Lembeli: CCM si Mama yangu

Lembeli: CCM si Mama yangu

Khaa!! Kama ule waraka wa dr kitila??

Ndiyo mkuu tusitishiane kufukuzana kwenye vyama kwa sababu ya kutofautiana mitizamo au kufuata mtizamo wa mwnykiti, hivi "zidumu fikra za mwenyekiti" bado zipo? cc W.J Malecela
 
JUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba, James Lembeli (CCM), amesema kuwa yuko tayari kufanyiwa lolote na chama chake lakini kamwe hatatengua msimamo wake wa kudai Serikali ya Tanganyika.

Kauli hiyo nzito ya Lembeli, mmoja wa wabunge wa CCM wenye msimamo mkali, ilipata kutolewa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere miaka ya 90 wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo chama hicho kilikuwa kikituhumiwa kwa rushwa na hivyo kupoteza mwelekeo.

Katika mazingira hayo, Mwalimu alisema kama chama hicho kisipojirekebisha, anaweza kurudisha kadi yao, kwani CCM haikuwa mama yake.

Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu huku akitumia maneno hayo ya Mwalimu, Lembeli ambaye pia ni Mbunge wa Kahama alisema baadhi ya wajumbe ni waoga na wanafiki kwa kuogopa kusimamia kile wanachokiamini.

“Historia haikarabatiwi, mimi naweza kufa au kuadhibiwa na chama changu kutokana na msimamo huu lakini historia itaandikwa.

“Pale Ikulu si kuna picha ya hayati Oscar Kambona, huyu si alifungwa kwa makosa ya uhaini, mbona picha yake haikuondolewa katika viongozi wa historia ya nchi hii?” alihoji.

Lembeli alidai kuwa Watanzania wasubiri wamuone wakati wa mjadala wa pamoja wa rasimu ya Katiba bungeni huku akitamba kuwa hatabadili msimamo hata kama unakinzana na wenzake wa CCM.

“Sina wa kumfurahisha zaidi ya wapiga kura wangu, hawa ndio wenye uwezo wa kunishughulikia endapo nitaunga mkono jambo ambalo litakuwa kinyume na wao.

“Mimi ndiye Lembeli na nitabakia kuwa hivyo, ndiyo maana nilikuwa nataka itumike kura ya siri ili kuhifadhi uhuru wa mawazo yetu. Nyerere alituambia kuwa wananchi wanataka mabadiliko na wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM,” alisisitiza.

Lembeli aliwataka wajumbe wenzake kuacha woga wa kufungwa na misimamo ya vyama au makundi yao kwani hata Rais Jakaya Kikwete aliwahi kusema: “Akili za kuambiwa changanya na zako.”


Chanzo:
Tanzania Daima
tgis ninja huwa anapenda kulopoka tu
 
- Kaka baba yako simjui ila one thing habari za kura ya siri na wazi sio ishu tena imeisha tuwe progressive tuongelee mapya ya kura za siri na wazi yamepitwa na wakati sasa!! na Kidumu chama cha mapinduzi

Le Mutuz

Le Mutuz hebu elewa nasema nini,issue ya kura ya siri na wazi haijaisha kwa kuwa wenye akili wanajua kwanini ccm ililazimisha kupigwa kura za aina mbili kuamua jambo moja.Kusema limekwisha sio sahihi isipokuwa ccm wameona ni heri kufunika kombe ili mwanaharamu apite,kwa bahati mbaya sana hakuna mwanaharamu ndiyo maana Mh.Lembeli ameamua kujilipua ili jamii ijue ccm wamen'gan'gania kura ya wazi ili waweze kuwaadhibu wana ccm wa aina ya Lembeli Kangi Lugola na Deo Filikunjombe.Huwezi kuanzisha mfumo huo wa upigaji kura ambao haupo na haujawahi kuwepo popote duniani kwa kutumia lugha nyepesi sana ya kiwango cha chini mno katika kuwashawishi wananchi kwa kuwaeleza eti RAIA WANATAKA KUONA MWAKILISHI WAO AMEAMUA NINI KATI YA SERIKALI 2 au 3,ndiyo sababu ya kukueleza hawa Watanzania sio wale wa enzi zile za kina hekaya za abunwasi ilipotokea sufuria kuzaa.
 
Kwa wale waumini wa serikali mbili 1. Nchi iitwayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni ipi? Yaani muungano wa Tanzania ni upi? Au ni Jamhuri ya muungano ya Tanzania? Nadhani wajuzi wa kiswahili watudadavulie.
2. Jamhuri hii ina ardhi yake? Je, inaendeshwa kwa mapato yatokanayo na rasilimali za ardhi yake?
3. Nchi ya zanzibar ni nchi ndani ya nchi ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania?
 
Lembeli; CCM si mama yangi
Kumbuka ccm imekufikisha ulipo, kama unataka Tanganyika hiyo sio sera ya ccm, kumbuka uliapa kulinda muundo wa muungano! Leo unageuka, kwanza neno lenyewe Tanga
 
Ufunguo ni ufunguo tu hata kama umbo ni dogo vipi na uko kwa matumizi sahihi tu, jaribu tena baadaye. LEMBELI NOMA
 
Lembeli; CCM si mama yangu
Lembeli ngoja nikukumbushe ccm imekufikisha ulipo, wakati ukigombea Ubunge kupitia ccm uliapa kulinda katiba yake yenye muundo wa serikali mbili,leo unabadika. Hivyo ni sawa na kumuasi mama yako aliyekubebea mimba miezi tisa akakuzaa, kukutunza,kukulea na kukuongoza.
Baada ya kuongozeka akasema ni ujanja na kuamua kumkasifu mama yako na kupinga kila analokuelekeza na mbaya zaidi wadogo zako nap ukawafundisha kumuasi mama yenu.
Hakika laana haitakuacha! Wako wapi? Augustine Mrema, John Shibuda, G55 na engine, niwewe Lembeli ulikuwa ukikashifu uponzani upinzani leo unabadilika.
Rais Paul Kagame aliwaambia kina Gen Nyamwasa na Patric Kalegeya Rwanda ndio imewafikisha hapo mlipo, Rwanda itawasaka popote mlipo na kwa kuwa mumeamua kuishi kama Mbwa na mtakufa kama Mbwa.
Ushauri wangu Lembeli sikiliza na fuata maamuzi ya CCM kwani ndicho kumekufisha ulipo na utakapo hama chama nenda katetee ue
 
Lembeli; CCM si mama yangi
Kumbuka ccm imekufikisha ulipo, kama unataka Tanganyika hiyo sio sera ya ccm, kumbuka uliapa kulinda muundo wa muungano! Leo unageuka, kwanza neno lenyewe Tanga



Hii Si sababu, wanaapa kwasababu ni matatizo ambayo tayari yapo. Na kwahoja yako mh.Rais aliapa kuitetea na kuilinda katiba ya JMT, lakini dunia imeshuhudia akishindwa kuitetea na kuilinda Mwaka 2010 pale aliposhuhidia Zanzibar kwa maksudi mazima wanajimega katika muungano.
 
- TOO BAD Katiba inatengezwa kwa mujibu wa sheria zilizopo sasa ambazo zipo wazi kwamba chama kinachotawala ndio chenye nafasi kubwa ya kuandika Sheria na sio vinginevyo!!

Le Mutuz

Hivi bwana mzee hiyo picha yako hapo juu ni ya mwaka gani? Una mawazo ya kijima sana!
 
Politiks bhana!, yaani inanguvu hata yakuingilia katiba ya nchi wakati kuna (uchumi, teknolojia na kijamii). Ila siasa imeshika hatamu jama!
 
Huyu nae,sio waliosema ndio kura ya wazi,akina Lembeli,Sitta,Mwakyembe,Sendeka,tumeshawajua hamna lolote wote ni wachumia tumbo tu
 
Le Mutuz hebu elewa nasema nini,issue ya kura ya siri na wazi haijaisha kwa kuwa wenye akili wanajua kwanini ccm ililazimisha kupigwa kura za aina mbili kuamua jambo moja.Kusema limekwisha sio sahihi isipokuwa ccm wameona ni heri kufunika kombe ili mwanaharamu apite,kwa bahati mbaya sana hakuna mwanaharamu ndiyo maana Mh.Lembeli ameamua kujilipua ili jamii ijue ccm wamen'gan'gania kura ya wazi ili waweze kuwaadhibu wana ccm wa aina ya Lembeli Kangi Lugola na Deo Filikunjombe.Huwezi kuanzisha mfumo huo wa upigaji kura ambao haupo na haujawahi kuwepo popote duniani kwa kutumia lugha nyepesi sana ya kiwango cha chini mno katika kuwashawishi wananchi kwa kuwaeleza eti RAIA WANATAKA KUONA MWAKILISHI WAO AMEAMUA NINI KATI YA SERIKALI 2 au 3,ndiyo sababu ya kukueleza hawa Watanzania sio wale wa enzi zile za kina hekaya za abunwasi ilipotokea sufuria kuzaa.

- Hawa wote wataadhibiwa tu ameadhibiwa yule baba yao watakuwa wao, CCM hatuna muda wa mchezo sasa ni kazi umeona mwenyewe wabunge 351 wamepigia msimamo wa Chama ndivyo inavyotakiwa, wawili hawatusmbui Lembeli anajua kwamba uchaguzi ujao ana matatizo maana kule jimboni hakuko sawa ana matatizo na viongozi wengi sana sijui atapitia wapi ndio maana wanaanza kujiweka sawa sasa sasa, CCM hatungalii nyuma tunakwenda kwa mbele Rais ameeenda bungeni ameweka chini msimamo asiyetaka atoke chaMA TU!!

lE mUTUZ
 
Hivi bwana mzee hiyo picha yako hapo juu ni ya mwaka gani? Una mawazo ya kijima sana!

- CCM ni chama kikubwa sana hakiwezi kuyumbishwa na wabunge 2 tu, so get that right watoke waje huko kwenu kwenye vurugu kila siku!!

Le Mutuz
 
Hakika wewe Jembe si kama yule Mbunge wa Arumeru Ole Madeye anayesema kura ya wazi ilitumika wakati wa maamuzi ya kumsurubisha Yesu hivyo na yeye tuamini anataka ya wazi ili kutusurubu wa Tanganyika? Nadhani anajua biblia kidogo sana yule mzee, maana imeandikwa watu walisema asurubiwe kwa kupaza sauti huku sauti za chini kama za akina Esther Bulaya, Kangi Lugola, Deo Filikunjombe na Lembeli wakisema asisurubiwe na wakati huo huo sauti za akina Samweli Sitta na akina Kificho zikisema asulubiwe kwa kuogopa kusikika na akina Kinana na Nape Nauye.
 
- CCM ni chama kikubwa sana hakiwezi kuyumbishwa na wabunge 2 tu, so get that right watoke waje huko kwenu kwenye vurugu kila siku!!

Le Mutuz
By the time you will be realizing the truth that an earth revolves around the sun it will be too rate, hata baba yako mr Malecela anataka na anajua umhimu wa serikali tatu.
 
By the time you will be realizing the truth that an earth revolves around the sun it will be too rate, hata baba yako mr Malecela anataka na anajua umhimu wa serikali tatu.

- Baba yako has nothing to do na this, wewe CCM haiwezi kuyumbishwa na Wabunge 2 tu hicho sio chama ila ni kundi la wahuni, CCM ni chama kikubwa kama kweli hawa wabunge ni mashujaa watoke tuwaone, ila wabunge 2 hawawezi kushindana na wabunge 351 ni insanity na hata kuwashangilia ni dalili za akili kama zao!!

Le Mutuz
 
Kwa wale waumini wa serikali mbili 1. Nchi iitwayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni ipi? Yaani muungano wa Tanzania ni upi? Au ni Jamhuri ya muungano ya Tanzania? Nadhani wajuzi wa kiswahili watudadavulie. 2. Jamhuri hii ina ardhi yake? Je, inaendeshwa kwa mapato yatokanayo na rasilimali za ardhi yake? 3. Nchi ya zanzibar ni nchi ndani ya nchi ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania?
Kama Zanzibar ni nchi, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaundwa na nchi zipi? Huu Muungano ni kiinimacho, ni muungano wa kinafiki na kisiasa(CCM BARA na CCM VISIWANI)
 
tunajua ccm sio mama yake, tunachotaka kujua ni atufafanulie je ile habari ya kwenda south na nyalndu ili kuuza mbuga kwa makaburu ni ya kweli au/ hii ni muhimu ili tujue tumuweke fungu lipi.
 
Back
Top Bottom