Leo 14-10-2019 Nyrerere day,tujadili na tujikumbushe

lee van cliff

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,522
2,000
Siku baba wa taifa alipofariki hakua rais Wala hakua mwenyekiti wa ccm Bali alika mstaafu na raia tu.

Lakini mambo yliyoshangaza ni mengi,machache ni haya.

Serkali ya marekani ilisema Kama ikihitajika inaweza kusaidia gharama za matibabu,

Hospitali ya St Thomas ilisema iko tayari kutoa huduma bure kwa heshima ya Nyerere

Siku mwili wa mpendwa wetu uliposhushwa airport maelfu ya wakazi wa Dar walijipanga bila kupangwa Wala kulazimishwa kwenye barabara zote ulipopitishwa mwili pande zote za barabara wakipunga mikono na wengi wakilia kumuaga,wengine walikimbia kutoka airport kwa miguu Hadi kwake msasani kuomboleza.

Waziri wa mambo ya nje wa USA bi madaline Albright alikuwepo uwanjani na Marais wengi wakiwakilisha mataifa yao,waziri huyo wa USA alipopewa nafasi kutoa Salam zake cnn wakasitisha matangazo mengine, wakarusha hotuba ya Mama huyo mubashara,akimwkilisha rais bill Clinton.

Marais zaidi ya Saba wa nchi za afrika walipanda coaster kuja uwanjani kwa pamoja .

Baadae mwli uliwekwa uwanja wa taifa watu kuaga na kutoa Salam zao za mwisho mwili ulikaa uwanja wa taifa wiki mbili lakini watu hawakuisha kuaga.

Baada ya mwili kusafirishwa kwenda musoma maelfu ya watu walikuwepo musoma kwa majonzi makubwa.

Mambo yote haya maelfu ya watanzania na eac walishuhudia mubashara kupita tv zao.

Mazishi yalihudhuliwa na maelfu ya waombolezaji toka dar Hadi musoma na afrika na duniani kote.

Je, Kuna kiongozi yeyote aliyepo madarakani ama aliestaafu anaweza kupata waombolezaji wengi kwa maelfu Kama nyerere?

Je, Kuna kiongozi anayependwa Kama Nyerere?

Je, Kuna kiongozi gani akistaafu ataendelea kukubalika Kama nyerere?

Je, Kuna kiongozi gani wa kumfananisha na Nyerere kwa matendo akili busara hekima na heshima kitaifa na kimataifa?

Nyerere alipokuwa hai alisafiri nchi nyingi na alipokelewa kwa heshima Sana na viongozi wa nchi ndogo na kubwa,alipokewa na kuongea na viongozi wakubwa na walioheshimika Sana wa nchi Kama USSR USA UK Fr China German Japan falme za kiarabu na nchi kadha wa kadha.

Nani Kama Nyerere?

Unaweza kumfananisha na Nani kwa viongozi waliopo madarakani na waliostaafu kwa Tz ya sasa?
 

Gellangi

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
1,796
2,000
Hakuna wa kufanana Naye,Mwl.J.K.Nyerere was an Intellectual and a Teacher.

Alikuwa binadamu kama sisi lakini moyo wake ulikuwa mkubwa na hakupenda watu wake wateseke.Siyo kama watawala wetu wa kisasa wanaotamani tulimie meno.

Watanzania tudai Kati a ya wananchi,wakati ni huu.Tuhamasishane kuidai.
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,099
2,000
Nyerere Atakumbukwa Na Vizazi Na Vizazi Kwa Kuwaunganisha Watanganyika Na Kujiona Kama Kabila Moja Kupitia Muungano Wa Zanzibar"
 

lee van cliff

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,522
2,000
Hakuna wa kufanana Naye,Mwl.J.K.Nyerere was an Intellectual and a Teacher.
Alikuwa binadamu kama sisi lakini moyo wake ulikuwa mkubwa na hakupenda watu wake wateseke.Siyo kama watawala wetu wa kisasa wanaotamani tulimie meno.
Watanzania tudai Kati a ya wananchi,wakati ni huu.Tuhamasishane kuidai.
lakini Kuna watu wanadai tuliyenae ni zaidi ya nyerere kwa miaka 4 kafanya mengi na makubwa.
Hakuna wa kufanana Naye,Mwl.J.K.Nyerere was an Intellectual and a Teacher.
Alikuwa binadamu kama sisi lakini moyo wake ulikuwa mkubwa na hakupenda watu wake wateseke.Siyo kama watawala wetu wa kisasa wanaotamani tulimie meno.
Watanzania tudai Kati a ya wananchi,wakati ni huu.Tuhamasishane kuidai.
 

koyola

JF-Expert Member
May 20, 2015
2,512
2,000
Huyu mzee maneno yake yalikua fikirishi sana kauli yake moja ni fundisho kubwa
Kwamba hata yeye kuna mabaya waliyafanya lakini watakaokuja wayache na warekebishe walipokosea, pia yapo mazuri ambayo waliyafanya wayaendeleze na kuyaboresha zaid.. maana binaadamu hakosi kasoro sio malaika.
Baada ya hayo nikatafakari kauli ya mjumbe mmoja wa bunge la katiba wakati huo kwa kauli zake alizozitoa bungeni kumkashif huyu mzee kwa mbwembwe nyingi.
Na nikirejea kua nae ni binaadamu hakosi kasoro midamu yu hai bado anaweza kurekebisha hizo kauli kwa mapungufu yake kama binaadamu,ili asemehewe...
 

Gellangi

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
1,796
2,000
lakini Kuna watu wanadai tuliyenae ni zaidi ya nyerere kwa miaka 4 kafanya mengi na makubwa.
Wanasema kwa vinywa lakini mioyoni mwao wanaufahamu ukweli,hawathubutu kutoa hoja au maoni huru.Tuna J.K.Nyerere moja tu ambaye alikuwa Mwalimu mwanzo mwisho[Denial does'nt heal ailment].Ukweli utatuweka huru,tuache kulinganisha watu bali tuwapime kwa yale wayatendayo.
Tumejishusha sana kama Taifa,tunasubiri vipaumbele kwa viongozi badala ya wananchi kuainisha vipaumbele na changamoto zao na viongozi wawezeshe kuweka sera bora za kuzitatua?
 

Onjwaria

JF-Expert Member
Sep 13, 2016
926
1,000
Hakuwa mbinafsi na siku zote aliaamini Tanzanian ni ya watanzania. Alipenda aitwe ndugu na kuchukia kuitwa mheshimiwa au mtukufu. Yeye alikuwa binadamu kama sisi na muda mwingi alipokuwa likizo alishiriki shughuli za kijamii kama kupalilia na kushiriki na wazee wenzake kucheza bao. Kamwe hakupenda kuabudiwa wala hakujilimbikizia Mali. Migodi mingi aliweka chini ya uangalizi wa jeshi ili kesho watanzania watakapokuwa na uwezo waje wachimbe. Aliweka viwanda na miradi Mikuu karibu kila mkoa. KWAKE hadi anakufa barabara ilikuwaa ya vumbi. Huyo ndiye Nyerere nimjuaye ambaye hakuna mfano wake TANZANIA
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom