Leo hii tarehe 26/8/2011 ndio tunafika siku ya mwisho ya Bunge la Bajeti kwa mwaka huu. Kuna mengi yamejitokeza likiwamo la David Jairo kuwafananisha Wabunge wa CCM na Ze Commedy.
Kama Si kwel Ze Commedy, kwa nini walimtaka Mh. Lema kufuta kauli au alete ushahidi kuhusiana na Uongo aliotoa Waziri Mkuu kulidanganya Bunge, na yeye akaamua kuleta Ushahidi ambao mpaka leo hukumu haitajwi! (Funika Kombe)
Kama Si Ze Masanja, mbona Mh. Zitto Kabwe alitakiwa atoe ushahidi alipowatuhumu Mawaziri, akaleta ushahidi, mpaka leo hakuna kilichozungumzwa tena! (Funika Kombe).
Kama Si kweli ni Ze Joti, mbona Mh. Kafulila aliwaeleza waziwazi alivyowakamata Wabunge wa CCM wa kamati yake akina Erasto Zambi wakipokea Rushwa, mpaka sasa ni Kimya!
Kama Si kweli ni Ze Mpoki, mbona Ushahidi aliotakiwa aulete Tundu Lissu au afute Kauli na Hakufuta Kauli akaleta Ushahidi, mbona nao Kimya!
Je Kama Si kweli ni Ze Wakuvanga, mbona Katibu Mkuu Kiongozi ametuambia kuwa Utaratibu wa Ku-Jairo ni wakawaida, wakati Waziri Mkuu alijifanya kushangaa siku ile nusura aanguke!
Je Kama Si kweli ni Ze Mac Reggan, mbona Mh. Ngeleja, alilikimbia na kuja kumlaki Jairo siku anayorudishwa ofisini wakati siku ile ya kwanza hata yeye alijifanya kumshangaa kwa kufanya kitendo cha ajabu!
Je Tutegemee Ripoti za Uchunguzi wa Ushahidi wa Lema, Zitto, Kafulila, Tundu Lissu zitasomwa leo!
Vinginevyo Mh. Jairo ataendelea kuwa right, kwamba Ze Bunge Ze Commedy.
Naomba kuwakilisha.