi huo ziliimarika pale ulipo nijibu kua walimu 'waonevu' lazima watafutiwe wababe wawashughulikie au mafaili yao yachafuliwe. Tangu sikuile, nilipowaita "aa ticha" nilijihisi najitangazia ushindi. Ushindi au ushinde?


  Mama, unakumbuka siku ile ulipopita ubavuni mwa shule yetu ukitoka sokoni? Uliponikuta nimepiga magoti mbele ya walimu kwa kosa lakuchelewa kufika shuleni, ulifanyaje?

  Ukawatotesha masika ya matusi walimu, kisha ukaninyakua, ukanitumbukiza ndani ya benzi nakuwaacha walimu wale waki fikicha macho kwa vumbi ulilo watimulia. Mama sikuile nilijiona kama malaika anaye paa mbinguni! Unafikiri nini kilitokea baadaye?

  Wenzangu wengine wote waliachiwa mara moja. Na tangu siku ile walimu walisema wana nawa mikono kufuatilia nidhamu ya wanafunzi ati wakidai kwanza kazi waliyo somea niku fundisha watoto madarasani wala siyo kuchunga wazururaji vichochoroni. Sikujua kama mama ulikua unachangia zaidi ya nusu ya nauli yakunifikisha nilipo!


  Nasikia walimu wangu wengi wamehamishwa. Masikini! Ninge wakuta ili niwatake radhi zao. Nasikia wengine wanatishia kuacha ualimu. Kabla ya hapo walimu walikua hawatoshi -je, wakijiuzulu? Lo! hata 'tuisheni' ita kuwepo kweli ? Hata ukiwa na pesa zako ni kazi bure basi!Najua hata wakija walimu wapya itachukua muda mrefu kuwazoea hadi nao wakipokee kiamkizi chetu cha"aa ticha".


  Wazazi hapo nilipo ni kikaangoni.Nakaangwa.Naamini nikirejea huko duniani nitakuwa kijana mpya.Hapa hapana kuchagua la kufanya,wala hapana kushindwa.Ni utekelezaji wa mipango tu.Najua mtataka kuwaita walimu wangu hawa madikteta,lakini mambo ya huku yanakwenda .Tunajifunza mengi kwao,na tunajifunza mengi zaidi tunapokuwa peke yetu.

  Tunawashukuru walimu hawa kwa kututenga sisi wafungwa vijana na maharamia wazoefu,kwani kulikuwa na minong'ono kwamba walikuwa wakitusubiri kwa hamu kubwa,Sikujua kwanini!
  Lakini shukrani zaidi ziwaende wabunge,kwani yasemekana ndio walioanzisha kilio cha utaratibu huu.


  Wazazi wangu,naomba mkiniandikia mnijibu haya:

  Je, mautingo wa daladala bado wanawasukuma wanafunzi nje ya mabasi yanayokimbia? Je,wauza unga na bangi bado wapo?

  Je,wazazi bado hamjaelewana na walimu shuleni?

  Je,yale magazeti yenye lugha ya sumu bado yanaaminiwa?

  Mambo haya yananiogofya, kila nikiyawaza naona kama yananitafutia tiketi yakurejea kwenye mdomo wa mamba.


  Wasalam,

  Mtoto wenu.
   
 2. Cestus

  Cestus JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 1,000
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  *shakin head*
   
 3. simba29

  simba29 Senior Member

  #3
  Jul 19, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 173
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Dogo . . .veri gudi!
   
 4. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Majuto ni mjukuu, we endelea tu kusota hadi gereza libomoke ..,utakula jeuri yako
   
 5. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,152
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Jichunge tu huko wasije kukuomba tigo
   
Loading...