Lema aanika meseji ya Ben Saanane

Lema aanika meseji ya Ben Saanane

Nawaaambia mkiwanyamazisha hawa wanaoongea ukweli hakika mawe yataongea!!
 
Siku hizi Ukawa wana CD mbili tu!

Moja ya Bashite nyingine ya Ben saanane, ya Kinana kila wakijaribu kuicheza Ina scratch
Ndicho ulichokiona kwenye ujumbe wote huo? Mungu akurehemu
 
Meseji ya Ben Sananee ipo wap . . ?
Bw. Mandella haulitendei haki jina la mwanamapinduzi mkubwa kuwahi kutokea Afrika. Unauliza swali ambalo jibu lake liko kwenye "paragraph" ya kwanza ya "thread". Ama haukuwa makini uliposoma hiyo "thread" au ulisoma kwa mrengo wa kutafuta makosa na ukashindwa kuona nukuu ya maneno ya Ben Saanane.
 
Mh Lema umeniliza machozi. Mungu wetu mwema akulinde daima.
 
Lema kaongea mpaka nimelia

Dunia hii haihitaji vilio bali ukakamavu na ushujaa wa kusema jambo kwa uwazi. Ukilia bado hujasaidia kumuunga mkono bali simama na upambambane kwa hoja na hata kwa silaha kama ikishindikana.
 
Hapo ndipo huwa namkubali Lema.

Anaweza kuwa na kasoro na madhaifu mengine lakini Lema sio mwoga na huwa anasema jinsi inavyotakiwa kusemwa. Na sio kusema tu bali kuishi na kutembea kwenye hayo maneno.
Lema angekuwa si mwoga angeendelea na kauli zake za awali za kusema "NI HESHIMA KUBWA KUMZOMEA FISADI LOWASA". Kama si mwoga mbona kanywea kuutamka uovu wa Lowasa aliokuwa akiuimba kila wakati?
 
Maneno ya hekima. Ukweli mchungu kwa wadhalimu. Unabii utakaotimia!

Kudos GL
 
Lema angekuwa si mwoga angeendelea na kauli zake za awali za kusema "NI HESHIMA KUBWA KUMZOMEA FISADI LOWASA". Kama si mwoga mbona kanywea kuutamka uovu wa Lowasa aliokuwa akiuimba kila wakati?

Huo ni mtazamo wako kwa miwani ya kiitikadi. Nazungumzia Taifa la Tanzania na wnanchi wake bila kujali hizo itikadi.
 
Ndio matatizo ya Jimbo la Arusha?
Hivi mbunge kila siku anazungumzia matatizo ya jimbo lake tu? Cosato Chumi juzi kawachana TFF na hadi magazeti yakauza sana, hivi hayo ni matatizo ya wana Mafinga? Very poor thinking capacity, the only thing you know ni kutumia computer na simu tu but kufikirii waachie wengine dogo.
 
Lema kaongea mpaka nimelia
Kipi kimekuliza? Kulia ni hulka ya mtu kuna watu wameumbwa nayo wengine hata wakifiwa na wazazi wao machozi hayatoki. Hivyo haina maana kulia kwako kumethibitisha kitu chochote. Kuna jamaa alikua anawaadhibu watoto wake wakilia na yeye hujifungia ndani kulia labda na wewe una emotions kama huyu jamaa.

Hili suala la Beb Saanane ni zito sana na hakuna sababu ya CHADEMA kulitumia kama mchezo wa kujijenga kisiasa wakati na wao pia wana hoja ya kujibu. Inakuaje Bongo flava wamevalia njuga suala la msanii mwenzao wakati CHADEMA walikaa kimya na kufanya safari za nje kana kwamba hakikutokea kitu. Katika siasa kama hizi ni aibu sana kuitumia familia ya mtu kama mtaji wa kujijenga kisiasa.

Serikali pia inatakiwa kuwa makini wakati matukio kama haya yakitokea bila hatua zozote kuchukuliwa zinatupa picha mbaya sisi wengine ambao si wanasiasa na tunataka ustawi wa maisha yetu bila kuogopa nini kitatutokea.
 
Hayo ndio matatizo ya wapiga kura wa arusha mjini waliyomtuma akaongee bungeni?
Utakuwa na wazimu siyo bure! Hivi hayo matatizo yakitatuliwa wakati amani ina mashaka itakufaa nn?
Au akizungumzia hayo matatizo ya Arusha yatakuwa hayatatuki? Kila jambo na wakati wake kwa sasa ameona ni vema kuizungumzia hilo alozungumzia kuna ubaya?
Nyie ndo ambao mkimkuta mtu amepatwa shida njiani hamumsaidii eti nilikuwa na safari zangu!!!!!
Jaribu kuelewa shida na maumivu ya wengine.
 
kwa wataalamu wa kusoma fikra mbona hiyo sms ni kama product manufactured by LEMA himself....... kiukweli nikijoin kwa uwezo wangu na maneno ya BEN sipati kama aliye andika ni yeye LABDA kama aliandikiwa
Ni vizuri ungeandika aloiandika Ben .
 
Huyu Lema hapa arusha tumemchoka mpaka kero, tunamvumilia tu kwasababu ni jamii yetu chugga angekuwa mwingine labda kutoka Tarime huko tungekuwa tushamtimua kitambo
 
Lema aanika meseji ya Ben Saanane
www.ippmedia.com/sw/habari/lema-aanika-meseji-ya-ben-saanane

Akichangia mjadala wa makadirio ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Lema alisema: “Kama itanyesha mvua ya radi basi itaambatana na mwanga na cheche zitazowamulika walaghai, watesaji na watetezi wa haki watapata mwanga katikati ya giza totoro la unyanyasaji.”

Mbunge huyo alisema maneno hayo ni ujumbe wa mwisho ya Ben Saanane ambaye hajui kama ni marehemu ama yupo hai.

“Lakini hata kumjadili humu haturuhusiwi. Nje mikutano ya hadhara hatufanyi. Kama kijana wa miaka 16 katika Taifa ambalo halina uhuru wa vyombo vya habari, halina chama cha siasa aliandika maneno machache tu “Assad must go, Assad will be next, leo Syria haina amani,”alisema.

“Uhuru wa habari ni altenative (mbadala) ya amani, si kikwazo cha amani. Watu wanapoongea wanatema nyongo, ‘wanarealise tension’. Leo tunapotaka kujadili mambo ya msingi, mnatumia nguvu na uwezo mlio nao, mtashinda,” alisema Lema.

Alisema kila jambo wanalotaka kulipitisha kwa wingi wao watashinda.

“Katika mchango wangu uliopita, nilisema Mungu hadhihakiwi, apandacho mtu ndicho avunacho,”alisema

Alifunguka kuwa alipokuwa gerezani, vijana waliokamatwa kwa makosa ya mtandaoni ni wengi na walikamatwa kimya kimya.

“Wanapelekwa mahakamani wanasomewa mashitaka bila ndugu zao kuwapo. Vijana wamejaa magerezani kwa sababu ya ukosoaji,” alisema na kuongeza kuwa haiwezekani kuwa na taifa lenye amani bila kuwa na uhuru wa habari.

“Msifikiri mnatunga sheria kutukomoa sisi. Mna watoto wanakua, wajukuu wanakua…Tunapopigania uhuru wa habari hatupiganii Chadema, CCM tunapigania taifa bora na huru,” alisema.

“Leo ndani ya bunge hatusemi, kwenye mitandao hawaongei, vyombo vya habari havitasema huko mitaani mikutano ya hadhara imezuiwa. Iko siku watu wataingia mitaani kudai uhuru mnaowanyima.

Alisema watu hao watakuwa hawajatumwa na Chadema wala CUF na siku hiyo kila mtu atatafuta nyumba ya kujificha.

“Unapozuia haki, unapozuia uhuru, unapozuia kweli unatengeneza balaa katika taifa hili. Tunalalamika kwa sababu familia zetu zinaishi hapa, tungekuwa na mpango wa kuondoka tungeenda kulalamikia Marekani.

“Tukisema miongozo ni mingi na sijui hata hotuba yangu itakuwaje. Kama hotuba ya Waziri wa habari na michezo mmeifanya hivi, hotuba ya waziri wa mambo ya ndani na uzoefu wa Lijualikani alipokuwa magereza na uzoefu wangu nilipokuwa magereza mtaanza kuizuia kwenye salamu.

“Wabunge mko wengi tusaidieni, mawaziri tusaidieni tukishamalizwa sisi, msumeno utakaofuata utakuwa kwenu. Ni nini mnakipigania waheshimiwa wabunge, kita kitu kinakuwa hovyo. Ni fedha?,” alihoji.

Lema alisema utu wa mtu haupimwi kwa ghorofa, cheo, bali unapimwa kwa kazi na wajibu alioufanya duniani.

“Mimi nilikamatwa nje hapo getini nikapelekwa Kondoa nikaweka ‘lock up’ (rumande) saa 4:00 hadi saa 8 usiku nikapelekwa Arusha nikatengwa chumba peke yangu, nikakaa jela nikatoka baada ya miezi minne. Mnaweza kufanya hivi leo,” alisema.

Lema aliongeza kuwa: “Mimi mkitaka kuniua niueni leo, kesho ni mbali. Mkitaka kumuua yeyote hapa muueni leo, kesho ni mbali. Haya mambo mnayotuzuia kuyasema mnafikiri tunasema tunapenda uwanaharakati.”

Alieleza kuwa ana mtoto wa kwanza ana miaka 11 na wa mwisho ana miaka minne na angependa kuona ndoa na harusi na elimu za watoto wake kwa macho yake.

“Lakini ikibidi nisione hiyo harusi kwa sababu ya kupigania ya ninachokipigania watakumbuka maisha yetu bungeni kupigania property (mali). Yalipigania haki na msingi wa taifa hili ambayo mmeishindwa,” alisema.

Alisema ni muhimu wanaokalia Kiti cha Spika wakaacha faraja, baraka na kuacha kutumia wingi wa wabunge wa CCM.

“Hapo alikaa Mzee Sitta leo ni marehemu, kila mtu atapita kwa wakati wake. Ni muhimu mkapita mkaacha faraja nyuma, baraka acheni kutumia wingi wenu vibaya. Simbachawene wewe una historia. Ulikuwa kondakta Mungu amekuweka mpaka umekuwa hapo, tulitarajia kukuona wewe unapigania nchi hii.

“Leo unaishi utafikiri umezaliwa katika familia ya Warren Bafet. Mtu akisimama kuongea ukweli unapinga.


Lema bana, sikujua kama huyu jamaa ni slow learner wa ajabu namna hii. Tangu ameanza harakati zake kisiasa, mwanzo kwa kikwete, alikuwa angalau hata nafoka, siku hizi kapoooooaa.

Hivi nimuulize Lema na UKAWA wote, mikakati yenu ya kuchukua nchi ipo vipi.? Jipimeni kwa mikakati madhubuti, wakati mwingine hata hatuhitaji kuona posts zenu za kike kike humu. wakati nyie mnalialia, CCM wanajipanga kwa uchaguzi ujao.

Mikutano ya ndani mnafanya kwa kusuasua, mikutatano ya wabunge wenu kwenye majimbo yao husika inafanyika kwa taabu, au ndio CDM mmekata tamaa.? semeni tu.

Kama mlizoea siasa za kwenda popote wakati wowote kipindi cha Kikwete, je hiki kipindi cha JPM cha kufanya siasa sehemu fulani fulani tu, mmejipangaje kimkakati.? au ni kulia lia tu na kulalamika.?
Hivi kweli mna ndoto za kuchukua nchi kishikaji tu kama kuokota sh 200 njiani unatembea.

Vinginevyo kisiasa ndo mmeshaliwa hivyo.
 
Kipi kimekuliza? Kulia ni hulka ya mtu kuna watu wameumbwa nayo wengine hata wakifiwa na wazazi wao machozi hayatoki. Hivyo haina maana kulia kwako kumethibitisha kitu chochote. Kuna jamaa alikua anawaadhibu watoto wake wakilia na yeye hujifungia ndani kulia labda na wewe una emotions kama huyu jamaa.

Hili suala la Beb Saanane ni zito sana na hakuna sababu ya CHADEMA kulitumia kama mchezo wa kujijenga kisiasa wakati na wao pia wana hoja ya kujibu. Inakuaje Bongo flava wamevalia njuga suala la msanii mwenzao wakati CHADEMA walikaa kimya na kufanya safari za nje kana kwamba hakikutokea kitu. Katika siasa kama hizi ni aibu sana kuitumia familia ya mtu kama mtaji wa kujijenga kisiasa.

Serikali pia inatakiwa kuwa makini wakati matukio kama haya yakitokea bila hatua zozote kuchukuliwa zinatupa picha mbaya sisi wengine ambao si wanasiasa na tunataka ustawi wa maisha yetu bila kuogopa nini kitatutokea.
Upumbavu mtupu! Unalia nini mwanaume mzima?
 
Hivi kuna watu wana utimamu wa akili wanawaza UKAWA wanaweza kuwa suluhisho la uongozi mbovu wa nchi hii???
Mkuu, nikikusoma akili yako unataka kusema waliosababisha matatizo ndiyo watakaoleta suluhisho la matatizo yao...... yaani ni kama vile unasema wakishindwa wale kila mtu atashindwa tu!
 
Back
Top Bottom