Leo Bunge linaahirishwa, una maoni gani?

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,585
5,758
Leo bunge linafikia tamati hadi msimu mwingine. Je, mbunge wako amekuwakilisha ipasavyo au ameenda kulala?
Nini kifanyike?
Bunge limetimiza wajibu wake?
 
Leo tarehe 26/08/2011 ndio siku ya mwisho ya Vikao vya mjadala wa Bunge la Bajeti. Kumbukumbu sahihi zinanionyesha kuwa kikao hiki cha leo ni kikao cha 57, ya kikao kikubwa cha 4 la Bunge la 9. Mengi yamezungumzwa, tumeshuhudia mijadala mikali na yenye ukinzani mkubwa kama vile..

1. Kukwamishwa kwa bajeti ya wizara ya nishati na madini,

2. Kuongezwa billion 95 katika wizara ya uchukuzi,

3. Kusimamishwa kazi na kuundwa tume ya bunge juu ya sakata la Nd. David Jairo-Katibu mkuu wa wizara ya nishati,

4. Sakata la uhuzwaji holela wa UDA (Shirika la usafirishaji dar es salaam),

5. Mvutano mkubwa kati ya wafanyabiashara wa mafuta na Ewura as wel as serikali,

6. Kusimamishwa kazi kwa Afisa wanyamapori kwa sakata la twiga walioporwa kwenda Qatara

7. Sakata la ununuzi wa Rada na report toka kitendo cha kijasusi cha upelelezi cha Uingeleza-SFU

8. Ongezeko la mshahara la 8.6% kwa wafanyakazi wa umma na ongezeko la kima cha chini kutoka sh. 135,600/= mpaka 151, 000

9. Kuletwa kwa Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano

10. Kujiuzuru kwa pacha mmoja kati ya RACHEL Bw. Rostam Azizi,

11. Kufariki kwa Mbunge Mussa Silima (Rest In Peace).

Katika hayo na mengine mengi HEBU KWA PAMOJA TUFANYE TATHIMINI JUU YA UNDENDAJI KAZI WA BUNGE HILI.

Nawasilisha!
 
- Kutenguliwa kwa kanuni za Bunge ili kuwafurahisha MAFISADI

- Wabunge vihiyo na vilaza kutoka chama cha Magamba kunusulika kupigwa.

- Waziri Mkuu pamoja na Mawaziri wengine kusema uongo Bungeni na kulidanganya taifa.
 
Leo bunge linafikia tamati hadi msimu mwingine. Je, mbunge wako amekuwakilisha ipasavyo au ameenda kulala?
Nini kifanyike?
Bunge limetimiza wajibu wake?

Mimi nilishaliahirisha tangu wiki iliyopita naangalia Primier League na Laliga bro
Sina time na Bunge la Bibi Kiroboto la vijembe mamilion yanaibiwa
 
Maneno yamekuwa mengi zaidi ya vitendo nathani ccm hakuna hata moja watakalo jivuni maana maisha ya wa tz bado magumu kupita kiasi mafuta bei juu,chakula tabu,sukari ndiyo balaa, nawasifusa sana cdm kwakuonyesha serekali njia mbadala yakutukwamuwa mungu naimani kubwa sana na cdm mungu aibariki cdm tunaimani nanyi sikuzote
 
Leo hii tarehe 26/8/2011 ndio tunafika siku ya mwisho ya Bunge la Bajeti kwa mwaka huu. Kuna mengi yamejitokeza likiwamo la David Jairo kuwafananisha Wabunge wa CCM na Ze Commedy.

Kama Si kwel Ze Commedy, kwa nini walimtaka Mh. Lema kufuta kauli au alete ushahidi kuhusiana na Uongo aliotoa Waziri Mkuu kulidanganya Bunge, na yeye akaamua kuleta Ushahidi ambao mpaka leo hukumu haitajwi! (Funika Kombe)

Kama Si Ze Masanja, mbona Mh. Zitto Kabwe alitakiwa atoe ushahidi alipowatuhumu Mawaziri, akaleta ushahidi, mpaka leo hakuna kilichozungumzwa tena! (Funika Kombe).

Kama Si kweli ni Ze Joti, mbona Mh. Kafulila aliwaeleza waziwazi alivyowakamata Wabunge wa CCM wa kamati yake akina Erasto Zambi wakipokea Rushwa, mpaka sasa ni Kimya!

Kama Si kweli ni Ze Mpoki, mbona Ushahidi aliotakiwa aulete Tundu Lissu au afute Kauli na Hakufuta Kauli akaleta Ushahidi, mbona nao Kimya!

Je Kama Si kweli ni Ze Wakuvanga, mbona Katibu Mkuu Kiongozi ametuambia kuwa Utaratibu wa Ku-Jairo ni wakawaida, wakati Waziri Mkuu alijifanya kushangaa siku ile nusura aanguke!

Je Kama Si kweli ni Ze Mac Reggan, mbona Mh. Ngeleja, alilikimbia na kuja kumlaki Jairo siku anayorudishwa ofisini wakati siku ile ya kwanza hata yeye alijifanya kumshangaa kwa kufanya kitendo cha ajabu!

Je Tutegemee Ripoti za Uchunguzi wa Ushahidi wa Lema, Zitto, Kafulila, Tundu Lissu zitasomwa leo!

Vinginevyo Mh. Jairo ataendelea kuwa right, kwamba Ze Bunge Ze Commedy.

Naomba kuwakilisha.
 
Mbunge wangu Maghembe hajaniwakilisha hata kidogo.
 
The MPs have low expectations,not revolutionary,lack influencial leaders,money hungry and not well informed.
Bunge lilikuwa bogus,we can live without it!!
 
Maneno yamekuwa mengi zaidi ya vitendo nathani ccm hakuna hata moja watakalo jivuni maana maisha ya wa tz bado magumu kupita kiasi mafuta bei juu,chakula tabu,sukari ndiyo balaa, nawasifusa sana cdm kwakuonyesha serekali njia mbadala yakutukwamuwa mungu naimani kubwa sana na cdm mungu aibariki cdm tunaimani nanyi sikuzote

Ni kweli ndugu yangu, tunawaomba wasikatishwe tamaa nakina Wassira, wameshashindwa kuongoza. Mungu bariki CDM.
 
Na vipi kuhusu utendaji kazi wa Spika, Naibu spika na wenyekiti wa bunge? Swala la kuomba miongozo na taarifa zisizo na maana mwalizungumziaje pia?
 
Na vipi kuhusu utendaji kazi wa Spika, Naibu spika na wenyekiti wa bunge? Swala la kuomba miongozo na taarifa zisizo na maana mwalizungumziaje pia?
<br />
<br />
hawa ndio walipoteza kabisa hadh ya bunge.
 
Walio wengi tumeshuhudia kamati ya wabunge wa CCM ikitumika kudhalilisha hadhi ya bunge na kulifanya liwe sawa na bunge lisilo na wabunge.

Tunawashukuru kambi rasmi ya upinzani na wale baadhi wasio wa CHADEMA wamekuwa mawakili wazuri wa wananchi, na kuonyesha kuwa unaweza kuwa na wabunge wachache wenye tija kwa taifa, kuliko kuwa na utitiri wa wa wasaliti wenye kujivika joho la wawakilishi wa wananchi kumbe ni wanadishaji wa raslimali zetu.
 
Jamani mimi na waza chai tu maana sukari imepanda bei kutoka 1900 - 2,400, acha CHADEMA wamalize kazi za bunge tuje tuandamane
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom