Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,575
Kusema ukweli huenda nchi hii ina mambo mengi sana kiasi kwamba hata yale masuala ya muhimu ya kutuunganisha kama Taifa huwa hatuyakumbuki tena kirahisi.
Leo ni siku ya kuwakumbuka mashujaa wa Taifa hili , kuna haja ya sisi pia kukumbushana masuala muhimu ambayo yamepelekea uwepo wa Taifa hili na mashujaa wetu waliokuwepo kipindi hicho.
Pamoja na ukweli kuwa Historia ya Taifa hili imepotoshwa na inataka kuandikwa kuanzia pale alipoanzia Mwalimu ila naamini kuna haja ya kuiandika vizuri historia yetu kwa faida za kizazi kijacho.
Napenda kuweka maswali haya ili tuweze kujadili na kupatiana majibu juu ya siku hii.
1. Hivi hawa mashujaa tunaowakumbuka tunawakumbuka kwa sababu gani haswa?
2. Hivi hawa mashujaa ni wakina nani ? walifanya nini hadi wakumbukwe?
3. Hivi siku ya leo ama tarehe hii 25-07 ina historia gani kwenye Taifa hili la Tanzania?
4. Hivi sikuku hizi zinawahusu pia upande wa pili wa Muungano?
5.Kuna haja ya kuwa na hii sikukuu?
6.Nini maana ya kiongozi mkuu kuweka zile zana za kale kama upinde?
7.Kwa nini mkuu wa majeshi huwa anaweka sime kwenye makaburi yale?
8.Sherehe hizi zilianza kuadhimishwa mwaka gani?
Nauliza maswali haya yote kwani najua kuwa vijana wengi wanajua kuwa baba wa Taifa ni Nyerere, sasa ni kwa nini hawa mashujaa wasingekuwa ndio mababu wa Taifa?