Lema: Nitabeba zigo la mabilioni ya Uswisi

Lema: Nitabeba zigo la mabilioni ya Uswisi

wataje isije ikawa porojo tu.na longolongo za kisiasa.kuna watu hawaridhiki na uchotaji wa hela
 
Nasikia hawezi tena kwenda Uk kwa sababu anatafutwa kwa kesi ya kujaribu kubaka, kwa hiyo akikanyaga UK tu na ubunge ndio basi manake atafungwa na sizani kama katiba ya tanzania inaruhusu wahalifu kuwa wabunge
Acha ujinga wee, kubaka au attempt ni serious allegation, waingereza wangemfuata Bongo. Pima ujinga mwingine kabla ya kuamini, usiwe kama mwana CCM
 
Kaka Lema huwezi kupewa hayo majina kwani jamaa zile hoja huwa ni mtaji wa kujinufaisha kisiasa, So we muachie hoja yake hiyo kwani karibia wote ni marafiki zake wa damu na ndio wanamuweka town sasa kama akikupa unategemea yeye pesa ya kuendea Dar live kwa Diamond atipatia wapi? Au unataka arudi kwao mwandiga kigoma kuvua migebuka na kutengeneza mawese?

Lema kuwa na huruma hata kidogo kamanda wangu.
 
Tatizo kamanda hawezi kuingia europe anatafutwa na polisi uk
 
Bora kaka!utakuwa umesaidia kulejesha kodi za wanaachi ili zitumike kwa ajili ya maslahi yao.naona waibuaji wa hoja wamekaa kimya.
 
KAKA WABANE HAWA HAWA WEZI UTAKUWA UMEWASAIDIA WANYONGE.USIOGOPE MAANA UOGA KATIKA KUTETEA HAKI NI DHAMBI(Mtoa hoja bungeni ni muoga)
 
Elimu kitu muhimi sana.Sipendi siasa za misifa
 
Nasikia hawezi tena kwenda Uk kwa sababu anatafutwa kwa kesi ya kujaribu kubaka, kwa hiyo akikanyaga UK tu na ubunge ndio basi manake atafungwa na sizani kama katiba ya tanzania inaruhusu wahalifu kuwa wabunge

Alitaka kukubaka wewe au mkeo?? hivi mbona huwa mnapenda kuchafua watu bila sababu?? baada ya kuandika uchafu wako hapa sasa unajisikiaje? mods vitu kama hivi vinastahili warning!!
 
Nimeipenda hii....Kwamba Lema alilakiwa Kahama kama Mfalme.
 
Nasikia hawezi tena kwenda Uk kwa sababu anatafutwa kwa kesi ya kujaribu kubaka, kwa hiyo akikanyaga UK tu na ubunge ndio basi manake atafungwa na sizani kama katiba ya tanzania inaruhusu wahalifu kuwa wabunge

Masalia aka PM7 Mtahangaika sana lakini hamtafanikiwa.
 
Lema tuambie Chopa na ambulance za UK zimefikia wapi?

Hebu ondosha mawazo yako ya kitoto hapa usije nisababishia Mi ban bure,,,,,,,,,,,,,,,,,,member kama huyu ni jamii ya kina Ritz na lile genge lake!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Nasikia hawezi tena kwenda Uk kwa sababu anatafutwa kwa kesi ya kujaribu kubaka, kwa hiyo akikanyaga UK tu na ubunge ndio basi manake atafungwa na sizani kama katiba ya tanzania inaruhusu wahalifu kuwa wabunge
Ukiachana na stori kama hizo hautapatwa na matatizo kama hayo Lema aliyotaka kukuletea.
 
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), amesema atamshawishi mbunge mwenzake wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ili ampatie majina ya vigogo walioficha fedha Uswisi awataje bungeni. Zitto ndiye aliibua hoja hiyo bungeni na kuwasilisha hoja binafsi akitaka Bunge liazimie kwa kauli moja na kuunda kamati teule ya kuchunguza tuhuma hizo na kuwachukulia hatua, vinginevyo serikali ikishindwa atawataja. Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini Kahama mkoani Shinyanga, alipopata mapokezi ya kifalme akiwa na Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, John Heche na kada mwingine, James Ole Millya, alisema kuwa atataja majina hayo bungeni. Lema alisema kuwa Watanzania wamekuwa na shauku ya kuwafahamu viongozi wao mafisadi waliopora fedha zao na kwenda kuzificha katika nchi za ughaibuni kama Uswisi, Mauritania, Dubai na Morocco. Alisema tangu hoja hiyo ifikishwe bungeni na serikali kuahidi kufuatilia, hadi sasa kumekuwa na ukimya ambao unazua maswali juu ya ukweli wa suala hilo kutoka kwa wananchi. “Nitamuomba Kamanda Zitto anipatie majina hayo nami Bunge lijalo niyaanike ili kukata kiu ya Watanzania walio na haja kubwa ya kuwafahamu, hata kama hatua hiyo itanisababishia kifo, mimi siogopi kufa,” alisema Lema. Aliwataka wakazi wa Kahama kuondokana na woga pindi linapofikia suala la kupigania haki zao na akasema wasiwaachie viongozi na wanachama wa CHADEMA pekee. Lema aliishutumu Serikali ya CCM akidai imeshindwa kuwajengea miundombinu mizuri na kuwakopesha mitaji mikubwa wachimbaji wadogowadogo pindi wanapovumbua maeneo yenye madini. Alisema kuwatimua wachimbaji hao ni kupanua wigo wa watu wasiokuwa na ajira, ombwe ambalo linaweza kuigharimu nchi hata kuingia katika machafuko. Wakati huo huo, kada mashuhuri wa CCM, Frank Mwaisumbe, aliyeitikisa ngome ya upinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 akiwania ubunge katika Jimbo la Mbeya Mjini, amehamia CHADEMA. Mwaisumbe aliyewahi kuwa Mhadhiri Msaidizi wa Kitivo cha Uchumi na Biashara katika Chuo Kikuu cha Tumaini-Iringa, kabla ya kuachana na kazi hiyo, ametangaza kujiunga na CHADEMA juzi. Alisema CCM imeshindwa kushughulikia kero na matatizo ya wananchi ikiwemo rushwa na makundi yanayowania madaraka. Jimbo hilo la Mbeya Mjini kwa sasa linaongozwa na Mbunge wa CHADEMA, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu baada kumshinda aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Benson Mpesya. Katika hatua nyingine, vijana wametakiwa kutokuwa na fikra mgando katika kupambana na matumizi mabovu ya rasilimali yanayofanywa na baadhi ya watu wachache ili kuliokoa taifa linaloangamia. Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Iringa, Joseph Lyata katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Luganga wilayani Kilolo. Lyata alisema ili taifa liweze kusonga mbele, lazima liwe na watu wenye uchungu na rasilimali zilizopo na kujali matumizi ya pamoja. Habari hii imeandaliwa na Ali Lityawi (Kahama), Gustav Chahe na Happiness Elias (Iringa)

CDK( chadema kaskazini)
 
Back
Top Bottom