Umeme ulianza kukatika na kuwaka mara kadhaa usiku wa manane, ilipofika alfajiri umeme ukapiga baibai my sani, ndiyo kwaheri hiyo haujarudi. Je, huko kwingine umeme upo? Kwa hali hii hayo maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yaliyoanza jana Jumapili hayataathirika?
Habari, Ndugu Mteja.
Asante kwa kuwasiliana na TANESCO Huduma kwa Wateja.
Pole sana kwa changamoto uliyoipata. Aidha, tunaomba radhi kwa kuchelewa kukujibu kutokana na changamoto ya muda (temporary) iliyojitokeza kwenye akaunti yetu, iliyosababisha ujumbe wako kutufikia kwa kuchelewa.
Tafadhali fahamu kuwa pale tunapolazimika kusitisha huduma ya umeme kwa ajili ya matengenezo yaliyopangwa au kutokana na hitilafu za dharura, huwa tunatoa taarifa mapema kadiri inavyowezekana, zikieleza sababu za usitishaji wa huduma, maeneo yatakayoathirika na, pamoja na muda unaotarajiwa wa kurejea kwa huduma.
Taarifa hizi hutolewa kupitia njia mbalimbali rasmi za mawasiliano, ikiwemo ujumbe mfupi wa simu (SMS) na makundi yetu rasmi ya WhatsApp yaliyopangwa kulingana na mikoa, wilaya na maeneo mbalimbali.
Iwapo hukupokea taarifa hizo, tunaomba radhi kwa usumbufu uliotokea.
Ikiwa ungependa kuzipokea kwa wakati, tafadhali tutumie namba yako ya WhatsApp kupitia inbox, pamoja na jina la wilaya na mkoa unaoishi, ili tukuunganishe kwenye kundi husika na pia kukujumuisha kwenye mfumo wetu wa ujumbe mfupi wa simu (Bulk SMS).Asante kwa uvumilivu na ushirikiano wako. ^CM