Lema amwomba Slaa agombee Arusha Mjini

Lema amwomba Slaa agombee Arusha Mjini

cdm wameanza. Kila mmoja anataka kuingia bungeni kusaka umaarufu ili agombee uraisi 2015. mara zzk mara slaa mara mbowe. Haya yetu macho

Mkuu hayo maneno ya Mbowe au Dr. Slaa kugombea urais umeyasikia wapi???.
Wala msipate shida AR kuna akina Slaa kibao na wala sio katibu mkuu.
Hilo la urais CDM analijua Zitto peke yake. Punguza kuwawekea watu maneno mdomoni mkuu!
 
Kama ni hivyo kwa nini wasimsimamishe mwana CDM wa hapo Arusha akachukua uwakilishi hadi waje huku Tegeta kumchukua boyfriend wa Josephine Mushumbusi mamaa ya pesa mingi?

sasa kwa hili utafichaje kwamba hupigwi kijiti,mlupo namba moja...
 
CCM hawatoitisha uchaguzi watapiga danadana maana akirudi rais wetu bungeni itakula kwao
 
MBUNGE wa zamani wa Arusha Mjini, Godless Lema amesema anatamani Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa agombea ubunge wa jimbo hilo akieleza anaamini atatoa mchango mkubwa zaidi kwa chama kabla ya mwaka 2015.

Lema alitoa kauli hiyo juzi usiku jijini Dar es Salaam, wakati wa harambee ya kuchangia chama hicho kwenye kampeni yake ya Vuguvugu la Mabadiliko maarufu kama Movement for Change (M4C) mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema katika chama hicho kuna watu wengi wanaoweza kuwa wabunge wa jimbo hilo, lakini yeye binafsi angependa Dk Slaa awe mbunge wa Arusha Mjini kwa sababu Katibu Mkuu huyo wa Chadema akiwa bungeni ni moto wa kuotea mbali.

Lema alisema: "Kuhusu ubunge wa Arusha sina hofu, atakuja Dk Slaa au mimi, ingawa sasa napenda aje Dk Slaa."

Alisema angefurahi kama Dk Slaa angekuwa mbunge wa jimbo hilo hasa katika kipindi hiki cha kutafuta mabadiliko kumpokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Lema alisema hivi sasa anafurahia mchango mkubwa anaoutoa katika chama chake akiwa nje ya Bunge.

"Nahisi kutoa mchango mkubwa katika chama nikiwa nje ya Bunge kuliko nilivyokuwa bungeni kwa sababu nimefanya shughuli nyingi zenye matokeo chanya katika taifa hili," alisema Lema.

Lema alienguliwa ubunge mwaka huu na Mahakama ya Kuu Kanda ya Arusha kwa kilichoelezwa kuwa alitumia lugha chafu katika kampeni za kuusaka ubunge huo mwaka 2010.

Kuchangia fedha za M4C
Lema alieleza kuwa fedha zitakazopatikana katika harambee hiyo zitatumika kununulia helikopta, magari, pikipiki, baiskeli na matumizi mengine ya Chadema kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa ukombozi kwa wananchi.

"Tusifanye siasa ili kutafuta vyeo bali tulenge kuleta mabadiliko chanya katika jamii iliyonyanyasika kwa muda mrefu. Nchi yetu ilipata uhuru, lakini sasa tunahitaji mabadiliko yanayowakomboa wananchi kutoka kwenye umasikini," alisema Lema.

Kauli ya Mbowe
Akizungumza katika harambee hiyo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kuwa, propaganda za ukabila, udini na rangi zinazoenezwa na CCM ni dhaifu na zimeshindwa kuidhoofisha Chadema.

Alisema kuwa wananchi wamezishtukia propaganda hizo na kwamba, wananchi wengi wamehamasika kutaka mabadiliko.

Katika harambee hiyo zaidi ya Sh270 milioni zilipatikana, kati ya hizo Sh250 milioni zikiwa ni ahadi na Sh20 milioni zikiwa ni fedha taslimu.

Kati ya fedha hizo, Sh20 milioni zilichangwa na tawi la Chadema nchini Marekani likiwa na majimbo yake Washington DC, Maryland na Virginia.

Watendaji wa Serikali
Kivutio kikubwa kilikuwa kwa baadhi ya watendaji wa Serikali kuchangia katika harambee hiyo na kutaka waitwe Wasamaria wema bila kutaja majina yao.

Mbowe alisema: "Kwa kuwa wananchi wametuamini, tumeacha njia ya maandamano na sasa tunataka kufika kila kata ya nchi hii ili kufikisha ujumbe wa mabadiliko kwa wananchi. "

Alisema kuwa wamekubaliana baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge wabunge wote wa Chadema watasambaa nchi nzima kueneza Vuguvugu la Mabadiliko.

Mwenyekiti huyo wa Chadema alisema kuwa mbali ya kufika kwenye kila kata chama hicho pia kimejipanga kufikisha ujumbe huo katika nchi zote ambako kuna Watanzania.

" Hatuna mchezo sasa, tumejipanga kuchukua dola ifikapo 2015, hawa CCM sasa ni kama wanaweweseka hawajui wanalolifanya, tutawang'oa tu," alisema Mbowe.

Alisema kuwa chama hicho kikifanikiwa kuchukua dola, kipaumbele kikubwa kitakuwa ni kuboresha elimu ambayo ni sekta muhimu kwa maendeleo ya taifa.

" Kipaumbele namba moja, mbili hadi tatu kitakuwa ni elimu. Tutawekeza zaidi kwenye elimu ili kuwawezesha wananchi kuhimili changamoto za dunia ya sasa hasa katika usimamizi wa rasilimali zao," alisisitiza Mbowe.

Aliwahimiza watu wanaokichangia chama hicho kwa kuficha majina yao kuacha hofu akisema: "Jitokezeni hadharani, hamna sababu ya kuhofu kama kweli mnahitaji mabadiliko. Tumepuuzwa, tumenyanyaswa na tumedhalilishwa kiasi cha kutosha, sasa basi tuache woga."

Alisema kuwa, CCM imeshindwa kuwasikiliza madaktari, walimu na wafanyakazi wengine lakini Chadema inaahidi kushughulikia matatizo ya makundi hayo.

Akizungumzia umuhimu wa harambee hiyo, Mbowe alisema mabadiliko yana gharama zake na kwamba wadau ndiyo wanapaswa kuchangia chama hicho.

Mbowe aliomba kila mpenda mabadiliko kuchangia kwa kadri ya uwezo wake na kwamba fedha zake zitailetea mabadiliko nchi hii.

Vyeo
Akizungumzia suala la nafasi za uongozi ndani ya chama hicho, Mbowe alisema kuwa, huu si wakati wa kugawana vyeo wala kutangaza nafasi za kugombea bali kukiimarisha chama ili kiweze kuwa na nguvu zaidi.

Naye Mwenyekiti wa M4C, Mkoa wa Dar es Salaam, Alex Mayunga alisema harambee hiyo ilikuwa na lengo la kukusanya Sh5 bilioni katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema katika hafla ya jana walipanga kupata Sh500 milioni, lakini hazikutimia kutokana na msongamano wa wananchi waliokuwa wakituma fedha kwa njia ya simu za mkononi.

"Tunadhani hadi kesho (leo) kiasi hicho kitatimia kwa sababu wananchi wengi wametuma fedha lakini bado hazijatufikia," alisema Mayunga.

Aliwataka wananchi kutuma fedha kwa kutumia njia ya simu za mkononi kwa sababu hiyo ndiyo njia rahisi.


Source: mwananchi
 
Tuwachie wanachama wa ARUSHA MJINI wachague wenyewe. yasije kuwa ya bwana ZITTO na SHIBUDA.
 
huyu lema ni mwehu anasema slaa anafaa kuwa mbunge wa Arusha, kama alijua hivyo kwanini alikata rufani si angeacha uchaguzi ukarudiwa?
 
Arusha hatuitaki ccm na wao wanalijua hata akisimama dhaifu na jiwe halafu hilo jiwe likapakwa rangi ya chadema..dhaifu miguu juu tunaimani na chadema.
 
M4C haitawabakiza ccm madarakani

itakuwaga historia tu ya kwmb tulikuwa na chama chenye jina hilo

kama ilivyokuwa KANU ya majirani zetu.
 
Magamba yanatamani yasingemvua Lema ubunge. Huwa hayasomi alama za nyakati na siku zote yanacheza pata potea
 
Lema ndio anawapangia kila kitu wafuasi wa Chadema Arusha.
 
Aiseee baba yangu mi nilipenda pale lema aliposema magamba hawata fika chrismass na alipo sema hii nchi ni laini kama maini
 
Nilikuwa siwaelewi chadema vzr ila sasa ndo nawaelewa ntawaunga mkono mpaka mwisho
 
Kwa Arusha ningekushauri ukae kimya, yasije yale ya Arumeru.

Mkuu kwa hiyo nyie Arusha akisema Lema nyie kama kondoo ni kufata tu...mie sina akili za kushikiwa wala siwezi kukaa kimya...mkuu wewe ndio kaa kimya una uwezo wa kupinga mawazo ya Lema.
 
Upuuzi tu, inamaana chama hakina watu wenye uwezo wa kuongoza jimbo la Arusha hadi Lema akatafute mtu Dar?

Mkuu wangu Ecoli hawa jamaa sijui vipi yaani Lema akisema kitu hawataki watu wahoji.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom