Na mm nimepigwa butwaa!Meseji ya Ben Sananee ipo wap . . ?
Na mm nimepigwa butwaa!Meseji ya Ben Sananee ipo wap . . ?
Hayo ndio matatizo ya wapiga kura wa arusha mjini waliyomtuma akaongee bungeni?
Kuna msemo what goes around comes around! Usifikiri suala hili ni jepesi kwamba mwathirika anaweza kuwa mwathiriwa kirahisi.Pengine Ben katekwa kweli. Pengine kauawa. Hatujui. Lakini binafsi sikupenda suala hili lilivyoshughulikiwa na CHADEMA yenyewe. Yaani halikupewa uzito unaostahili kabisa tangu let go. Kulikuwa na mzaha mzaha mwingi sana. Kama Mbowe asingeenda Ulaya na badala yake yeye, Lissu na wengineo wakawasha moto bila woga, naamini Ben pengine angekuwa ameshapatikana. Tumeona moto uliowashwa kwa akina Roma. Japo nao mpaka sasa hatujui kilichowapata lakini angalau walipatikana. Na hili ndilo jambo la muhimu zaidi.
Baada ya muda Kubenea naye akaibuka na Mwanahalisi yake: Eti Msaidizi wa Mbowe kuibuka. Hii ilitoa picha mbaya sana kuwa pengine Ben amekuwa victim wa msigano wa kimadaraka huko Chadema. Inasikitisha sana kama kijana huyu msomi amekuwa mhanga wa siasa zetu hizi zisizo na kichwa wala miguu. Damu ya mtu haipotei kamwe na haki na ukweli hata ufichwe na kucheleweshwa vipi siku moja utajipambanua tu. Kama ni vyombo vya dola ndiyo vimemteka na kumfisha hatimaye ukweli utajulikana na historia itasema ukweli. Kama chama chake kimemficha ili siku moja kimuibue kama shujaa napo itajulikana tu. Sad!![]()
Hayo ndio matatizo ya wapiga kura wa arusha mjini waliyomtuma akaongee bungeni?
...
“Uhuru wa habari ni altenative (mbadala) ya amani, si kikwazo cha amani. Watu wanapoongea wanatema nyongo, ‘wanarealise tension’. Leo tunapotaka kujadili mambo ya msingi, mnatumia nguvu na uwezo mlio nao, mtashinda,” alisema Lema. ...
“Unapozuia haki, unapozuia uhuru, unapozuia kweli unatengeneza balaa katika taifa hili. Tunalalamika kwa sababu familia zetu zinaishi hapa, tungekuwa na mpango wa kuondoka tungeenda kulalamikia Marekani ...
Maneno ya hekima kabisa. Mwenye masikio na asikie neno ambalo Lema kawapatia CCM.
Hakika Lema amekomaa sasa
Maneno yanagusa sana.
Huwezi kunyamazisha watu wanaosimamia ukweli milele.
Umehakiki cheti?Naona Lema anahekima sana ila hajui anachokipigania ndio tatizo. Natamani kama nchi ingekuwa na chama cha wanaharakati wa ukweli kama hawa wakitetea maslahi ya umma badala ya kale ka saccos ka mtu na baba mkwe wake. Inaumiza sana kwa kikundi cha familia furani kutumia mpaka damu za watanzania eti leo lema yuko radhi kumwaga damu yake kwa faida ya ka saccoss kweli CHADEMA mmerogwa na aliye waroga anawageuza kama anavyotaka
Mabox!Lema aanika meseji ya Ben Saanane
www.ippmedia.com/sw/habari/lema-aanika-meseji-ya-ben-saanane
Akichangia mjadala wa makadirio ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Lema alisema: “Kama itanyesha mvua ya radi basi itaambatana na mwanga na cheche zitazowamulika walaghai, watesaji na watetezi wa haki watapata mwanga katikati ya giza totoro la unyanyasaji.”
Mbunge huyo alisema maneno hayo ni ujumbe wa mwisho ya Ben Saanane ambaye hajui kama ni marehemu ama yupo hai.
“Lakini hata kumjadili humu haturuhusiwi. Nje mikutano ya hadhara hatufanyi. Kama kijana wa miaka 16 katika Taifa ambalo halina uhuru wa vyombo vya habari, halina chama cha siasa aliandika maneno machache tu “Assad must go, Assad will be next, leo Syria haina amani,”alisema.
“Uhuru wa habari ni altenative (mbadala) ya amani, si kikwazo cha amani. Watu wanapoongea wanatema nyongo, ‘wanarealise tension’. Leo tunapotaka kujadili mambo ya msingi, mnatumia nguvu na uwezo mlio nao, mtashinda,” alisema Lema.
Alisema kila jambo wanalotaka kulipitisha kwa wingi wao watashinda.
“Katika mchango wangu uliopita, nilisema Mungu hadhihakiwi, apandacho mtu ndicho avunacho,”alisema
Alifunguka kuwa alipokuwa gerezani, vijana waliokamatwa kwa makosa ya mtandaoni ni wengi na walikamatwa kimya kimya.
“Wanapelekwa mahakamani wanasomewa mashitaka bila ndugu zao kuwapo. Vijana wamejaa magerezani kwa sababu ya ukosoaji,” alisema na kuongeza kuwa haiwezekani kuwa na taifa lenye amani bila kuwa na uhuru wa habari.
“Msifikiri mnatunga sheria kutukomoa sisi. Mna watoto wanakua, wajukuu wanakua…Tunapopigania uhuru wa habari hatupiganii Chadema, CCM tunapigania taifa bora na huru,” alisema.
“Leo ndani ya bunge hatusemi, kwenye mitandao hawaongei, vyombo vya habari havitasema huko mitaani mikutano ya hadhara imezuiwa. Iko siku watu wataingia mitaani kudai uhuru mnaowanyima.
Alisema watu hao watakuwa hawajatumwa na Chadema wala CUF na siku hiyo kila mtu atatafuta nyumba ya kujificha.
“Unapozuia haki, unapozuia uhuru, unapozuia kweli unatengeneza balaa katika taifa hili. Tunalalamika kwa sababu familia zetu zinaishi hapa, tungekuwa na mpango wa kuondoka tungeenda kulalamikia Marekani.
“Tukisema miongozo ni mingi na sijui hata hotuba yangu itakuwaje. Kama hotuba ya Waziri wa habari na michezo mmeifanya hivi, hotuba ya waziri wa mambo ya ndani na uzoefu wa Lijualikani alipokuwa magereza na uzoefu wangu nilipokuwa magereza mtaanza kuizuia kwenye salamu.
“Wabunge mko wengi tusaidieni, mawaziri tusaidieni tukishamalizwa sisi, msumeno utakaofuata utakuwa kwenu. Ni nini mnakipigania waheshimiwa wabunge, kita kitu kinakuwa hovyo. Ni fedha?,” alihoji.
Lema alisema utu wa mtu haupimwi kwa ghorofa, cheo, bali unapimwa kwa kazi na wajibu alioufanya duniani.
“Mimi nilikamatwa nje hapo getini nikapelekwa Kondoa nikaweka ‘lock up’ (rumande) saa 4:00 hadi saa 8 usiku nikapelekwa Arusha nikatengwa chumba peke yangu, nikakaa jela nikatoka baada ya miezi minne. Mnaweza kufanya hivi leo,” alisema.
Lema aliongeza kuwa: “Mimi mkitaka kuniua niueni leo, kesho ni mbali. Mkitaka kumuua yeyote hapa muueni leo, kesho ni mbali. Haya mambo mnayotuzuia kuyasema mnafikiri tunasema tunapenda uwanaharakati.”
Alieleza kuwa ana mtoto wa kwanza ana miaka 11 na wa mwisho ana miaka minne na angependa kuona ndoa na harusi na elimu za watoto wake kwa macho yake.
“Lakini ikibidi nisione hiyo harusi kwa sababu ya kupigania ya ninachokipigania watakumbuka maisha yetu bungeni kupigania property (mali). Yalipigania haki na msingi wa taifa hili ambayo mmeishindwa,” alisema.
Alisema ni muhimu wanaokalia Kiti cha Spika wakaacha faraja, baraka na kuacha kutumia wingi wa wabunge wa CCM.
“Hapo alikaa Mzee Sitta leo ni marehemu, kila mtu atapita kwa wakati wake. Ni muhimu mkapita mkaacha faraja nyuma, baraka acheni kutumia wingi wenu vibaya. Simbachawene wewe una historia. Ulikuwa kondakta Mungu amekuweka mpaka umekuwa hapo, tulitarajia kukuona wewe unapigania nchi hii.
“Leo unaishi utafikiri umezaliwa katika familia ya Warren Bafet. Mtu akisimama kuongea ukweli unapinga.
Wewe siku zote huna tofauti na vichaa wa Mirembe.Hayo ndio matatizo ya wapiga kura wa arusha mjini waliyomtuma akaongee bungeni?
Hebu tafakari vizuri, hoja nyingi wanazojenga wabunge bungeni zinafuatwa?
Niliowanukuu mna hoja moja tu kuu, uhuru wa kusema na kuandika lolote bila mipaka.
Ebu tuwe wa kweli na kujiuliza:
Hivi kweli wawakilishi wetu hawana jambo la msingi (kero za maendeleo) la kuzungumzia ila linalogusa maslahi yao binafsi (uhuru usio na mpaka wa kusema lolote)?
Mh Lema, hajakomaa kisiasa, kama ninyi niliowanukuu mnavyoamini. Laiti angetumia maneno yake ya hekima[/V] kuhamasisha wapiga kura wake kwa masuala ya maendeleo, nami ningeungana nanyi kumpa sifa zinazostahili. Lakini maneno yake ya hekima[/V] yamejaa vijembe na chuki iliyo wazi km ’ Leo tunapotaka kujadili mambo ya msingi, mnatumia nguvu na uwezo mlio nao. Kwa lugha kama hiyo, hakika hupewi nafasi ya kuongea katika jamii
Kuna mwalimu shule ya msingi alikua anasema " ukiamua kuniloga, hakikisha nnakufa, ukinikosakosa hautabaki salama"..the return of GL.
dah“Leo unaishi utafikiri umezaliwa katika familia ya Warren Bafet. Mtu akisimama kuongea ukweli unapinga.
Hebu tafakari vizuri, hoja nyingi wanazojenga wabunge bungeni zinafuatwa?
Usijifanye mjuaji ilhali unaandika utumbo tu
Kuna kipindi huwa nakaa nafikirii mtu mwenye ufahamu duni kama huu, kama anatumia computer kuandika hata kufungua account aliwezaje.
"..kama itanyeesha mvua ya radi... "Meseji ya Ben Sananee ipo wap . . ?