Lembeli: CCM si Mama yangu

Lembeli: CCM si Mama yangu

My dear
REMEMBER:Rasimu itakuja kwa wanainchi tutaipiga chini hata mtuburute UKWELI UTABAKI
 
Mbunge wa Kahama (CCM) Mhe.James Lembeli, amewagusa pabaya sana Vigogo na wachumia Tumbo wa CCM...."Mimi ni mmoja wa Waumini wa kuidai Serikali ya Tanganyika, hilo naliweka wazi na wala siogopi, nataka Watanzania wajue kuwa, tunachopigania ni Muungano wa Usawa kwa pande zote za Muungano, kama Ipo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, sioni Sababu ya kuikataa Serikali ya Tanganyika... "Siko tayari kuunga Mkono na Kupitisha Rasmu ya Katiba yenye Muundo wa Serikali mbili kama Chama changu kinavyotaka kwa Sababu hayo sio Mabadiliko na wala sio Demokrasia... "Tukifuata hata maelekezo ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, alituasa kuwa Watanzania wanahitaji Mabadiliko na akasema wazi kuwa wasipoyapata Mabadiliko ndani ya CCM, watayatafuta nje ya CCM... "Sasa mimi naona hii ilikuwa ni fursa kwa Chama changu kuwapatia Watanzania Mabadiliko, lakini bado msimamo wake sio wa Mabadiliko hayo, ndio Sababu mimi nimeona nianze kuonyesha njia ya kuelekea kwenye Mabadiliko hayo.
 
Hata wakimfukuza ataenda mahakamani kwa hiyo bora wamuache tu waendelee kuuguza maimivu polepole hadi 2015
 
Kidogo kidogo paka anafungwa kengele...
 
Mbona hajahama huko SSM sasa?? Wapiga debe tu hawa seeking public attention!!
 
Mbunge wangu jembe na ametumwa na zaidi ya watu milioni moja wa Kahama.Ongeza kwenye ile 60% ya Jaji Warioba

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
- TOO BAD Katiba inatengezwa kwa mujibu wa sheria zilizopo sasa ambazo zipo wazi kwamba chama kinachotawala ndio chenye nafasi kubwa ya kuandika Sheria na sio vinginevyo!!

Le Mutuz

Kwa hiyo unataka kutuambia KATIBA inayotafutwa hapo na kutumia mamilioni ya kodi zetu si ya WATANZANIA bali ni ya CCM? Nauliza tu nipate kujua
 
Kwa hiyo unataka kutuambia KATIBA inayotafutwa hapo na kutumia mamilioni ya kodi zetu si ya WATANZANIA bali ni ya CCM? Nauliza tu nipate kujua

mjomba usihangaike na huyo mzee , ni kati ya wachache sana walionufaika na hii katiba mbovu , ccm ikifa Le Mutuz naye anakufa njaa !
 
Lembeli; CCM si mama yangu
Lembeli ngoja nikukumbushe ccm imekufikisha ulipo, wakati ukigombea Ubunge kupitia ccm uliapa kulinda katiba yake yenye muundo wa serikali mbili,leo unabadika. Hivyo ni sawa na kumuasi mama yako aliyekubebea mimba miezi tisa akakuzaa, kukutunza,kukulea na kukuongoza.
Baada ya kuongozeka akasema ni ujanja na kuamua kumkasifu mama yako na kupinga kila analokuelekeza na mbaya zaidi wadogo zako nap ukawafundisha kumuasi mama yenu.
Hakika laana haitakuacha! Wako wapi? Augustine Mrema, John Shibuda, G55 na engine, niwewe Lembeli ulikuwa ukikashifu uponzani upinzani leo unabadilika.
Rais Paul Kagame aliwaambia kina Gen Nyamwasa na Patric Kalegeya Rwanda ndio imewafikisha hapo mlipo, Rwanda itawasaka popote mlipo na kwa kuwa mumeamua kuishi kama Mbwa na mtakufa kama Mbwa.
Ushauri wangu Lembeli sikiliza na fuata maamuzi ya CCM kwani ndicho kumekufisha ulipo na utakapo hama chama nenda katetee ue

Kama ndio msimamo wa CCM kulinda katiba kwanini walianzisha mchakato wa kuivunja? Nadhani kuna mahali mkuu una miss point
 
Kwa hiyo unataka kutuambia KATIBA inayotafutwa hapo na kutumia mamilioni ya kodi zetu si ya WATANZANIA bali ni ya CCM? Nauliza tu nipate kujua

huyo ndugu huwa nashindwa kuelewa kuwa huwa anajitoa ufahamu!? Au ni kweli hana Ufahamu!?
 
mjomba usihangaike na huyo mzee , ni kati ya wachache sana walionufaika na hii katiba mbovu , ccm ikifa Le Mutuz naye anakufa njaa !

Usimkatie tamaa bado tunanafasi ya kuelimisha kwamba kwanza Tanzania vyama vyetu ni baadaye.Tumuelimisha kuwa watanzania kwanza halafu baadaye viongozi wetu,vinginevyo likitokea lolote wa kwanza kuathirika siyo viongozi wala familia zao,bali sisi watanzania wa kawaida.Kuna siku ataelewa tu.
 
huyo ndugu huwa nashindwa kuelewa kuwa huwa anajitoa ufahamu!? Au ni kweli hana Ufahamu!?

Ufahamu anao ila kumbuka ni kati ya wale wachache wanafaidi zaidi KEKI ya TAIFA,na nina uhakika kuna siku atatambua kuwa hawatendi jaki kwa watanzania maskini ambao wamewanyang'anya haki zote za msingi hata za kuamua kwa ajili ya mustakabali wa nchi yao.

Mimi si muumini wa Serikali tatu lakini ninaamini serikali mbili zitawezekana kama tutaweka UTAIFA wetu mbele kwa kuwapa watanzania hoja na kukubaliana kwa hoja na maridhiano bila kulazimishana.Kwa sasa chama tawala kimeshindwa kutumia hoja na kinatumia HOJA ya NGUVU na WINGI wao ili kupata wakitakacho.
 
Back
Top Bottom