Lema ashinda rufaa dhidi ya ubunge wake!

Lema ashinda rufaa dhidi ya ubunge wake!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,018
Reaction score
20,489
Leo mahakama imefurika mapema, hali ya hewa ni nzuri,

Updates:

- Bado hukumu haijaanza kusikilizwa, nyuso za wakombozi zimejaa bashasha. Hii ni dalili nzuri kwa kupokea matokeo!

- Viongozi wote wachadema ndio (Mh Mbowe na waambata wote) wanaingia, watu pipooooziii

- Kamanda Lissu ndio anaingia watu pipooziiii

- Naaam kamanda, Ben Saanane ndio anaingia. Sasa kazi mtindo mmoja, ukombozi unakaribia

- M/kiti wa Bavicha Heche ameshawasili eneo la tukio. Bado tunawasubiri majaji tu

DSC00029.JPG

Lema, Mbowe na Mnyika wakiwa Mahakamani

DSC00031.JPG

Hawa ndo waliofungua kesi

More Updates:

- Tumeamriwa kuzima simu zote, sasa majaji wanaingia,

- Kwanza hukumu inaanza kusomwa!

- Kwanza inasomwa historia ya kesi hii, tukio kwa tukio

- Mtanisamehe sitaripoti kila kinachotamkwa na msoma hukumu, naripoti yale muhimu tu, mfano vifungu vinavyo muingiza au kumtoa mrufani na hitimisho la mahakama tu!,

- Mahakama imejiridhisha kuwa madai ya udharirishaji hayakuathiri uchaguzi wala mlalamikaji (CCM)

Tumeshindaaaaa!

Tangu sasa Lema ni mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema,

CCM wameamriwa kulipa gharama za kesi hii tangu ilipofunguliwa mpaka ilipoishia!

Hiyo ndiyo habari.
Mahakama ya Rufaa imeona kuwa hoja madai ya washitaki hayakuathiri mwenendo wa uchaguzi.

Picha baada ya ushindi:
DSC00054.JPG

DSC00067.JPG

DSC00078.JPG


[video=youtube_share;Jv0H_81TCoI]http://youtu.be/Jv0H_81TCoI[/video]
 
Tuhabarishe yatakayojiri toka huko mkuu.
Try to your best levels.
 
Leo mahakama imefurika mapema, hali ya hewa ni nzuri,

Kamanda Yericko Nyerere walete walete hao majaji,na kwa sababu umethibitisha kwamba hali ya hewa ni nzuri basi tunaamini tayari mambo ni mazuri,ila wale wanaoendelea kulumbana watuvumilie kwanza kwa muda wasiingize zile Thread zao za kujibizana kwa sababu najua kuna mwingien naye leo anakuja kumwagika humu,wasubiri kwanza tukishamaliza masuala ya hukumu basi waje humu tena tuanze kuona mnyukano wao.
 
Kama unariport wewe mkuu YERIKO basi natumai tutapata habari nzuri wapi mkuu BEN SAANANE?
 
Back
Top Bottom