Nampa hongera sana kamanda Lema na Chadema kwa ujumla kwa matokeo haya. kimsingi, mahakama ya rufaa imejielekeza vizuri, hukumu hii imeendelea kuipa heshima kubwa mahakama ya rufaa ya Tanzania.
Hongereni sana majaji kwa hukumu hii, mmetumia taluma zenu kuzuia upotoshaji uliofanywa na mahakama kuu amabao endapo msingeupatia tiba nzuri, ungekuja kuwatesa watu wengi kwa kuwanyima haki zao.
Swali langu nikuwa vipi kuhusu mishahara ya Lema, inamaana atalipwa mishahara yote iliyokuwa imezuiliwa baada ya mahakama kuu kutengua ubunge wake au alikuwa akiendelea kulipwa mshahara hadi katika kipindi alichokuwa anasubili rufaa? Mwenye jibu tafadhali!