Leo natangaza rasmi kuacha kushabikia soka la Tanzania

Niwe wazi kabisa. Soka la bongo niliacha kulifuatilia siku nyingi zilizopita. Na sababu haswa ya kuachana nalo ni aina ya mpira tunaocheza. Vilabu vilivyopo ni vitatu tu. Simba, Yanga na Azam. Hao wengine sijui Ihefu, Mbeya kwanza, Mbeya City na nyingine za aina hiyo ni upuuzi mtupu.

Mpira unaochezwa uwanjani ni wa hovyo, hauna kitu choxhote cha ufundi, ni butuabutua tu.
Waamuzi nao ni eneo lingine ambalo linaangusha soka la bongo ambalo tayari ni bovu. Haswa linesman. Hawa hawajui wakati gani mchezaji anakuwa off side. Akiona beki kazidiwa mbio na mshabuliaji kawa mbele kwao wao ni off side hata kama alianza kukimbia akiwa on side.
Kwa kifupi sina muda wa kufatilia soka la bongo.
Sawa sawa mkuu ngoja nije kwenye camp yako. Tubakie tu na Liverpool yetu. Bongo nyoso.
 
Yes zote ni sababu za msingi kabisa zilizofanya niamue hivyo. Nimekuja kuona soka la bongo ni michosho tu ngoja mimi ni focus tu kwenye mpira wa mabeberu hamna namna.
Hivi bongo kuna kinachofanyika kwa standard 🤣🤣🤣

Huwa nawashangaa watu fulani mnakua kwenye banda mnaangalia labda mechi fulani ulaya mathalani chelsea vs Southampton halafu second half ya hiyo mechi kuna mechi nyingine bongo mathalani simba vs mwadui basi utasikia tuondolee hiyo mechi ya ulaya tuwekee simba vs mwadui 🤣🤣🤣,huwa nachekaga sana
 
Leo hii tarehe 26/10/2021 mimi Chaliifrancisco nikiwa na akili timamu kabisa natangaza kusimama kufuatilia na kushabikia mpira wa hapa kwetu Tanzania. Kama nitakuja kushabikia tena sijui lakini itategemea na tathmini nitakazofanya mwenyewe nikiridhishwa nitaamua.

Sababu zilizofanya nifikie uamuzi huu ni kwanza kutokana na jinsi team zetu za hapa nyumbani zinavyoshindwa kufanya vizuri kimataifa kutokana na hujuma za baadhi ya watu (viongozi) mfano ni team ya Biashara Utd kushindwa kusafiri kwenda Tripoli kwaajili ya mechi ya marudiano katika kombe la Shirikisho.

Kumekuwa na tetesi kuwa viongozi walipokea rushwa ili wakwamishe team kwenda Libya. (Hata kama sio za kweli lakini kitendo cha kushindwa kupeleka team ni upuuzi usiovumilika kabisa).

Uongozi wa club walishajua watashiriki michuano hiyo tokea mwisho wa msimu na maandalizi yalitakiwa yawepo hata kwa kupitisha bakuli kama Yanga lakini wamezembea. Na kama ni kweli walivuta mlungula basi ni fedheha sana kwa soka letu. Hawa watu wafungiwe maisha na TAKUKURU wakamate wapige miaka 50 ndani.

Sababu nyingine ni team kutofanya vizuri kutokana na uzembe/kubweteka (complacency)

Mfano ni Simba msimu uliopita walibweteka sana na kuidhrau Kaizer Chiefs matokeo yake kila mtu anajua kilichotokea. Kiuhalisia kweli Simba alikuwa na nafasi nzuri zaidi ya kusonga mbele lakini complacency ndio tatizo.

Kitu hicho hicho kimejirudia tena msimu huu (weekend iliyopita). Haiingii akilini team ishinde ugenini goli 2 halafu kocha ashindwe ku manage mchezo wa marudiano nyumbani na team inafungwa 3 na kutolewa. Hii haikubaliki.

Kitu cha pili ni huu uamuzi wa club ya Simba kuamua kumtupiga virago kocha Didier Gomes. Hebu angalia CV (takwimu) za kocha huyu tokea ametua Msimbazi.
View attachment 1987372
Hivi ni wapi tutapata kocha mwenye uwezo kama huyu? Simba wametumia kigezo gani kuachana na huyu kocha? Kwa takwimu hizi ni ngumu kupata kocha ambae anaweza kufikia angalau robo tatu ya alichokifanya Da Rosa.

Mimi kutokana na habari hii ya kuondolewa Da Rosa ndio kumenifanya sasa nifikie maamuzi ya nilichokuwa nakifikiria cha kuachana na soka la Tanzania ambalo halina tija.

Yani ili uweze kuelewa soka la Tanzania lazima uwe na ukichaa fulani. Ukiwa mtu smart kama mimi hili soka la bongo halikufai.

Until then. I rest my case.
Umechelewa karibu sisi wengine kitambo hatupo huko, wachekeshaji kibao
 
Hivi bongo kuna kinachofanyika kwa standard 🤣🤣🤣

Huwa nawashangaa watu fulani mnakua kwenye banda mnaangalia labda mechi fulani ulaya mathalani chelsea vs Southampton halafu second half ya hiyo mechi kuna mechi nyingine bongo mathalani simba vs mwadui basi utasikia tuondolee hiyo mechi ya ulaya tuwekee simba vs mwadui 🤣🤣🤣,huwa nachekaga sana
Kwakweli mkuu ni sawa na unakula mchemsho wako mzuri wa kuku wa kienyeji halafu mtu akunyang'ane akupe chips mayai.
 
Binafsi nitaendelea kuishabikia Simba japo kwasasa nimekubali..Simba inatimu mbovu Sana.. wachezaji wakawaida Sana..huyu banda Ni sawa na kichuya.. kiukweli kwasasa mchezaji mzuri Ni Bwaliya pekee..anaweza ku dribble kiasi flani.. lakini Banda kanoute..na Duncan Ni wachezaji wakawaida Sana..wanajua kucheza lakini sio tishio..labda sakho Nampa muda.
 
Binafsi nitaendelea kuishabikia Simba japo kwasasa nimekubali..Simba inatimu mbovu Sana.. wachezaji wakawaida Sana..huyu banda Ni sawa na kichuya.. kiukweli kwasasa mchezaji mzuri Ni Bwaliya pekee..anaweza ku dribble kiasi flani.. lakini Banda kanoute..na Duncan Ni wachezaji wakawaida Sana..wanajua kucheza lakini sio tishio..labda sakho Nampa muda.
Ndio hivyo mkuu mimi nimeshautua mzigo huu maana ni kama gunia la misumari tu.
 
Back
Top Bottom