Nteko Vano,
..lakini Mkapa alikuwa mbunge huko kusini kwa miaka mingi sana. nini ilikuwa rekodi yake kama mbunge??
..pia lets look at the big picture: hivi kweli ni halali kwa mikoa ya kusini kusubiri miaka 40++ toka uhuru kujengewa hiyo barabara na daraja??
..tatizo siyo kwamba CCM hawafanyi kitu, wanafanya lakini ni kwa kasi ya konokono. hawana ubunifu and they think they have all the time in the world.
..mikoa ya kusini hali inasikitisha. anazaliwa mtu kwenye nyumba ya makuti, mpaka anapata vitukuu navyo vinaishi kwenye nyumba ya makuti, and yet tunasema tuna serikali ya wananchi na wasomi kutoka eneo hilo.
..Mkapa kuwa Raisi wa Tanzania nzima haimaanishi na wala haihalalishi mikoa ya kusini kukosa barabara na huduma nyingine muhimu, au zao la korosho kutelekezwa na wananchi kugubikwa na umasikini.