Lazaro Nyalandu akamatwa na kushikiliwa na TAKUKURU mkoani Singida

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Watu wasiojulikana,wakiwa na silaha wamevamia kikao cha CHADEMA kata ya Itaja jimbo la Singida Kaskazini na kuondoka na Mhe. Lazaro Nyalandu , M/kiti wa Kata ya Itaja na aliyekuwa mgombea ubunge wa CHADEMA jimbo la Singida Kaskazini, David Jumbe mpaka sasa hatujui wamepelekwa wapi.
-----

UPDATES
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU)imemkamata aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu kwa mahojiano.

Kamanda Polisi mkoani Singida Sweetbert Njewike amethibitisha

Mkuu wa TAKUKURU Singida, Joshua Msuya amesema walipata taarifa za uwepo wa viashiria vya rushwa kwenye mikutano ya moja ya Vyama vya Siasa mkoani humo baada ya kufuatilia ndipo walimkuta Lazaro Nyalandu akiwa katika nyumba moja ambayo si ofisi ya CHADEMA akiendesha kikao.

Lazaro Nyalandu na wenzake, baada ya kupelekwa polisi na TAKUKURU, Jeshi la polisi wamewanyima dhamana na wanatuhumiwa kwa kusanyiko lisilokuwa halali, ambalo linaweza kupelekea vitendo vya rushwa. Walishasaini dhamana mbele ya wakili wao ila ikapokelewa simu na dhamana ikafutwa.

zaidi...

Nyalandu akamatwa na Takukuru


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike, alilithibitishia Nipashe jana kuwa Nyalandu alikamatwa na Takukuru mkoani humo.

Hata hivyo, kamanda huyo alisema hajafahamu sababu za kukamatwa Nyalandu kwa kuwa taasisi iiyomkamata inajitegemea na ndiyo yenye uwezo wa kueleza sababu.

“Ni kweli Nyalandu amekamatwa, lakini hajakamatwa na polisi bali Takukuru, ni vizuri ukawapigia ili wakueleze sababu za kumkamata ni zipi,” alisema.

Nyalandu ambaye kwa sasa ni kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alikamatwa jana wakati akiwa kwenye kikao cha Chadema, Kata ya Itaja, Jimbo la Singida Kaskazini kilichofanyika mkoani Singida.

Ofisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani alipopigiwa simu kuthibitisha kukamatwa na Taasisi hiyo, alikiri na kusema uchunguzi unaendelea bila kufafanua uchunguzi gani.

Katibu Mkuu wa Chadema, Vincent Mashinji, alipoulizwa kuhusu tukio la kukamatwa kwa Nyalandu, alisema mpaka jioni alikuwa anashikiliwa na Takukuru na alikuwa hajaambiwa sababu za kukamatwa kwake.

Nyalandu (49) aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2000 akiwakilisha Jimbo la Singida Kaskazini kwa tiketi ya CCM na mwaka 2005 na 2010 alichaguliwa tena kwenye jimbo hilo.

Novemba mwaka 2010, Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete alimteua Nyalandu kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara hadi Mei 2011, alipohamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii alikokaa kwa miaka mitatu.

Januari mwaka 2014 nyota ya Nyalandu iliendelea kupaa kwa kuteuliwa na Rais Kikwete kuwa Waziri kamili wa Maliasili na Utalii nafasi aliyoitumikia hadi Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Baada ya kutangaza kuwania urais Desemba 28 mwaka 2014 na kushindwa kwenye hatua za awali, Nyalandu aliamua kuwania ubunge kwenye jimbo lake na alichaguliwa kwa kipindi cha nne ingawa mwaka 2017 aliamua kuachana na CCM na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Oktoba 30, Nyalandu alitangaza kujiuzulu nyadhifa zake zote ndani ya CCM ikiwamo ubunge akilalamikia baadhi ya mambo ambayo aliona hayaendi sawa ikiwamo suala la Katiba mpya.

Nyalandu alisema amechukua uamuzi huo kutokana na kutokuridhishwa na mwenendo wa siasa nchini Tanzania, ukiukwaji wa haki za kibinadamu, ongezeko la vitendo vya kidhalimu dhidi ya raia na kutokuwapo kwa mipaka baina ya mihimili ya dola.

 

Attachments

  • IMG-20190527-WA0041.jpg
    IMG-20190527-WA0041.jpg
    66.5 KB · Views: 105
Breaking News

Watu wasiojulikana,wakiwa na silaha wamevamia kikao cha Chadema kata ya Itaja jimbo la Singida Kaskazin na kuondoka na Mhe. Lazaro Nyalandu , Mkiti wa Kata ya Itaja na aliyekuwa mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Singida Kaskazin David Jumbe mpaka sasa hatujui wampelekwa wapi
Bokoharam wameshafanya yao.
IMG_20190525_132941_962.jpeg
 
Breaking News

Watu wasiojulikana,wakiwa na silaha wamevamia kikao cha Chadema kata ya Itaja jimbo la Singida Kaskazin na kuondoka na Mhe. Lazaro Nyalandu , Mkiti wa Kata ya Itaja na aliyekuwa mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Singida Kaskazin David Jumbe mpaka sasa hatujui wampelekwa wapi
Bila shaka ni policcm, aka watu wasiojulikana
 
Hivi hawa watu wasiojulikana serikali imeshindwa kuwajua kweli?

Wasiojulikana wanawavamia wapinzani, wanawateka na kuwaua lkn wanabaki wasiojulikana ila akiguswa kada au kiongozi na wasiojulikana huwa wanajulikana mapema sana.

Serikali inajinasuaje na tuhuma za kuwatumia wasiojulikana kuwazima wapinzani wa ukweli?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom