Leo ndio ilizaliwa Tanzania

Ndio maana niliwahi kusema huko nyuma kuwa Jumbe anazo akili sana ndio maana alipoona mambo ya kuburuzwa tu akaamua kuweka mguu chini, akaishia kuwekwa pembeni!

Kaka,

Lazima usome Pan-Africanism or Pragmatism? Lessons of Tanganyika-Zanzibar Union. Issa G. Shivji. Yeyote anaekuja kutoka Tanzania akuletee tafadhali. Hutaamini Jumbe, licha madhaifu yake, kwenye suala la Muungano aliweka mguu kweli kweli.
 
Wakati tunajaribu kufikiria kuhusu Muungano wetu, tujiulize kwanza ni muungano upi duniani ambao ni mkamilifu kabisa na ambao hauna kasoro a.k.a kero? Ni nchi gani zilizoweza kuungana na ambazo uhusiano kati yake si vitu vinavyozungumzwa.

Binafsi naamini ile hali tu ya kuzungumzia kasoro na jinsi ya kuzitatua inaonesha kuwa muungano wetu unazidi kukomaa siku kwa siku. Ninaamini tungekuwa mbali kama tungeamua kukaa siku moja na kusema "ok, nini hasa matatizo ya muungano?" na kwa kiasi kikubwa tuyashughulikie yale makubwa kwanza (ya Kikatiba) halafu tushughulikia yale ya utendaji na mambo madogomadogo. Lakini kwangu la msingi ni kukaa chini na kuangalia Muungano unakwazwa wapi Kikatiba na lipi tunaweza kulishughulikia mara moja na lipi tunaweza kulipa muda.

Njie pekee ya kuwa na Muungano kamili usiokuwa na matatizo ni dissolution of former nations into a single political entity. Hakuna cha mawaziri wakuu wawili, serikali mbili au tatu n.k vinginevyo hatuna budi kukaa chini na kuona ni muungano gani ambao utakuwa as perfect as possible?
 
Kaka,

Lazima usome Pan-Africanism or Pragmatism? Lessons of Tanganyika-Zanzibar Union. Issa G. Shivji. Yeyote anaekuja kutoka Tanzania akuletee tafadhali. Hutaamini Jumbe, licha madhaifu yake, kwenye suala la Muungano aliweka mguu kweli kweli.

alaaaa ,kumbe upo???mkulu khabri za usa???
 
Wakati tunajaribu kufikiria kuhusu Muungano wetu, tujiulize kwanza ni muungano upi duniani ambao ni mkamilifu kabisa na ambao hauna kasoro a.k.a kero? Ni nchi gani zilizoweza kuungana na ambazo uhusiano kati yake si vitu vinavyozungumzwa.

Binafsi naamini ile hali tu ya kuzungumzia kasoro na jinsi ya kuzitatua inaonesha kuwa muungano wetu unazidi kukomaa siku kwa siku. Ninaamini tungekuwa mbali kama tungeamua kukaa siku moja na kusema "ok, nini hasa matatizo ya muungano?" na kwa kiasi kikubwa tuyashughulikie yale makubwa kwanza (ya Kikatiba) halafu tushughulikia yale ya utendaji na mambo madogomadogo. Lakini kwangu la msingi ni kukaa chini na kuangalia Muungano unakwazwa wapi Kikatiba na lipi tunaweza kulishughulikia mara moja na lipi tunaweza kulipa muda.

Njie pekee ya kuwa na Muungano kamili usiokuwa na matatizo ni dissolution of former nations into a single political entity. Hakuna cha mawaziri wakuu wawili, serikali mbili au tatu n.k vinginevyo hatuna budi kukaa chini na kuona ni muungano gano ambao utakuwa as perfect as possible?

Leo tunapozungumza, Scotland inataka kujitenga toka The United Kingdom. Juzi juzi wamepewa Bunge lao na Waziri Kiongozi wao (wanaita wenyewe First Minister). Hivyo ni kweli, hakuna muungano ambao hauna kero. Lazima ziwepo.

MwanaKijiji, suala la kuvunja vinchi vinavyoungana na kuwa na Nchi moja ni suala la kimjadala. Mjadala wenyewe utaongozwa na 'mapambano ya kifikra'.

Ninaamini katika kutoa fursa kwa 'minority' na hivyo kuwa na mfumo unaotoa uhuru kwa vinchi vilivyojiunga kujiendesha katika masuala yasiyo ya Muungano . Ninaamini mfumo huu ni endelevu zaidi kuliko kuwa na mfumo ambao ni 'too central. Serikali moja ya Muungano kwa Tanganyika na Zanzibar ni jambo jema sana, lakini ninaogopa kuwa 'minority' watamezwa na 'majority'. Kwa attitude ninayoiona ya sisi watu wa Tanganyika kwa Wazanzibari, watamezwa na kubinywa kweli kweli. Mwalimu Nyerere aliliona hili katika fikra zake na hata alionya katika Kitabu chake cha Uongozi wetu na Hatma ya Tanzania. Changamoto kubwa ni kuwa na mfumo wa Muungano ambao hautapelekea wasaliti wachache kwa tamaa zao kuuvunja. Mfumo wa sasa haupiti jaribio la uendelevu. Mabadiliko ya kisiasa yatakayopelekea chama tofauti na CCM kushika madaraka kokote ama Zenji au Bara, yaweza kuuweka muungano katika matatizo makubwa. Tujadiliane ili tuwe na mfumo utakaovuka viunzi hivyo.
 
kwa hio dodoma walikataa muafaka kwa kuulinda muungano?
 
Nitoe wazo jingine:

Kuna ubaya gani wa kuwa na Serikali moja kuu (Rais, Makamu, na Waziri Mkuu na Baraza moja la Mawaziri) halafu mnakuwa na Mabaraza ya Wawakilishi katika pande zote za muungano na kuwa na Gavana wa pande zote mbili ambaye anasimamia Maeneo huru (Bara na Zanzibar)? Hivyo kimsingi unabakia kuwa na serikali mbili (Provincial na Union) Na mahusiano na ni kati ya serikali ya province na ile ya muungano. Na kuna mahusiano yanayohusu interstate. Kimsingi ni kama mfumo wa Marekani ambapo haziko serikali 50 (in fact they are) lakini kimahusiano ni serikali mbili FEderal na State (regardless of the number of states).

Mfumo wa namna hii utakuwa mzuri sana hasa kama tutaamua kuungana na Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
 
Mimi naona hata kuwe na mfumo gani bado kuna wale ambao wataunung'unikia hususan kama hali ya kiuchumi sio nzuri (which is and always will be the case). Halafu ukileta na Kenya, Uganda, Rwanda, na Burundi kwenye equation...hapo ndio kabisaa....matatizo makubwa yanakuwa inevitable.
 
Jana nilimsikiliza Prof. Kabudi kwenye "This week in perspective" ya TBC1

Alisema yafuatayo nanukuu

"... hata mimi nilikuwa napenda kuwe na serikali tatu, lakini baada ya kuangalia mazingira halisi ya wakati huo na hata ya sasa kwa kweli nadhani serikali mbili ndio muafaka..."

Alimaanisha hivi... wakati wa Muungano... Population ilikuwa 300 Zanzibar, na Tanzania bara 11Mil.

Sasa 1m Zanzibar, na Bara 37mil... alisema kwamba kusema kuwa na serikali tatu maana yake ni duplication ya serikali ya jamhuri hasa kwa Tanzania Bara, kwa maana already serikali ya Jamhuri... above 90% ni Tanzania Bara.... Ni hekima ya kuifanya serikali ya Bara iwe ndani ya muungano...

Nadhani tunajidili mengine kwa muundo tuuache kama ulivyo!Tuacheni siasa sasa uchumi tu basi.
 
Nitoe wazo jingine:

Kuna ubaya gani wa kuwa na Serikali moja kuu (Rais, Makamu, na Waziri Mkuu na Baraza moja la Mawaziri) halafu mnakuwa na Mabaraza ya Wawakilishi katika pande zote za muungano na kuwa na Gavana wa pande zote mbili ambaye anasimamia Maeneo huru (Bara na Zanzibar)? Hivyo kimsingi unabakia kuwa na serikali mbili (Provincial na Union) Na mahusiano na ni kati ya serikali ya province na ile ya muungano. Na kuna mahusiano yanayohusu interstate. Kimsingi ni kama mfumo wa Marekani ambapo haziko serikali 50 (in fact they are) lakini kimahusiano ni serikali mbili FEderal na State (regardless of the number of states).

Mfumo wa namna hii utakuwa mzuri sana hasa kama tutaamua kuungana na Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Ule wako Maalimu Seif na Abeid Aman Karume na Viongozi wa juu wa vyama vya siasa Zanzibar wakusikie...

Hakuna tatizo la muungano kwa wananchi, tatizo ni viongozi... angalia uwakilishi wa Zanzibar unavyotisha watu 4,000; wana mbunge. mwakilishi, masheha kibao, wakuu wa wilaya mikoa etc..
 
Nitoe wazo jingine:

Kuna ubaya gani wa kuwa na Serikali moja kuu (Rais, Makamu, na Waziri Mkuu na Baraza moja la Mawaziri) halafu mnakuwa na Mabaraza ya Wawakilishi katika pande zote za muungano na kuwa na Gavana wa pande zote mbili ambaye anasimamia Maeneo huru (Bara na Zanzibar)? Hivyo kimsingi unabakia kuwa na serikali mbili (Provincial na Union) Na mahusiano na ni kati ya serikali ya province na ile ya muungano. Na kuna mahusiano yanayohusu interstate. Kimsingi ni kama mfumo wa Marekani ambapo haziko serikali 50 (in fact they are) lakini kimahusiano ni serikali mbili FEderal na State (regardless of the number of states).

Mfumo wa namna hii utakuwa mzuri sana hasa kama tutaamua kuungana na Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Mzee Mwanakijiji, heshima yako!

Unasema kama tutaamua kuungana na Kenya, Uganda, Rwanda, na Burundi? haya ni mawazo ya raia kama mimi na wewe, ambao tuna nia ya kushirikiana na ndugu zetu, na hatuoni matatizo yoyote ya kutawaliwa na Rais mmoja. Ebu fikiria mkutano wa kufikirika kati ya Museveni, Kikwete, na Kibaki. Ikiwekwa mezani kuwa hizi nchi ziungane, wazo kubwa vichwani mwa hao watu watatu ni nani awe Rais miongoni mwao. Hoja itakufa pale pale.

Museveni ameingia madarakani kwa mtutu wa bunduki, na inavyoonekana ndivyo atakavyotoka. Anajiona yeye peke yake ndiye bora kuwa Rais kuzidi mtu mwingine yeyote. Ameshawishi uvunjaji wa katiba ili aendelee kutawala. Anaweza kumwambia Kikwete na Kibaki kuwa tuungane na Rais awe Kibaki au Kikwete? atataka awe yeye au hakuna Muungano, au Muungano uwepo na yeye aendelee kuwa Rais wa Uganda.

Vivyo hivyo kwa Kibaki. Ameshindwa uchaguzi lakini amejiapisha na kutwaa tena madarakani juu ya damu za raia anaotaka kuwalinda. Kikwete amejiandaa miaka kumi kuchukua madaraka na ameingia kwa kuteketeza mamilioni ya fedha za wananchi kwa mgongo wa kuwaletea maisha bora. Nani kati ya hawa viongozi watatu atamfuata mwenzake na kutaka nchi zao ziungane, huku akitambua kwamba katika Muungano anaweza kupoteza madaraka yake? Matokeo yake, tunaambulia miundo ya miungano inayolinda madaraka ya viongozi, badala ya kulinda maslahi ya wananchi.

Lakini angalia, Wakenya wanafanya biashara Tanzania, na Watanzania wako Kenya wanafanya biashara. Mabasi ya kutoka Dar kwenda Mwanza na Bukoba yanapitia Kenya na Uganda. Watanzania, Wakenya, na Waganda walioko nchi za nje, hawakuwa na matatizo yasiyokuwa na vichwa wala miguu. Mwaka juzi tu Kikwete alikutana na Bush kuteta, na katika hali ambayo haieleweki, Wakenya wakadai Kikwete alimwongelea vibaya Kibaki. Sasa angalia Wakenya wanavyotukanana na Watanzania kwenye mitandao.

Mgogoro wa Burundi ni wa Watusi na Wahutu. Mgogoro wa Rwanda ni wa Wahutu na Watusi. Ilifikia mahala yakawepo mapendekezo kwamba, ili kutatua migogoro ya aina hii, inabidi Watusi wote wapelekwe Rwanda na Wahutu wote wapelekwe Burundi ili kila kabila lijitawale, liwe na Rais wake, kwa sababu inajulikana kuwa tatizo ni madaraka (mlo). Ilifikia mahala kuwa hata nchi kama Somali ambayo haina kabila, ila kuna koo, au Ethiopia, zitengwe katika vibaba ili kila kibaba kiwe na Rais wake.

Angalia Urusi ilivyosambalatika. Msambalatiko unaendelea na itafikia mahala hata zile zilizodhaniwa kuwa ni nchi, zitagawanyika katika vibaba au koo, na kila ukoo utataka kuwa na bendera, wimbo wake wa taifa, na Rais wake. Sababu ya yote haya ni madaraka, na raia baki wanachochewa na kuingizwa katika mkumbo. Kwa nini tuige mifano ya nchi au makundi ya watu wanaojigawa? Vilevile sioni sababu yakuiga mifano au makundi ya watu wanaoungana. Kwa nini tusiangalie asili yetu nini?

Hizi hoja za kumezwa na kupoteza utaifa sijuhi mantiki yake nini hasa. Yaani leo inaaminishwa kuwa Mmasai wa Tanzania akiungana na Mmasai wa Kenya, wote wawili watapoteza utaifa wao? Ebu nipe historia ya utaifa wa Mmasai? Ukweli ni kuwa, hili kabila moja la kimasai, lenye mataifa mawili ya Tanzania na Kenya, likirudi katika hali yake ya asili, halipotezi utaifa wake, kinachopotea ni madaraka ya watawala wa Tanzania na Kenya. Hilo ndilo tatizo letu wakati wa kutafuta muundo wa Muungano ambao ni muafaka. Hili sio tatizo la Afrika tu, bali dunia nzima.

Hivi kabla ya ukoloni, watu wa Afrika walikuwa wamemezwa na nani? huu woga wa kumezwa unatoka wapi? Serikali ya Tanganyika iko wapi? Nitajie makamu wake au Rais wake. Kwa hiyo inakubalika kwa Serikali ya nchi kubwa kama Tanganyika "the majority" kumezwa ndani ya Serikali ya Muungano wa Tanzania, lakini haikubaliki kwa nchi ndogo kama Zanzibar "the minority" kumezwa ndani ya Serikali ya Muungano.

Umetoa mfano wa Marekani, lakini hata Rais wa Texas, Samwel Houston, alikuwa na mawazo kama haya haya, kuwa eti Texas ni nchi ndogo ingemezwa na Marekani. Lakini kilichojulikana, na ambacho kinajulikana mpaka leo, ni kuwa Rais Houston, na kama walivyo wanasiasa wengine, aliweka mbele hatima ya madaraka yake, kuliko hatima ya jinsi raia wa Texas ambavyo wangenufaika na Muungano. Hivyo, maamuzi ya hatima ya muungano wao hayakuachwa mikononi mwa Rais Houston.

Toka nchi ya Texas "the minority" na nchi ya Marekani "the majority" ziungane, ilichukuwa muda mrefu kabla hata ya kutoa Rais wa Marekani. Raia wa Texas hawakupoteza utamaduni wao, asili yao, na kadhalika. Sasa hivi wanafaidi matunda ya Muungano. Kuwapa watu madaraka sio lazima kuwa na Serikali za majimbo.

Ni kitu gani ambacho Rais wa Zanzibar anashindwa kukifanya ila kinaweza kufanywa na Waziri Mkuu wa Zanzibar? Alafu hii hoja ya kuwa wakati Muungano unaundwa, lengo lilikuwa kuwa na Serikali tatu, Aboud Jumbe amelitoa wapi? Mbona katika ukurasa 4 wa Kitabu cha Uongozi wetu na hatima ya Tanzania, imeandikwa kwamba waasisi hawakutarajia kuwa na Serikali tatu au moja? Jumbe na Nyerere nani mkweli?
 
Jana nilimsikiliza Prof. Kabudi kwenye "This week in perspective" ya TBC1

Alisema yafuatayo nanukuu

"... hata mimi nilikuwa napenda kuwe na serikali tatu, lakini baada ya kuangalia mazingira halisi ya wakati huo na hata ya sasa kwa kweli nadhani serikali mbili ndio muafaka..."

Alimaanisha hivi... wakati wa Muungano... Population ilikuwa 300 Zanzibar, na Tanzania bara 11Mil.

Sasa 1m Zanzibar, na Bara 37mil... alisema kwamba kusema kuwa na serikali tatu maana yake ni duplication ya serikali ya jamhuri hasa kwa Tanzania Bara, kwa maana already serikali ya Jamhuri... above 90% ni Tanzania Bara.... Ni hekima ya kuifanya serikali ya Bara iwe ndani ya muungano...

Nadhani tunajidili mengine kwa muundo tuuache kama ulivyo!Tuacheni siasa sasa uchumi tu basi.

Hapatakuwa na duplication hata kidogo. Hapatakuwa mwingiliano wa kazi za serikali kwani kila serikali itakuwa na majukumu yake. Mfano serikali ya muungano haitajihusisha na Kilimo. Hapatakuwa na Wizara ya Kilimo katika muungano, kwa mfano. Vile vile hapatakuwa na Wizara ya Mambo ya ndani ya Tanganyika au ya Zanzibar. Duplication gani hapo?
 
Nawapongeza Watanzania wote kwa kuadhimisha miaka 44 ya Muungano... Si haba mafanikio ni mengi kwa kuwa!

1. Utaifa upo... hakuna anayejitambulisha kama mZanzibar au mTanganyika nje ya mipaka yetu. na hata ndani ni kwa nadra.

2. Watu wamechanganyika! Idadi kubwa ya Watanzania hawajui hata Tanganyika ilikuwa je...

3. Ikumbukwe kwamba Tanyanyika huru ilidumu kwa muda mfupi sana... yaani December 1961 hadi April 1964.

Changamoto...

Muungano wetu umekuwa wa kisiasa na Kijamii zaidi...

Kwa sasa tunapenda uwe ujikite kiuchumi...yaani zanzibar ianze kuwa na viwanda vidogo vidogo iachane na kutegemea Utalii tu... kwa kuwa hii ni hatari..
Umezungumza maneno mazito sana , WaZanzibari hawajitambulishi kama WaTanzania hilo nakupa changamoto utafute ni wapi WaZanzibari wanajitambulisha kama WaTanzania ?Mpaka aulizwe kwa mara ya pili au tatu na huenda yakatokea mabishani nakumbuka kesi moja ilitokea Marekani katika Ubalozi wa Tanzania ,Mzanzibar aliandika kazaliwa Zanzibar ubalozi ukamtaka abadilishe aandike Tanzania hapo ikawa vita ya kwanza ya Dunia ,jamaa hakukubali kabisa na alishinda vita hiyo.
Hivyo hivyo utaona katika nchi za nje Wazanzibari wanakuwa na mkusanyiko wao ambao wanakuwa na ofisi club zao kwa jina la Zanzibar mfano Canada Uingereza na Uarabuni huko kote wanajiita WaZanzibar tena hushiriki katika sherehe kwa kutumia nembo hiyo ya Zanzibar. Ila waTanganyika wanaona aibu kujitokeza kwa jina la Nchi yao Tanganyika ,sasa mvutano upo kati ya balozi za Tanzania na kundi hili au na watu hawa wa kutoka Zanzibar.
Usiseme idadi kubwa hawajui ,itakuwa unajidanganya WaZanzibari wanaifuatilia historia ya nchi yao ndio maana hata kwenye vita vya siasa utasikia bado wana historia ya kutoelewena tokea zamani au tokea mfumo wa vyama vingi uanzishwe Zanzibar ,wanakwambia vyama vingi vilianzia kwao demokrasia ilianzia kwao,tV ya rangi ilianzia kwao,nyumba za gorofa zilianzia kwao Umeme ulianzia na hiyo kwa Afrika nzima sio Tanganyika ila nawashangaa kwa yote hayo yalioanzia kwao bado leo hii ni wa mwisho.
Pwoit yako ya tatu ,mimi sikubaliani kwani naamini hadi hii leo Tanganyika ipo ila wenyewe wamekwenda kufuatilia Muungano ,hakuna kifungu kinachosema Tanganyika imeondolewa na pia hakuna kifungu kinachosema serikali ya Tanganyika iliwajibishwa au ilivunjwa ,kwa maana hiyo serikali ipo ila imekwenda likizo lini itarudi ndio haijulikani.
 
Muungano ni muhimu kwa ajiri ya kuondoa matatizo yanayoweza kuletwa na wazanzibar kwa Tanganyika, Zanzibar jinsi ilivyo siku ambayo inajitenga na Tanganyika, pemba nao wanatangaza uhuru wao, hii italeta matatizo makubwa kwani watawara wa zanzibar (wafalme) hawatakubali watatumia jeshi kukirejesha kisiwa mikononi mwao. unaweza kuona jinsi gani serikali ya tanganyika itakavyokuwa na kazi.
 
Heshima mbele wanaJF
UDINI ni chanzo kikubwa kabisa cha matatizo muyaonayo ndani ya hiri ri-MUUNGANO.
Udini unatugawa kwa rikasi ra ajabu sana,chini kwa chini,ni ngumu sana kurecognize dariri zake,siku ikifika mutakaa midomo wazi.
 
Kyoma na Kamundu,
Wakuu habari za masiku na hasa Kyoma karibu sana... maneno yenu nimeyasikia wakuu somo zito kama Zitto mwenyewe.

Kwanza kabisa namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kuujalia Muungano wa nchi zetu, pamoja na matatizo yote yaliyotokea na ambayo yanaendelea kuwepo lakini kwa rehma zake nina hakika siku zinakaribia kuweza kutatua matatizo haya.
Kwa sehemu kubwa ya maelezo ya Zitto nakubaliana naye sana tu na hasa muundo wa Uongozi ambapo Tanzania itakuwa na Majimbo mawili - Bara na Visiwani. Nami pia sintape ndekeza kuwepo kwa marais wawili huu ni mfumo butu wenye kuumiza zaidi na umepitwa na wakati, kisha hata sintapenda kusikia jina la Tanganyika kwa sababu jina hilo lina historia ndefu sana ikiwa ni pamoja na kuziunganisha nchi za Rwanda na Burundi hivyo inaweza kunipa picha ya kuweka madai ya nchi hizo kuwa sehemu ya Tanganyika. Maadam tulisha amua kuua jina la Tanganyika basi ni bora kuzaliwa kwa jimbo jipya la Bara ambalo litakuwa na serikali zake ndogo ya Kijimbo sawa na ile ya Zanzibar isipokuwa sioni nafasi ya rais wa Zanzibar ama Bara...
Nachotofautiana na ndugu Zitto na wasomi wengine akina Prof. Shivji ni pale wanaponukuu Muundo wa Muungano wetu na kuutazama kama vile tumeungana jana na hiyo katiba imetungwa juzi tu. Jamani ni miaka 44 toka tuungane na sababu za Muungano huo haziwezi kuchukuliwa kirahisi kwa sababu leo hii tupo ktk mazingira tofauti kabisa.

Tukumbuke tu kwamba mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa muhimu pamoja na kwamba kuna siri kubwa ya Mapinduzi hayo ambayo hadi leo imekuwa ikifichwa na serikali yetu..
Hadi leo haijulikani nafasi ya kina Abdoulrahmani Babu na wanachama wa Umma party ambao kwa kiasi kikubwa ndio walikuwa karibu zaidi na Okello ambaye kumbe kutokana na historia aliwahi kuishi na kufanya kazi Zanzibar..
Pamoja na matukio yote yaliyotangulia ni muhimu hawa wasomi wetu waelewe kwamba Zanzibar iliyopinduliwa haikuwa salama hata kidogo na Muungano ule ulikuwa na malengo ya Muda. hapo nakubaliana na Jumbe ambaye hasemi wala hapingi Muungano huo isipokuwa yale yaliyofuatia..
Hivyo kina Shevji kusema:- Constitutionalism and Democracy were least respected both in the formation of the Union...
Hapa kashemsha kwa sababu hakuna muungano wowote unaofuata demokrasia ktk formation ya muungano huo isipokuwa sababu za kuunda Muungano huo ndizo zinaweza kuvuta kipengele cha demokrasia ikiwa swala national security halina uzito badala yake ni vitu kama nguvu ya Kiuchumi..Kwa hiyoi uzito wa national security hauhitaji ushauri wa wananchi wala wanasheria ikiwa usalama huo upo matatizoni..Hiyo mwanzo.

Lakini pale alipoongezea neno - And its continued existence! - hapa ndipo napokubaliana naye kwa sababu katiba ya muungano huo ilikuwa ni ya Muda ku secure Mapinduzi. Hivyo narudi kwa Jumbe kwamba hapa ndipo utata mkubwa unapojiingiza kwamba baada ya Mapinduzi kuwa safe na national security tukokuwepo na threats toka nje na ndani, ilitakiwa marekebisho makubwa ya katiba ya Muungano ambayo inge deal na hali tuliyofikia kwa faida ya wananchi wote wa Pande mbili..
Na kwa hakika sisi sote tunajaribu kuepuka the real issue ya Muungano huu kwa kuvuta yale tuliyotangulia hali problem kubwa ya Muungano wetu ni hali iliyopo sasa hivi Kikatiba. Who cares mtoto alizaliwa ktk mazingira gani?... hata Yesu inasemekana alizaliwa ktk zizi la mbuzi sijui Kondoo lakini baadaye kaja kuwa mbora wa viumbe wengi waliozaliwa ktk mahekalu.
The real issue ya muungano wetu ni makuzi yake ambapo katiba ile iliyoundwa kwa muda imechukua uhai wa kudumu! Katiba ile ya kiulinzi inawapa security sasa hivi baadhi ya viongozi na hasa wale wa wenye asili na Afroshiraz na pengine kuvchukua hatua nyingine kulinda Chama cha Mapinduzi..

Hivyo basi kama tulivyoondokana na Ujamaa kuingia mapinduzi ya kiuchumi na kukubali hali halisi ya Utandawazi inabidi Tanzania tuondokane na zile ndoto za security na hivi sasa na kuutazama Muungano huo kwa kutumia darubini za KIUCHUMI..
Na hapo bnila shaka tutapata solution kirahisi zaidi badala ya kuendelea kutazama nyuma kumtafuta mchawi hali wachawi ni sisi wenyewe kuendelea kuitukuza katiba yenye malengo tofauti na hali halisi tunayo face....
 
Kyoma,

Asante kwa maoni yenye maswali mengi sana. Jambo moja la kuzingatia ni kuwa tumeungana tukiwa tayari tumepata uhuru kila nchi kivyake. Hivyo hali ya utaifa na kumezwa kwa identity inaingia hapo. Mfano wa Wamasai huwezi kueleza hali ya Taifa la Zanzibar kwani wamasai sio Taifa na hawajawahi kuwa Taifa. Vile vile wachaga, wagogo na wale wote waliokuwa ndani ya Tanganyika mara baada ya Uhuru. Mwalimu alipokea makabila ndani ya territory ya Tanganyika. Baada ya tarehe 9 disemba ndio tukawa Taifa na tukafanya kaiz ya kujenga Taifa la Tanganyika kabla hatujaanza kujenga Taifa la Tanzania baada ya Muungano mwezi April, 1964. Kama mkoloni angeamua kuipa uhuru Kilimanjaro na baadae Kilimanjaro ikaja kuungana na the rest of Tanganyika tatizo la minority na majority tunalolizungumza kuhusu Zanzibar leo lingekuwapo. Ndio maana Wazanzibar wanapozungumzia Muungano wanazungumza kama Wazanzibar, Taifa la Zanzibar. Lakini nao pia wana makabila yao. Hii ndio hoja ambayo Mwalimu alikuwa akiitoa kuhusiana na Shirikisho la Afrika Mashariki. Akijenga hoja kuwa Mataifa haya ukishayapa uhuru kabla ya muungano, itakuwa tabu kuungana. Mpaka leo Hakuna muungano wa Afrika Mashariki.

Suala la minority vs majority halikwepeki katika the question of the union kwa sababu wakoloni walikwishatugawa na kupewa nchi mbili ambazo baadae ziliungana kama Mataifa huru mawili, wajumbe wa UN na OAU. Kumbuka Zanzibar ililipa ada ya UN kwa miaka 40 ambayo nasi tukaja kuirithi kama Tanzania. Lilikuwa ni Taifa.

Kwamba Muungano ulimaanisha serikali tatu. Siwezi kusema ni nani mkweli kati ya Jumbe na Nyerere. Wote waweza kuwa wakweli kutokana na maoni yao. Wote wapia waweza kuwa waongo kutokana na tafsiri zao za mambo. Ila kumbuka tu kuwa arrangement ya sasa ya Muungano ilikuwa ni ya muda na ndio maana 1964 Katiba ilikuwa ni articles of the Union. Baadae Katiba ya Tanganyika ikafanyiwa marekebisho kidogo kuwa Katiba ya Muda ya Muungano na kudumu mwapa 1977 tulipotunga (kwa muda wa masaa 3 kukiwa na wachangiaji 4 tu) katiba ya Muungano ya kudumu. Hapa ndipo matatizo ya Jumbe na Mwalimu yalianza na kuishia mwaka 1984 kwa Jumbe kujiuzulu nyadhifa zake za uongozi.

Tuendelee na mjadala
 
Huu mjadala unanikumbusha mzee wa hoja, Mzee Mkandara (simsikii siku hizi). Aliwahi kutoa mfano wa ndoa; kwa maana kwamba, ili ndoa iwe imara, mke na mme warudie katika hali zao za uchumba (kulinda identity ya mke na mme). Ili isije ikaonekana wote wawili wamemezwa katika ndoa yao, inabidi wafufue na kulinda haki zao walizokuwa nazo kabla ya ndoa. Haki zenyewe, mojawapo ni kila mtu kumrudia mchumba wake wa zamani (girl & boy friends).

Kuna wanaosema, ili Muungano uimalike na uweze kudumu, basi Zanzibar iwe na identity yake. Yaani iwe na wimbo wake wa Taifa, Bendera yake, nakadhalika. Vivyo hivyo kwa Tanganyika. Siku timu ya taifa ya Zanzibar na Tanganyika zikimenyana, timu ya Zanzibar itapigiwa wimbo wake wa taifa tofauti na wimbo wa taifa itakaopigiwa timu ya Tanganyika. Baada ya hapo utapigwa wimbo wa Taifa wa Tanzania.

Watanganyika watapepelusha bendera ya Tanganyika kushangilia timu yao, na Wazanzibari watapeperusha bendera ya Zanzibar kushangilia timu yao. Katika hali ya namna hii, sijuhi nani atapeperusha bendera ya Tanzania. Watu wa nanma hii wanataka tuamini kwamba, kurudisha "identity" ya Tanganyika na Zanzibar ndani ya Muungano wa Tanzania, ndiko kuimarisha Muungano.

Wakati Tanganyika inaundwa na Wazungu huko Ujerumani, kuna vikabila vidogo sana na makabila makubwa. Vivyo hivyo Kenya na Uganda. Sikuwahi kusikia kelele kuwa Wamasai walimezwa na Wakikuyu. Au Wazahanati wamemezwa na Wasukuma. Nadhani labda, kama Wazaramo wangeulizwa kabla ya kuunda Tanganyika, wangetoa hoja kama zinazotolewa leo.

Hakuna Mtanganyika aliyeulizwa, hivyo, hatuwezi kuongea tena mambo ya makabila au himaya, kwa sababu tulikwisha kuundiwa nchi na kupewa. Tuliambiwa kuwa hiyo nchi tuliyopewa ina "identity" ambayo hatutakiwi kuipoteza. Hili ndilo linanipa wasiwasi kubwa. Ukitaka kuhoji chimbuko hasa la hiyo identity ya Tanganyika, hakuna jibu la maana, zaidi ya kwamba ndivyo tulivyo pewa.

Afrika tumefikia mahala paya sana. Tulianza na Marais wa maisha (kamuzu na Mobutu). Wakaja Marais waliounasa kwa mtutu wa Bunduki (Doe, Museveni, Kagame, Habyarimana, Sankara, ..........). Sasa imekuja staili nyingine ambayo ni tishio. Viongozi wanaposhindwa kwa kura, hawataki kutoka madarakani. Inavyodhaniwa, alianza Salmin Amour 1995. Akafuatia Kibaki, na sasa Mugabe.

Wote hawa walichochea makundi ya watu na kupata wafuasi wa kutosha wanao waunga mkono. Kama ambavyo mapinduzi hayakuanza kwa mkupuo, kwani ilianza nchi moja, ikafuatiwa nyingine, na zilizofuata zikaendelea kujifunza mpaka kiama, ndivyo ambavyo mtindo wa kushindwa na kug'ang'ania madaraka unavyoanza kupokelewa vizuri miongoni mwa watawala. Sio kweli kwamba viongozi wa Afrika hawaoni tatioz Zimbawe, bali wanajifunza mbinu, ndio maana wako kimya.

Sasa inaeleweka wazi, kama ilivyotokea Kenya, kwamba viongozi wa Afrika wanaweza kufanya ufisadi wote wanaoutaka bila kutiwa hatiani. Lakini ikitokea wakashindwa uchaguzi, hawatakubali kutoka, kwani yatatokea mazungumzo ya kumkutanisha aliyeshindwa kihalali na aliyeshindwa kimizengwe, ili waunde Serikali ya umoja wa kitaifa na waendelee kulinda ufisadi wao.

Hilo sio tatizo kubwa sana. Wasiwasi wangu ni kuwa, ili hali ya namna hii iweze kutokea; yaani Kibaki aweze kuwa na wafuasi, na Odinga aweze kuwa na wafuasi, na Mugabe aweze kuwa na wafuasi, na Salmin aweze kuwa na wafuasi, na Maalim Seif aweze kuwa na wafuasi, lazima ziwepo mbinu za makusudi za kuwachochea raia na kuwagawa katika mafundo, ili hata kama mtu wao akishindwa, basi wawe tayari kufa ili kumlinda.

Kwa hiyo, raia wanatumiwa kama siraha. Kibaki akikataa kutoka madarakani, watu wanauana kwanza mpaka kinaeleweka, ndipo juhudi za kimataifa zinafikiwa ili kuwakutanisha watawala waheshimiwa, na papo kwa papo mahuaji yanasitishwa. Hii ina maana kwamba, tutafikia mahala ambapo, Wakikuyu watasema, kama mambo yenyewe ndiyo haya, basi tuivunje nchi ili Wakikuyu warudie identity yao, na wawe na Rais wao, ambaye siyo Mjaluo. Vivyo hivyo Waunguja na Wapemba.

Ndio maana nasema, viongozi wa namna hii, wanaotaka madaraka kwa udi na uvumba, hawapashwi kuachiwa maamuzi makubwa kama ya kutafuta muundo wa Muungano. Matatizo ya Unguja na Pemba au Tanganyika na Zanzibar, sio matatizo ya wananchi. Ni matatizo ya madaraka. Wananchi wanachochewa kuwa wafuasi. Ndipo tunaanza kujenga chuki zinazoonekana sasa hivi.

Tunaendelea kuwa na Muundo wa Muungano usio faa, eti kwa sababu tunaogopa kuwakasirisha Wazanzibari. Sasa nini maana ya Muungano. Tunaweza tukawa na Serikali moja, chini ya Rais mmoja, makamu wake mmoja, na Waziri Mkuu mmoja. Tanzania nzima inakuwa ni mikoa ambayo wakuu wake wanachaguliwa moja kwa moja na wananchi badala ya kuteuliwa.

Hatuhitaji Mabunge mengine, by the way, Bunge la Seneti litafanya kazi gani ambayo imeshindwa kufanywa na Bunge la Muungano au Bunge la Wawakilishi. Tumeambulia Muungano ambapo, Zanzibar inachagua Wabunge katika Bunge la Muungano kutoka katika majimbo ya uchaguzi, kama ambavyo inavyofanyika bara. Lakini baraza la Wawakilishi la Zanzibar, linateua tena Wabunge zaidi ya wale waliochaguliwa, kuingia katika Bunge la Muungano. Tanganyika hakuna kitu kama hicho.

Tunahitaji Bunge moja, lakini lenye wawakilishi wanaowakilisha wananchi, badala ya kuwakilisha vyama vya siasa. Kama Wazanzibar wanaona hiyo haifai, sioni haja ya kung'ang'ania kitu kinachowafaa viongozi, lakini kinawaumiza wananchi.
 
Kyoma,
Huu mjadala unanikumbusha mzee wa hoja, Mzee Mkandara (simsikii siku hizi). Aliwahi kutoa mfano wa ndoa; kwa maana kwamba, ili ndoa iwe imara, mke na mme warudie katika hali zao za uchumba (kulinda identity ya mke na mme). Ili isije ikaonekana wote wawili wamemezwa katika ndoa yao, inabidi wafufue na kulinda haki zao walizokuwa nazo kabla ya ndoa. Haki zenyewe, mojawapo ni kila mtu kumrudia mchumba wake wa zamani (girl & boy friends).

Kuna wanaosema, ili Muungano uimalike na uweze kudumu, basi Zanzibar iwe na identity yake. Yaani iwe na wimbo wake wa Taifa, Bendera yake, nakadhalika. Vivyo hivyo kwa Tanganyika. Siku timu ya taifa ya Zanzibar na Tanganyika zikimenyana, timu ya Zanzibar itapigiwa wimbo wake wa taifa tofauti na wimbo wa taifa itakaopigiwa timu ya Tanganyika. Baada ya hapo utapigwa wimbo wa Taifa wa Tanzania

Duh.... sikuwa na maana hiyo mkuu!...Yaani hata wimbo wa Taifa!..nilichokuwa nikisema ni nafasi ya kila mmoja wao katika ndoa yaani nchi zote mbili ni lazima zitambue kuwa ndoa ni makubaliano kati ya watu wawili..Kila mmoja wao ana haki zake kama binadamu na kutokuwepo kwa haki hiyo ama kutotambua nafasi ya kila mmoja wao ktk ndoa hiyo basi hiyo ndoa haiwezi kudumu..
 
Mkandara, kumbe upo Mzee! nilikuwa sijakusikia. Karibu wewe mimi mwenyeji bwana.
Zitto nakutafuta sana. ni PM email yako au simu, kuna jambo la msingi nataka tuongee

thanks
 
Back
Top Bottom