Buyaka
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 1,643
- 1,786
Utawala mpya wa Rais Samia Suluhu Hassan leo umeangusha moja ya nguzo za katikati za urithi, legacy, ya aliyekuwa Rais John Pombe Magufuli kwa kutumbuliwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.
Kama ulipenda alichokisimamia John Magufuli pengine leo ni siku ya huzuni.
Nilimwona kwenye clip mapema mwaka huu saa sita za usiku akivamia kibanda cha mchaga kwa mbele, kwa nyuma ni ghala lenye shehena ya mzigo wa bia na mapipa ya dizeli na petroli zinazouzwa bila kulipiwa kodi, bila kutolewa risiti, bila taratibu za kuhifadhi shehena ya petroli ndani ya jengo wala bila ya usajili wa biashara zaidi ya leseni za kuuza vocha na mafuta ya taa.
Alikuwa amebeba tochi, amejikunyata kwenye kikoti cha baridi, ameambatana na afisa wa TRA, mwanahabari na askari polisi.
Sikuwahi kumwona au kusikia kiongozi wa nchi hii katika historia yake ya miaka 60 akifanya kazi nje ya ofisi kwenye giza tororo saba usiku, awe Afisa Mtendaji, Diwani, Mbunge, Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa, Waziri, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais au Rais.
Nitamkumbuka kwa taswira ile.