Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,741
- 218,330
Lazaro Nyalandu, Mwanaccm wa kwanza kujivua Ubunge kwa sababu ya kupinga Udikteta wa Magufuli wa kuteka, kutesa na kushambulia watu kwa risasi, ambaye baadaye alikimbilia CHADEMA na kupokelewa kwa heshima na hatimaye kupewa Cheo kikubwa cha kuongoza Kanda ya kati, miezi kadhaa baada ya kurudi tena CCM ili kubahatisha cheo bila mafanikio amefunguka kuhusu wema wa CHADEMA.
Nyalandu amenukuliwa akisema kwamba "Wanachama wa CHADEMA wanakisapoti sana chama chao na wana upendo mkubwa sana miongoni mwao". Ameendelea kufunguka kwamba jambo hili halimo ndani ya CCM ( Haifahamiki amekumbwa na nini )
Bali ikumbukwe kwamba hata Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliwahi kunukuliwa kwenye vikao vya Chama chake kwamba , "WANACCM HAWAACHIANI MAJI YA KUNYWA MEZANI " kwamba kama ukiacha maji yako kwenye kadamnasi ya chama hicho unaweza kuwekewa kitu kizito ndani yake, Ushahidi wa kuachiana maji mezani anao Phillipo Mangula.
Tutafakari sana Ujumbe huu wa Nyalandu.