Lazio; Minala ana miaka 17 sio 42

Lazio; Minala ana miaka 17 sio 42

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Posts
22,475
Reaction score
21,046
140530053017_lazio_minala_ana_miaka_17_sio_42__512x288_bbc_nocredit.jpg


Uchunguzi wa shirikisho la soka la Italia umebaini kuwa mchezaji tineja wa Cameroun Joseph Minala ana umri wa miaka 17 wala sio 42 kama ilivyodhaniwa na kuripotiwa katika vyombo vya habari.

Mnamo mwezi Februari mtandao mmoja wa michezo barani Afrika ulichapisha habari ambayo ilizua dukuduku iwapo kiungo huyo alikuwa amedanganya umri wake .

Mtandao huo ulichapisha habari za kuashiria kuwa hakuwa tineja bali mtu mwenye umri wa miaka 42.
140529145738_joseph_minala_512x288_getty.jpg


Uchunguzi uliofwatia ulimlazimu kukatiza kwa muda mipango yake ya kucheza soka ya kulipwa hadi pale matokeo ya uchunguzi yangewekwa wazi na maafisa wa shirikisho la soka la Italia.

Minala alijiunga na klabu hiyo yenye makao yake mjini Rome na hata alishiriki mchuano wa vijana wasiozidi umri wa miaka 23 wa Viareggio mnamo mwezi wa Februari.

source: BBC Swahili - Habari
 
da kweli jamaa anasura ya kiutu uzima kabisaaaaaaaaaaaaaa
 
Asee !!!

Akili inakubali lakini macho yanakataa..

Duuh!!!.. 17??
 
pole sana mkuu minala, naona maumbile yako yanataka kukunyima haki yako ya msingi
 
140530053017_lazio_minala_ana_miaka_17_sio_42__512x288_bbc_nocredit.jpg


Uchunguzi wa shirikisho la soka la Italia umebaini kuwa mchezaji tineja wa Cameroun Joseph Minala ana umri wa miaka 17 wala sio 42 kama ilivyodhaniwa na kuripotiwa katika vyombo vya habari.

Mnamo mwezi Februari mtandao mmoja wa michezo barani Afrika ulichapisha habari ambayo ilizua dukuduku iwapo kiungo huyo alikuwa amedanganya umri wake .

Mtandao huo ulichapisha habari za kuashiria kuwa hakuwa tineja bali mtu mwenye umri wa miaka 42.
140529145738_joseph_minala_512x288_getty.jpg


Uchunguzi uliofwatia ulimlazimu kukatiza kwa muda mipango yake ya kucheza soka ya kulipwa hadi pale matokeo ya uchunguzi yangewekwa wazi na maafisa wa shirikisho la soka la Italia.

Minala alijiunga na klabu hiyo yenye makao yake mjini Rome na hata alishiriki mchuano wa vijana wasiozidi umri wa miaka 23 wa Viareggio mnamo mwezi wa Februari.

source: BBC Swahili - Habari

Da jamaa anaonekana aliugua sana DENGUE utotoni
 

UTATA WA UMRI WAMALIZIKA
Uchunguzi wa chama cha soka la Italia FIGC umebaini kuwa kiungo wa Lazio Joseph Minala umri wake ni miaka 17 na sio miaka 42.
Tovuti mmoja ya Afrika mwezi Februari ilisema Minala ambaye ni mzaliwa na Cameroon, ana miaka 42 na sio 17.
Tuhuma hizo zilisababisha uchunguzi rasmi uliosababisha mchezaji huyo kuhojiwa.
"Uchunguzi haujaonesha haja yoyote ya kuchukua hatua za kinidhamu" imesema taarifa ya FIGC.
Minala alijiunga na klabu hiyo ya Rome mwaka jana na kucheza katika michuano ya Viareggio ya vijana mwezi Februari.





· ·
10430443_439924489478352_2856954834507737951_n.jpg
​
 
Mmmh! 17? sura imekomaa hivyo nina wasiwasi na hao wachunguzi
 
Ukiangalia sura utakata hata hawa lukaku (1993) Luke shaw (1995) chamberlain (1993)
 
Back
Top Bottom