Lengo la tbc1 na shindano la ndoto

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,507
11,883
Wana JF ningependa kujua lengo la TBC1 na LAPF katika shindano la ndoto ambalo linaendeshwa na mama TERRY.Nia ya kipindi sijailewa vizuri kwani imekuwa ni kuonyesha umaskini tulionao watanzania au kusaidia kutatua matatizo ya jamii kama elimu etc au kuboresha biashara wazifanyazo washindani?Jee sisi watazamaji tupige kura kwa kuangalia kigezo gani?ubunifu,kutunza mazingira au kuangalia familia masikini zaidi ndio tuipe kura?mshindi atapata tsh 5m naomba maoni wana jf
 
Nadhani ni majibu yote mawili. Kuna shindano jingine la serebuka. Sijajua hizi idea wanazitoa wapi ila kama zina manufaa kijamii, poa tu
 
Pia kuna hiki kipindi cha "Chereko". Mimi binafsi nimeshindwa kabisa kuelewa maana ya hiki kipindi. Kuwatangazia the select few harusi zao jinsi zilivyokuwa? Ili iwe nini?

Mwanzoni nilidhani atakuwa anatuonyesha au kutuelezea vitu vilivyotofauti (unique) kwenye hizo harusi anazoonyesha ili tufunguke macho / tupate ideas.

Au labda kutuelezea juu ya mambo mbali mbali ambayo watu hukabiliana nayo wakati wa kuandaa shughuli ya harusi na send-off. Hii ingewafungua macho wale ambao wanatarajia kufunga ndoa.

Lakini kwa format aliyonayo mimi kwa kweli nimeshindwa kuona maana ya hicho kipindi
 
Labda tunaonyeshwa mavazi na ku-imagine gharama zilivyotumika. Binafsi pia nilielewa pengine kingekuwa ni cha kuelezea mila, desturi na tamaduni za wanandoa walikotoka pamoja na muungano wao mpya. Maisha yao baada ya ndoa n.k. ila naona ni chereko tu kwa kweli yaani ni maneno tu kama kutangaza biashara vile sija
 
kwa ujumla wake hapo juu mi ndo siilewi kabisa TBC1; kila siku najiuliza maswali mengi yakiwemo haya! Yote yaliyoelezwa hapo juu ndio mapato ya kodi zetu? na yana tija gani kwa umma wetu kwa ujumla? Yaani imekuwa kama ni kijiwe flan hivi cha dili!:angry:
 
Back
Top Bottom