Mh. Razaro alitoa taarifa kuwa Mh. Lema kagoma kula kwa sababu kanyimwa dhamana na pia kwa jinsi alivyokamatwa kwa kudhalilishwa mbele ya familia yake. Baada ya kuachiliwa kwa dhamana akaja na taarifa kuwa hakugoma kula bali alifunga kuliombea taifa, japo kwa neno la Mungu, Yesu alisema ufungapo usimwambie mtu wala kutangaza, bali iwe siri na Mungu aonaye sirini atakujibu na kukuhesabia thawabu, bali ukitangaza tayari umepata thawabu kwa wanadamu na usitegemee thawabu kwa Mungu, yaani ni kama umeshinda njaa.
Swali la msingi linakuja kwa viongozi wetu, wanaojiita akili kubwa, mbadala na wanaotaka tuwaamini, tukio moja kila mtu ana version yake, moja hapo litakuwa la kweli na moja la uongo, na yote ni kutafuta huruma. swali ni je nani muongo kati ya hao wawili? au hawakuwasiliana kama serikali ya MAJIPU?