Ukiangalia kwenye macho ya sheria unaona mwanga fulani wa Haki, Mwanga wenye matumaini kwa wananchi wake! Sijui ni kwa namna gani watu wanajaribu kuipindisha miale hii ya mwanga huu mzuri na kuitia MAKENGEZA ili hakii ionekane kuwa ni mbaya kwa watu wake.
Hongereni sana wale wote mlioiona hii nuru hata pale wale walipotaka kuwatia makengeza na kujaza ukungu machoni na mioyoni mwenu, mlisimama na kutafuta Miwani ile yenye kuona vizuri huo mwanga! Mkasimama mkasema HAPANA njia ni hii!
Si wengi walio upande wa pili wataweza kukubaliana nanyi ila iko siku watautambua ukweli! HAKI ITABAKIA KUWA HAKI HATA KAMA ITACHELEWESHWA!
Mungu uwabariki wote hata wale waliokuwa hawataki haya yatimie.