Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Mh mkuu wa mkoa Mrisho Gambo karibu jiji la Arusha, jiji linaloongozwa kwa umahiri na CHADEMA chini ya Kalisti Lazaro naibu meya Viola Licky na mbunge bab'kubwa Godbless Lema. Kwa kuwa mstahiji meya wetu amekwenda safari ya kikazi Ujerumani nadhani umetumia busara kubwa kumsaidia yafuatayo;
1- Kukabidhi hundi kwa vikundi vya kinamama na vijana ambavyo vimepata fedha hizo kutokana na mapato ya ndani ya jiji ambalo sisi madiwani 33 wa CHADEMA na 1 Abdul Tojo wa CCM tumeziidhinisha. Bahati mbaya wewe si mjumbe wa baraza la madiwani lakini utapewa taarifa juu ya fedha hizo.
2- Ongea vizuri na watumishi wa jiji chini ya mkurugenzi ili waongeze spidi na kasi ya kuendana nasi ili TUIPELEKE ARUSHA KULE WALIOTUAMINI NA KUTUCHAGUA WANAPOTAKA
3- Hili la kukutana na wazee na makundi maalumu ni jambo jema sana. Ila dhamira ya moyo wako haikusuti kukutana na WAPIGA KURA WETU wakati sisi madiwani TULIOCHAGULIWA NA WENGI unatukwepa? Ni lini tutakutana na wewe tuongee mustakbali wa ARUSHA YA CHADEMA, MBONA UNATUKWEPA? Au ni zile tetesi za wewe kutaka kugombea jimbo la Arusha 2020, HUONI NI SAWA NA WALE WALIOTAKA KUIRITHI KANZU YA YESU WAKATI MWENYEWE KAIVAA? Kama tetesi ni kweli UNAJIMUDU? Utafilisikia hapa mkuu ila karibu sana
4- Ni busara ufanye pia mikutano ya hadhara na umshirikishe DC DAQARO maana yeye ni diwani wa kata zote (kwa akili zake na amekuwa akisema) na alitukatalia wengi tusiongee mbele ya wananchi wetu alipokuja ktk ziara yake kwa sababu zake binafsi. MKISHAKUSANYA KERO KWA KUWA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA HAMNA BAJETI YA MAENDELEO MTULETEE KTK BARAZA LA MADIWANI PIA TUWAPATIE WABUNGE WETU WATATU (Mh Lema, mh Joyce Mukya na mh Catherine Magige) ili wapeleke bungeni ambako wewe huendi kwa ajili ya utatuzi.
5- Na mwisho ukague miradi TULIYOPIGANA KUITEKELEZA ili wewe mkuu na wengine wasiopenda kusema ukweli kuwa Arusha chini ya CHADEMA tumepiga mzigo wa maana ambao haukuwahi kufanyika muda wote mlipokuwa mnatekeleza ilani yenu ya CCM ambayo 2015 Arusha waliigomea COMPLETELY!!! Nashauri upige na picha mkuu ili UMDHIBITISHIE MH RAIS MAGUFULI KUWA WATOTO KIUMENI WAMEDHAMIRIA UTUMISHI ULIOTUKUKA!
#TUKUTANE_FIELD_______HAINA_KUFELI_CHIEF!!!!!!
By Binamu Bananga