Lema aanika meseji ya Ben Saanane

Lema aanika meseji ya Ben Saanane

Lema aanika meseji ya Ben Saanane
www.ippmedia.com/sw/habari/lema-aanika-meseji-ya-ben-saanane

Akichangia mjadala wa makadirio ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Lema alisema: “Kama itanyesha mvua ya radi basi itaambatana na mwanga na cheche zitazowamulika walaghai, watesaji na watetezi wa haki watapata mwanga katikati ya giza totoro la unyanyasaji.”

Mbunge huyo alisema maneno hayo ni ujumbe wa mwisho ya Ben Saanane ambaye hajui kama ni marehemu ama yupo hai.

“Lakini hata kumjadili humu haturuhusiwi. Nje mikutano ya hadhara hatufanyi. Kama kijana wa miaka 16 katika Taifa ambalo halina uhuru wa vyombo vya habari, halina chama cha siasa aliandika maneno machache tu “Assad must go, Assad will be next, leo Syria haina amani,”alisema.

“Uhuru wa habari ni altenative (mbadala) ya amani, si kikwazo cha amani. Watu wanapoongea wanatema nyongo, ‘wanarealise tension’. Leo tunapotaka kujadili mambo ya msingi, mnatumia nguvu na uwezo mlio nao, mtashinda,” alisema Lema.

Alisema kila jambo wanalotaka kulipitisha kwa wingi wao watashinda.

“Katika mchango wangu uliopita, nilisema Mungu hadhihakiwi, apandacho mtu ndicho avunacho,”alisema

Alifunguka kuwa alipokuwa gerezani, vijana waliokamatwa kwa makosa ya mtandaoni ni wengi na walikamatwa kimya kimya.

“Wanapelekwa mahakamani wanasomewa mashitaka bila ndugu zao kuwapo. Vijana wamejaa magerezani kwa sababu ya ukosoaji,” alisema na kuongeza kuwa haiwezekani kuwa na taifa lenye amani bila kuwa na uhuru wa habari.

“Msifikiri mnatunga sheria kutukomoa sisi. Mna watoto wanakua, wajukuu wanakua…Tunapopigania uhuru wa habari hatupiganii Chadema, CCM tunapigania taifa bora na huru,” alisema.

“Leo ndani ya bunge hatusemi, kwenye mitandao hawaongei, vyombo vya habari havitasema huko mitaani mikutano ya hadhara imezuiwa. Iko siku watu wataingia mitaani kudai uhuru mnaowanyima.

Alisema watu hao watakuwa hawajatumwa na Chadema wala CUF na siku hiyo kila mtu atatafuta nyumba ya kujificha.

“Unapozuia haki, unapozuia uhuru, unapozuia kweli unatengeneza balaa katika taifa hili. Tunalalamika kwa sababu familia zetu zinaishi hapa, tungekuwa na mpango wa kuondoka tungeenda kulalamikia Marekani.

“Tukisema miongozo ni mingi na sijui hata hotuba yangu itakuwaje. Kama hotuba ya Waziri wa habari na michezo mmeifanya hivi, hotuba ya waziri wa mambo ya ndani na uzoefu wa Lijualikani alipokuwa magereza na uzoefu wangu nilipokuwa magereza mtaanza kuizuia kwenye salamu.

“Wabunge mko wengi tusaidieni, mawaziri tusaidieni tukishamalizwa sisi, msumeno utakaofuata utakuwa kwenu. Ni nini mnakipigania waheshimiwa wabunge, kita kitu kinakuwa hovyo. Ni fedha?,” alihoji.

Lema alisema utu wa mtu haupimwi kwa ghorofa, cheo, bali unapimwa kwa kazi na wajibu alioufanya duniani.

“Mimi nilikamatwa nje hapo getini nikapelekwa Kondoa nikaweka ‘lock up’ (rumande) saa 4:00 hadi saa 8 usiku nikapelekwa Arusha nikatengwa chumba peke yangu, nikakaa jela nikatoka baada ya miezi minne. Mnaweza kufanya hivi leo,” alisema.

Lema aliongeza kuwa: “Mimi mkitaka kuniua niueni leo, kesho ni mbali. Mkitaka kumuua yeyote hapa muueni leo, kesho ni mbali. Haya mambo mnayotuzuia kuyasema mnafikiri tunasema tunapenda uwanaharakati.”

Alieleza kuwa ana mtoto wa kwanza ana miaka 11 na wa mwisho ana miaka minne na angependa kuona ndoa na harusi na elimu za watoto wake kwa macho yake.

“Lakini ikibidi nisione hiyo harusi kwa sababu ya kupigania ya ninachokipigania watakumbuka maisha yetu bungeni kupigania property (mali). Yalipigania haki na msingi wa taifa hili ambayo mmeishindwa,” alisema.

Alisema ni muhimu wanaokalia Kiti cha Spika wakaacha faraja, baraka na kuacha kutumia wingi wa wabunge wa CCM.

“Hapo alikaa Mzee Sitta leo ni marehemu, kila mtu atapita kwa wakati wake. Ni muhimu mkapita mkaacha faraja nyuma, baraka acheni kutumia wingi wenu vibaya. Simbachawene wewe una historia. Ulikuwa kondakta Mungu amekuweka mpaka umekuwa hapo, tulitarajia kukuona wewe unapigania nchi hii.

“Leo unaishi utafikiri umezaliwa katika familia ya Warren Bafet. Mtu akisimama kuongea ukweli unapinga.
Suala la mtu kupotea katika jamii yake ni zito sana. Ni angekuwa amefariki dunia akazikwa ingeeleweka. Akili za watu zinawaza, zinafikiri na zinatafakari hata kama hawaongei. Kila jambo lina mwisho wake kama ni jema ni mzuri lakini kama ni baya ni aibu.
 
BruceLee kama unayajua waliyokuwa wanayafanya nyamaza endelea na mambo yako.Inakusaidia nini kuchimbachimba maisha ya wenzako?
 
Ben Saanane... Tunakulilia Mkuu .... Mungu akulinde akuhifadhi popote ulipo ...
 
Mara mojamoja jaribu hata kumuomba mwamna kama yupo akupe ushauri wa nini cha kuchangia maana naona kwa akili yako haiwezekani kabisa kiwa na mawazo positive kwa taifa na ukautoa ukada nanchuki.

Maana alicho kionge lema hapo kina mgusa hata yule asiye na chama ila kilicho nigusa zaid katika maelezo yake ni pale alipo sema msifikiri mnafanya haya kutukomoa sisi mna watoto na mna wajukuu na wanakua, nadhan wana CCM wengi mna tatizo la kuto fikiria future yenu na ya taifa kwa ujumla wake. Mnawazia ya hapo hapo mlipo kwa wakati huo na si ya kesho. Kama ambavyo leo mmeanza kujutia ujinga mlio ufanya kwenye katiba ya warioba .
Hawa sifa yao ni kujua kusoma na kuandika tu, wala wasikuumize kichwa.

Si unaona hata bosi wao anajua Saddam Hussein alikuwa raisi wa Kuwait?
 
Sasa hizo meseji za Ben ziko wapi, jamani mbona povu? Hili sakata la kijana Ben inabidi wamkamate Mbowe na kumuuliza, ni yeye ndiye atakuwa anajuwa ukweli si CCM.
Kuna kipindi huwa nakaa nafikirii mtu mwenye ufahamu duni kama huu, kama anatumia computer kuandika hata kufungua account aliwezaje.
 
Lema bana, sikujua kama huyu jamaa ni slow learner wa ajabu namna hii. Tangu ameanza harakati zake kisiasa, mwanzo kwa kikwete, alikuwa angalau hata nafoka, siku hizi kapoooooaa.

Hivi nimuulize Lema na UKAWA wote, mikakati yenu ya kuchukua nchi ipo vipi.? Jipimeni kwa mikakati madhubuti, wakati mwingine hata hatuhitaji kuona posts zenu za kike kike humu. wakati nyie mnalialia, CCM wanajipanga kwa uchaguzi ujao.

Mikutano ya ndani mnafanya kwa kusuasua, mikutatano ya wabunge wenu kwenye majimbo yao husika inafanyika kwa taabu, au ndio CDM mmekata tamaa.? semeni tu.

Kama mlizoea siasa za kwenda popote wakati wowote kipindi cha Kikwete, je hiki kipindi cha JPM cha kufanya siasa sehemu fulani fulani tu, mmejipangaje kimkakati.? au ni kulia lia tu na kulalamika.?
Hivi kweli mna ndoto za kuchukua nchi kishikaji tu kama kuokota sh 200 njiani unatembea.

Vinginevyo kisiasa ndo mmeshaliwa hivyo.
Wewe maskini unaandika huu ujumbe ukiwa kwenye kachumba kako unakolipia TZS 20,000/= kwa mwezi huko Tandale na elimu yako ya darasa la saba ili uweze kwenda Lumumba kwa wale mafisi wenzako kulipwa TZS 7,000/=halafu huyo unayemsema yuko Bungeni amekuzidi elimu, uchumi, exposure na hata ufahamu.

Lema akitaka kuacha siasa ili asitukanwe na maskini wapuuzi kama wewe anaweza na bado akaendelea kuishi maisha mazuri tu ambayo wewe kama una TV ile ya mgongo huwa unaishia kuyaona tu kwenye tamthilia.

Its sad watu wema na wasio na hatia wanakufa halafu wapuuzi wa Lumumba kama wewe mnaishi!
 
Hayo ndio matatizo ya wapiga kura wa arusha mjini waliyomtuma akaongee bungeni?
Kungekuwa na uwezekano, ubongo wako ulipaswa kuzikwa kabla ya mwili maana u marehemu tayari.

Mimi sijawahi kwenda kupiga kura ili mbunge akaseme bungeni eti 'maji ya shida' ilhali inajulikana kuna matatizo makubwa zaidi ya maji...HAKI!
 
Meseji ya Ben Sananee ipo wap . . ?
Watu wengine mko Jf kwa sababu hakuna mchujo. Yaani thread yote hujaona msg ya Ben Saanane wakati imewekwa mwanzo tu halafu na wewe unataka wakuite Gt?
 
Hayo ndio matatizo ya wapiga kura wa arusha mjini waliyomtuma akaongee bungeni?
Let's be serious; Bungeni siyo mahali pa kuongelea 'parochial issues'; baraza la madiwani litafanya kazi gani? Aidha zipo njia nyingi za Mbunge kuwasilisha matatizo ya jimbo lake kwa waziri husika. Bunge ni chombo cha kutunga sheria, kusimamia serikali na kuishauri serikali kuhusu sera mbalimbali.
 
Sema ukweli japokuwa mchungu.

Big up LEMA
 
Mimi ni kada, lakini wenye masikio ya kusikia wasikie, Lema aliambia taifa kupitia bunge.
 
Kungekuwa na uwezekano, ubongo wako ulipaswa kuzikwa kabla ya mwili maana u marehemu tayari.

Mimi sijawahi kwenda kupiga kura ili mbunge akaseme bungeni eti 'maji ya shida' ilhali inajulikana kuna matatizo makubwa zaidi ya maji...HAKI!
Wala usipoteze muda na mwana Lumumba, hapo anatuliza maumivu maana kaipata ya udoni tena kwenye giza nene
 
Siku hizi Ukawa wana CD mbili tu!

Moja ya Bashite nyingine ya Ben saanane, ya Kinana kila wakijaribu kuicheza Ina scratch
Pohamba jaribu kufikiri kidogo kwa kutumia ubongo, utakuja baki huna cha kujitetea. Maana mjinga maudhui yake huandikwa kwenye mchanga!!
 
Uhovyo wake uko wapi? Maana kuna watu hamnaga akili nadhani unafiki umetawala mioyo yenu
uko kwenye kutetea tabaka la juu ilo hali ni ametoka tabaka la chini anayajua fika matatizo ya huko

ila ajakufikia uhovyo wako wa kuja kuuliza swali la hovyo ikiwa majibu ushapewa kwa maneno ya lema

ajakufikia uhovyo wako wa kutetea u hovyo wake na kujionesha ulivyo mpuuzi kushindwa kujua tabaka la chini/upinzani/wanyonge wanavyo nyanyaswa

kifupi ww ni hovyo kuliko simbachawene.
 
Lema aanika meseji ya Ben Saanane
www.ippmedia.com/sw/habari/lema-aanika-meseji-ya-ben-saanane

Akichangia mjadala wa makadirio ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Lema alisema: “Kama itanyesha mvua ya radi basi itaambatana na mwanga na cheche zitazowamulika walaghai, watesaji na watetezi wa haki watapata mwanga katikati ya giza totoro la unyanyasaji.”

Mbunge huyo alisema maneno hayo ni ujumbe wa mwisho ya Ben Saanane ambaye hajui kama ni marehemu ama yupo hai.

“Lakini hata kumjadili humu haturuhusiwi. Nje mikutano ya hadhara hatufanyi. Kama kijana wa miaka 16 katika Taifa ambalo halina uhuru wa vyombo vya habari, halina chama cha siasa aliandika maneno machache tu “Assad must go, Assad will be next, leo Syria haina amani,”alisema.

“Uhuru wa habari ni altenative (mbadala) ya amani, si kikwazo cha amani. Watu wanapoongea wanatema nyongo, ‘wanarealise tension’. Leo tunapotaka kujadili mambo ya msingi, mnatumia nguvu na uwezo mlio nao, mtashinda,” alisema Lema.

Alisema kila jambo wanalotaka kulipitisha kwa wingi wao watashinda.

“Katika mchango wangu uliopita, nilisema Mungu hadhihakiwi, apandacho mtu ndicho avunacho,”alisema

Alifunguka kuwa alipokuwa gerezani, vijana waliokamatwa kwa makosa ya mtandaoni ni wengi na walikamatwa kimya kimya.

“Wanapelekwa mahakamani wanasomewa mashitaka bila ndugu zao kuwapo. Vijana wamejaa magerezani kwa sababu ya ukosoaji,” alisema na kuongeza kuwa haiwezekani kuwa na taifa lenye amani bila kuwa na uhuru wa habari.

“Msifikiri mnatunga sheria kutukomoa sisi. Mna watoto wanakua, wajukuu wanakua…Tunapopigania uhuru wa habari hatupiganii Chadema, CCM tunapigania taifa bora na huru,” alisema.

“Leo ndani ya bunge hatusemi, kwenye mitandao hawaongei, vyombo vya habari havitasema huko mitaani mikutano ya hadhara imezuiwa. Iko siku watu wataingia mitaani kudai uhuru mnaowanyima.

Alisema watu hao watakuwa hawajatumwa na Chadema wala CUF na siku hiyo kila mtu atatafuta nyumba ya kujificha.

“Unapozuia haki, unapozuia uhuru, unapozuia kweli unatengeneza balaa katika taifa hili. Tunalalamika kwa sababu familia zetu zinaishi hapa, tungekuwa na mpango wa kuondoka tungeenda kulalamikia Marekani.

“Tukisema miongozo ni mingi na sijui hata hotuba yangu itakuwaje. Kama hotuba ya Waziri wa habari na michezo mmeifanya hivi, hotuba ya waziri wa mambo ya ndani na uzoefu wa Lijualikani alipokuwa magereza na uzoefu wangu nilipokuwa magereza mtaanza kuizuia kwenye salamu.

“Wabunge mko wengi tusaidieni, mawaziri tusaidieni tukishamalizwa sisi, msumeno utakaofuata utakuwa kwenu. Ni nini mnakipigania waheshimiwa wabunge, kita kitu kinakuwa hovyo. Ni fedha?,” alihoji.

Lema alisema utu wa mtu haupimwi kwa ghorofa, cheo, bali unapimwa kwa kazi na wajibu alioufanya duniani.

“Mimi nilikamatwa nje hapo getini nikapelekwa Kondoa nikaweka ‘lock up’ (rumande) saa 4:00 hadi saa 8 usiku nikapelekwa Arusha nikatengwa chumba peke yangu, nikakaa jela nikatoka baada ya miezi minne. Mnaweza kufanya hivi leo,” alisema.

Lema aliongeza kuwa: “Mimi mkitaka kuniua niueni leo, kesho ni mbali. Mkitaka kumuua yeyote hapa muueni leo, kesho ni mbali. Haya mambo mnayotuzuia kuyasema mnafikiri tunasema tunapenda uwanaharakati.”

Alieleza kuwa ana mtoto wa kwanza ana miaka 11 na wa mwisho ana miaka minne na angependa kuona ndoa na harusi na elimu za watoto wake kwa macho yake.

“Lakini ikibidi nisione hiyo harusi kwa sababu ya kupigania ya ninachokipigania watakumbuka maisha yetu bungeni kupigania property (mali). Yalipigania haki na msingi wa taifa hili ambayo mmeishindwa,” alisema.

Alisema ni muhimu wanaokalia Kiti cha Spika wakaacha faraja, baraka na kuacha kutumia wingi wa wabunge wa CCM.

“Hapo alikaa Mzee Sitta leo ni marehemu, kila mtu atapita kwa wakati wake. Ni muhimu mkapita mkaacha faraja nyuma, baraka acheni kutumia wingi wenu vibaya. Simbachawene wewe una historia. Ulikuwa kondakta Mungu amekuweka mpaka umekuwa hapo, tulitarajia kukuona wewe unapigania nchi hii.

“Leo unaishi utafikiri umezaliwa katika familia ya Warren Bafet. Mtu akisimama kuongea ukweli unapinga.
Uyu Yanga chawene kazi yake kupinga miongozo kla mbunge wa upinzani akisimama ivi ana jimbo uyu
 
Back
Top Bottom