Lema amvaa Mkapa, yeye (Mkapa) ajitetea... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lema amvaa Mkapa, yeye (Mkapa) ajitetea...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, May 31, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,548
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Mkapa atoa siri ya mafanikio, Lema amvaa

  RAIS Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, ameeleza siri ya mafanikio ya uchumi na siasa ya Serikali yake, miaka kumi aliyokaa madarakani kuwa ni uwazi na ukweli katika mambo yote hata magumu yaliyoikabili Serikali.

  Akizungumza kwenye mjadala maalumu kuhusu uwekezaji barani Afrika, ulioandaliwa na Taasisi ya Uwezeshaji na Uwekezaji (ICF), Mkapa aliyetambulika enzi zake kama Mzee wa uwazi na ukweli, alisema sera hiyo ilimsaidia kupata uungwaji mkono kutoka kwa umma ambao ulipewa fursa ya kujua mazuri na mabaya yaliyokuwa yakitokea na njia ya kukabiliana nayo.

  "Uwazi na ukweli ulisaidia kuwapa wananchi taarifa sahihi kuhusu hali ya uchumi, fedha na changamoto zote zilizoikabili Serikali na wao kupata fursa ya kushiriki kuzitafutia ufumbuzi," alisema Mkapa.
  Alitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni kuwawezesha kiuchumi wanawake na vijana ambao ndiyo idadi kubwa ya wananchi sehemu nyingi duniani.

  Hata hivyo, wakati Mkapa akitamba kwa mafanikio hayo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Goodless Lema, ‘amemvaa' na kumtupia lawama kutokana na umaskini uliotopea Mtwara licha ya mkoa huo kuwa na utajiri wa kutisha.

  Akihutubia mkutano wa hadhara Kijiji cha Mangamba, Kata ya Likonde, Wilaya ya Mtwara jana, Lema alisema Mkapa licha ya kuongoza taifa kwa miaka 10, alishindwa kuwawezesha wakazi wa mkoa huo kuondokana na umaskini.

  "Mkapa amekaa madarakani kwa miaka 10 lakini Mkoa wa Mtwara umeendelea kuongoza kwa umaskini nchini," alisema Lema na kuongeza:

  "Leo nimepata jibu kwa nini Mkapa ameukimbia mkoa huu, hataki kuishi hapa, nimetembelea Kijiji cha Namayanga na kujionea umaskini unaotisha."

  Alisema wananchi wa Mtwara hawapaswi kuvitazama viashiria vya maendeleo kama majengo ya ghorofa yaliyopo Dar es Salaam, bali kuitazama hali yao ndani ya mkoa alikozaliwa Mkapa.Lema ambaye alikuwa Mbunge wa Arusha Mjini kabla ya ushindi wake kutenguliwa na mahakama, alisema kushindwa kwa Mkapa kufikia matarajio ya umma, kunaweza kutumika kama kigezo cha kumuombea dua mbaya.

  "Mkapa ameiongoza nchi hii kwa miaka 10 akiwa Rais, leo hii Mtwara ni aibu tupu watu wa hapa wanaishi katika nyumba za nyasi na udongo zinazotaka kudondoka, bila elimu wakitembea pekupeku na kushindwa hata kumudu kununua malapa ya Sh700," alisema.

  Alisema Mtwara ina rasilimali za asili kama bahari, gesi, ardhi yenye rutuba kwa kilimo cha korosho, mafuta na bandari yenye kina kirefu, lakini bado inakabiliwa na `umasikini wa kutupwa.'
  Lema alisema kutokana na umaskini huo, Mkapa ambaye ni mzaliwa wa Kijiji cha Lupaso, wilayani Masasi, ameamua kukimbia mkoa kwenda kuishi Lushoto, mkoani Tanga.

  Alisema hata wa watoto wao wameishia mitaani kufanyabiashara ndogo za korosho, maji, mitumba na nyinginezo zinazodhalilisha utu wa binadamu kutokana na kukimbia maisha magumu mkoani humo.
  "Leo hii Machinga kila mahali, hili ni zao la wanaMtwara kutokana na kupumbazwa kielimu hawataki watoto wenu wasome waweze kufunguka akili zao na kudai haki," alisema.

  Alisema badala yake watawala wanawanyonya haki zao ikiwamo kuwakopa wakulima wa korosho, hivyo kusababisha mzunguko mdogo wa fedha.

  Alisema kama mzunguko huo ungekuwapo, wakulima wangeweza kuwalipia watoto mahitaji yao kama ada za shule, lakini kwa vile hilo halifanyiki, wamebaki kuwa mbumbumbu na kutawalika kwa rahisi.
  Aliwataka wakazi hao kuachana na CCM kutokana na kuendelea kuwapumbaza kwa zaidi ya miaka 50 na kujiunga na Chadema kupigania mabadiliko ya nchi.

  Katika hatua nyingine, Lema alisema ataandaa maandamano makubwa mjini Arusha kutaka watu wote waliomo magerezani mkoani humo wanaokabiliwa na kesi mbalimbali za wizi wa kuku, sigara, ubakaji, ujambazi na wahalifu wote kuachiwa huru iwapo Serikali ya CCM haitawafikisha mahakamani mawaziri waliojiuzulu wanaodaiwa kutafuna zaidi ya Sh9 bilioni za umma.

  "Haiwezekani hawa wezi wa mabilioni ya shilingi waishie kujiuzulu, huku maskini ambao wengi wamefungwa kwa kesi za wizi wa kuku na wengine kufungwa kwa kusingiziwa... nao waachiwe huru kama walivyoachiwa mawaziri wanaotuhumiwa kuiba mali ya umma," alisema.


  CHANZO: Mwananchi
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,548
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Hivi ni mafanikio yapi ambayo Watanzania waliyoyaona wakati wa awamu ya Mkapa?

  Ikumbukwe aliingia madarakani kwa mbwembe za kujiita Mr Clean kisha akaunda Tume ya Warioba kuchunguza tatizo la rushwa nchini na kuja na mapendekezo ya jinsi ya kupambana nayo. Baada ya kukabidhiwa ripoti ile haikufanyia kazi na kuaicha ipigwe na vumbi pale Ikulu huku yeye na Serikali yake wakiendeleza ufisadi.

  • Aliwaingiza makaburu wa Net Group Solutions wauza stationeries toka RSA kwa mtutu wa bunduki pale TANESCO ambao hawakujua chochote kuhusiana na umeme na kuwapa management positions na kuwalipa mabilioni ya pesa za walalahoi.
  • Aliuza mashirika yetu mbali mbali ikiwemo NBC kwa bei ya kutupa kwa kile kilichoitwa ubinafsishaji na hadi leo hii hakuna matunda yoyote ya tunayoyaona ya sera ile ya Mkapa
  • Kashfa za EPA, Kagoda na Meremeta zote zilitokea wakati Mkapa akiwa madarakani
  • Alihusika katika ununuzi wa rada ambayo baadaya ilikuja kufahamika kwamba ilikuwa imenunuliwa kwa ufisadi wa hali juu....kumbukeni kauli ya Mramba, "hata majani tutakula lakini rada ni lazima inunuliwe."
  • Alihusika katika kumpa zabuni shemeji yake katika uuzwaji wa mali mbali za posta na simu zikiwemo nyumba
  • Alihusika katika ukwapuaji wa nyumba za Serikali ambao umeingiza Serikali katika hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 300 and counting
  • Alihusika katika kununua ndege bomu ya Rais huku akiwa amebakisha miezi mitatu kumaliza awamu yake.
  • Ununuzi wa helicopters na magari ya jeshi ambao ulijaa ufisadi wa hali ya juu ulifanyika katika awamu yake.
  • Hakukuwepo na ongezeko la ajira kwa Watanzania na hii ilisababisha Watanzania waiite awamu yake awamu ya Ukapa
  • Hakukuwa na ahueni yoyote katika upatikanai wa maji, umeme, matibabu au elimu. Upatikanaji wa maji ulikuwa bado ni wa shida katika mikoa minngi nchini na hali kadhalika umeme. Hospitali zetu nyingi zilikuwa hazina dawa, vifaa muhimu na vitanda vya kulalia wagonjwa vilikuwa adimu na hivyo wagonjwa wengi kulala chini au wagonjwa hadi saba kulalia kitanda kimoja au godoro moja.
  • Mishahara ya Wafanyakazi wengi nchini bado ilikuwa ni duni sana na haikuendana na gharama halisi za maisha
  • Wanafunzi wengi bado walikuwa wanahudhuria shule ambazo hazikuwa na hadhi ya kuitwa shule na wengi walikaa chini na hawakuwa na walimu wa kutosha
  • Pia Mkapa alihusika katika ukwapuaki wa Kiwira Coal Mining na pia kufanya biashara akiwa Ikulu.

  Tunaona Mkapa anavyojarbu kutaka kujipandisha chart kwamba awamu yake ilikuwa na mafanikio. Je, kama kulikuwa na mafanikio katika awamu ya Mkapa ni mafanikio yepi yaliyopatikana wakati wa awamu ya Mkapa ambayo Watanzania hawakuyaona hadi kutamka, "Mkapa kaleta ukapa?"
   
 3. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Hadi sasa katima magari 680(iveco) yualiyoidhinishiwa fedha ni 510 tu yalinunuliwa tena ni katika wakati wake,
   
 4. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  hayo nayo maneno
   
 5. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wizi wote na ufithad wote huu umezaliwa wakat wa mwinyi ukalelewa na kukua mikonon mwa n,jomba mpaka na kunenepa na kuota miziz kwa bw.jk2,
   
 6. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hii hali ya wizi ipo tokea enzi za mwinyi ila walikuwa wamezuia mawasiliano kati ya raia na serikali yaani walikuwa wanakula na kipofu huku hawamshiki mkono ndio maana watz walikuwa wanajionea afueni.

  kwa upande wa ankoli jakaya yeye kaaribu kwa kula huku anamshika mkono kipofu na mbaya zaidi kasaidia katika uuawaji wa chama wao wanakiita cha mapinduzi. Kinachoonekana hapa nikuwa mkapa na ndio wameanza halafu baba riz ndio kamalizia kabisaa.

  RIP Tanzania!
   
 7. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  hukumu ya rufaa yake inatolewa lini? Tafadhali
   
 8. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  haiusiani na mada,sawa ndugu.
   
 9. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  hivi unajiteteaje kabla ya kushambuliwa? maana kulingana na post yako mkapa ndiye alizungumza kabla ya lema!
   
 10. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kamanda Lema yupo honeymoon,lakini hukuhuko ndio analeta maangamizi makubwa je akitoka likizo akarudi kazini rasm!....patakuwa hapatoshi
   
 11. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Namkubali sana lema..cjuh nimpe nini
   
 12. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #12
  May 31, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Kujitetea na kushambuliwa kwa mkapa ni hoja endelevu mwanzo wake ni siku alipokabidhi madaraka, haina mwisho, na yeye anajua ndio maana kila akipata nafasi ya kuongea atahakikisha anatengeneza mazingira ya kuelezea mafanikio ya serikali ya awamu ya tatu hata kama ni msibani.
   
 13. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #13
  May 31, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Ni kweli kila mtanzania anayo haki ya kuishi popote pale nchini, lakini hii ya Mkaahapa kuikacha Mtwara na kwenda kuishi Tanga ni ajabu inayoandamana na aibu!

  Yeye kama kioo cha Taifa hakutakiwa kufanya maduguri hayo, kwanini asimwige Nyerere?
  ...hii inaonyesha dharau aliyo nayo juu ya mahala anakotoka.

  Lema ana substance kubwa sana kwenye vidonge anavyompa Mkapa!
   
 14. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #14
  May 31, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  mpe tigo
   
 15. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #15
  May 31, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mkapa hua akiongea ananipa kichefuchefu maana anaongea utafikiri alikua Rais wa UK...
   
 16. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #16
  May 31, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kwenye msako wa nyani ngedere hawezi kusalimika!
   
 17. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #17
  May 31, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  mkuu kwanini aigwe nyerere..???!~!

  .. lol.. hehehe!
   
 18. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #18
  May 31, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  kuna wananchi wenye akili mbovu,hata kama analala njaa,hana nguo,hana nyumba akipata mtu wa kijijini kwao kiongozi hata kama hamsaidii kwa lolote anaona fahari sana. Ukimtukana/kumsema huyo kiongozi yuko tayari kukuchinja. Nina wasiwasi watu wa ntwara wako hivo. Inabidi kuwa makini,unawezakuta unakimbiwa badala ya kukimbiliwa. Ni sawa na leo uende msoga ukawaambie jk ni bomu!!!
   
 19. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #19
  May 31, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,787
  Likes Received: 36,795
  Trophy Points: 280
  Lema amevuka ujembe sasa amekuwa sururu, may god bless godbless lema.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 20. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #20
  May 31, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kazi kweli kweli angeendeleza mkoa kwa kasi wangesema anapendelea kwao yaani Mkapa mbinafsi. Maana tumeshaanza JK kasema bagamoyo kujengwe bandari na kiwanja cha ndege tayari tunasema hili mara lile. Jamani, ukiwa rais wa TZ unatakiwa kuangalia masuala ya nchi. Nakumbuka wazee wa mkoa walimuita Mkapa wakamuuliza mzee mbona unatutupa huku umaskini umekithiri sana.... Mkapa aliwajibu kuwa yeye sio rais wa kusini bali wa Tanzania. Akasema, serikali inawajengea barabara ambayo miaka yote imekuwa tatizo na zinajengwa barabara na miundombinu kuunganisha mkoa na mikoa mingine kama ruvuma, pia kusini na msumbiji kuna daraja litajengwa pamoja na utafutaji wa rasilimali gas kwa ajili ya umeme hivyo hivi vitakuwa chachu ya maendeleo kwa kanda hii. Zaidi ya hapo nifanyaje? Hata bodi ya korosho kipindi kile iliimarishwa. Akasema shirikianeni na wabunge wenu pamoja na mawaziri wangu wanaotoka huku kulisukuma gurudumu la maendeleo na wananchi waamke na kujituma kikubwa waende shule. Lema kwa hiyo kauli sikusapoti na usirudie tena maana ni ubaguzi kwa watazania wengine, ina maana rais akitoka AR akazane huko umaskini uishe? akifanya hivyo atabalance vipi na mikoa mingine?.
   
Loading...