MABOGOJOHA
JF-Expert Member
- Aug 28, 2016
- 541
- 427
Bado nafikicha macho na wala siamini hiki ninachokiona. Naota au ndio ukweli wa hiki ninachokitazama? Hapana, siamini. Leo Kubenea anamshangilia Zitto!!?? Hii ni kali ya karne. Yaani pamoja na magomvi waliyonayo baada ya Kubenea kutumia vilivyo magazeti yake kumnanga Zitto lakini leo pale Bungeni anamshangilia na kumuona kama malaika na kuyashadidisha maudhui ya Zitto kwa bashasha ya makofi. Siamini ni Kubenea huyu huyu au mwingine au kilikuwa kivuli chake pale Bungeni.
Nikikumbuka wawili hao walivyogombana na kuadhiriana tena mbele ya hadhara na maandishi yasiyo ya kiungwana, lakini leo nawaona wamekaa pamoja tena kwa bashasha. Ama kweli hizi siasa zina mambo na vijambo. Tuweke akiba ya maneno!