Rais Samia umeanza kunikosha, bado Sabaya tu

Rais Samia umeanza kunikosha, bado Sabaya tu

Etwege

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2018
Posts
7,953
Reaction score
19,864
Rais Samia ulianza kuugusa moyo wangu ulipomrejesha Paul Makonda kazini, na leo tena umeukuna moyo wangu baada ya kumteua kijana mchapakazi Ally Hapi.

Sasa umebakiza kumrudisha ulingoni kijana Lengai Ole Sabaya na moyo wangu utakuwa umeukuna moja kwa moja kabisa Rais Samia.

Paul Makonda, Ally Hapi, Lengai Sabaya ni vijana wa Magufuli na ni wachapakazi kwelikweli lakini walichafuliwa na matapeli Chadema wakishirikiana na wauza madawa ya kulevya na mafisadi ya nchi hii.

Lakini wahenga walishasema muda ni mwalimu mzuri sana na sasa imepita miaka 3 hamna tapeli yoyote aliyeweza kuleta ushahidi kuhusu tuhuma za hao vijana.
 
Paul Makonda, Ally Hapi, Lengai Sabaya ni vijana wa Magufuli na ni wachapakazi kwelikweli lakini walichafuliwa na matapeli Chadema wakishirikiana na wauza madawa ya kulevya na mafisadi ya nchi hii.
Usichokujua ni kwamba chama kimerejeshwa mikononi mwao. Maana yake ni kwamba wana nguvu kuliko wale washamba toka ile Kanda pendwa.

Na mtu akikuzidi nguvu Utaratibu unajulikana. Unakuwa mpole halafu unaungana naye tu. Kaeni kwa kutulia tu.

Huyo Makonda alitaka kuleta za enzi za jiwe wamekata kichwa. Hata huyo Sabaya akipewa uDC atalazimika kupoa kama Heri James ili familia yake iendelee kwenda chooni.
 
Sabaya anarudi soon. Ni suala la muda tu. Lazima makomandoo wa uchaguzi warudi maana bila hivyo CCM wa mama ni wepesi sana kuliko unyoya
 
Rais Samia ulianza kuugusa moyo wangu ulipomrejesha Paul Makonda kazini, na leo tena umeukuna moyo wangu baada ya kumteua kijana mchapakazi Ally Hapi....
Eeh Mnyeti yuko wapi sijui ili waunde ile dream team kiboko ya chadema!
 
Sabaya Jambazi. Mbona mnapenda watu wenye Record za Uhalifu dhidi ya Wananchi wa Tanzania ndio wawe Viongozi wenu?
Ndo ujue CCM hawana nia njema na watanzania. Wao wanachoangalia ni jambazi gani ataendelea kuwafanya wabaki madarakani kwa namna yoyote ile.
 
Back
Top Bottom