LAWAMA KWA wana-CCM tu?

Mkuu Exaud, kila Kundi lina wajibu wake, Wajibu wa CCM siyo sawa na wajibu wa vyama vya Upinzani ( kwa mfano). Kila kundi linatakiwa kutimiza wajibu wake kikatiba, sasa huwezi huwezi kuwalaumu wapinzani kwa sababu serikali ni corrupt, utaweza kuwalaumu tu kama hawatimizi wajibu wao ambao ni Watch dogs, sasa kazi ya Chama tawala ni kusimamia na kuhakikisha wananchi waliokiweka madarakani wanastahili kufurahia raslimali ambazo mungu amejalia, kwa hiyo unaona kwamba being on rulling side unakuwa na majukumu mengi zaidi and so as lawama.
 
Mimi ninavyo ona bora ikiwa serikali imeshindwa kununua bidhaa za wananchi/wakulima bora iwaachilie wakauze wenyewe wanopo ona kuna bei nzuri.
Niliwahi kupata fursa ya kutembea kwa kibiashara nchi kama Dubai, Thailand, singapore na Honk kong, ama kwa hakika bei nilioiona huko ya Karafuu, Kahawa na Chai sikuamini kua nyumbani sisi ni maskini. Kwa mfano Dubai kili moja ya Karafuu ni Dhs. 32 Equiv. to $9 wakati nenda kaulize Pemba mkulima na muuzaji wa karafuu kwa SMZ analipwa kiasi gani? It's shame hata kutaja mbali kua hapati malipo yake hapo hapo. Mkarafuu huo huo uliolimwa na babu yake kwenye shamba lao hana ruhusa kuuza hata hapo Dar, Tanga au Kenya.

Hayo ndiyo chanzo cha umasikini wanaotiwa wananchi na ndipo ukasema uzuri wa CCM hauonikani? Vipi utaona mazuri wakati basic and neccesity things can not be afforded?
Believe me hakuna watu wastaarabu na wepesi kuwatawala kama wa TZ this does not mean kua wajinga, No ni kwa sababu they don't care much about wasting time in these bloody stupid politics, but when it reach time waka realize kua wanapotezwa direction hapo ndio pabaya. Iwapo CCM wanataka waonekane wazuri, kwaza waondoshe Immunity au Protection kila mmoja awe ajibike kwa makosa alioyofanya la si hivyo itakua kama sasa raisi ajae lazima amprotect wa zamani. Bana Hawa wana Dhambi nyingi tu.
 
kwani viongozi wa chama gani kingine wamewahi kuwa madarakani wakaboronga au wakafanya mema ili tuwapime? mpaka sasa nchi hii imewahi kutawaliwa na waheshimiwa wa ccm pekee na ndio tunaofahamu madudu waliyoyafanya na sina haja kuyaorodhesha hapa.
waswahili wanasema mwizi na hindi lake na hadi sasa mwizi tunayemwona na mahindi yetu yaliyoibiwa ni mwanaccm pekee. chadema, tlp au cuf alitawala lini hata tuone alivyokwiba au alivyofanya ubadhirifu?
lovulovu

Lovulovu!

Nakushukuru kwa kuwa umewapa mwanga akina Nziku na Exaud!
CCM imekuwa madarakani kwa miaka 48 ilikuwa TAA ikabadili jina na kuzaliwa TANU ambayo nayo kwa kuhofia ukewenza ikaimeza Afro Shiraz Party na akazaliwa huyu mdudu anayeitwa CCM. Shehe ni yule yule ila amekuwa akibadili kanzu tu!!! yeS. Kuna wakati wote tulilazimishwa kuwa wana-ccm lakini ilipofika 1992 wengi tulibwaga manyanga!!! Tulitumia ccm kama choo tu ili tuweze kwenda Chuo Kikuu!!!

Kwa miaka yote hiyo CCM wamekuwa wakiimba wimbo wa umasikini,ujinga, maradhi, siasa safi na uongozi bora bila ya mafanikio ya kujivunia sana kwa hiyo basi lawama ni stahili yao mpaka waende mbele ya haki kama chama au mmojammoja period!!

Kwa vile waTZ wana laana pamoja na kumbukumbu hafifu sana bado wanaendelea kuwasikiliza hawa wapuuzi na wezi wakubwa!!!

Kuna wakati Mzanaki mmoja alituimbia wimbo wa siasa ni klilimo ukaisha ladha akiwa na Mmakonde mmoja anayeitwa Kawawa!! Badaae akaja na wimbo wa kilimo cha kufa na kupona kila mtu akalima mapaka kwenye miteremko ya milima ya Uluguru na mpaka maua KWENYE flower beds za shule yalikatwa wanafunzi na waalimu wakapanda mahindi matokeo yake Dar kukawa na mbu mpaka akaja Mjapani akaanza kupuliza dawa mitaani bila mitaro ya maji machafu kujengwa!! Hadi leo sijaona tija yake!
Leo hii baada ya miaka thelathini amekuja Mkwere(JMK) aka Matonya akiwa na yule TYSON wa Musoma aliyekwenda kuua upinzani amekuja na maajabu ya KILIMO KWANZA!! Kwa kweli CCM kwa kutuona mabwege hawajambo!!! Kikwete anajiunga na akina Bush kugawa chandarua kila kaya mbili wakati nyumba moja wanaishi watu 20 this is crazy!!!

Yule Mkapa aliyejiuzia Kiwira aliuza mpaka mashamba y mengi pamoja na Mbarali na KAPINGA kwa waarabu hivi lini mwarabu kawa mkulima!!!! Kama CCM sio wehu hiyo kilimo kwanza itaanzia wapi!!! Mtibwa ya sukari anayo Mkapa kwanini wasimnyanganye kwanza!!!

Kwa hiyo Exaud na wenzako hata mfanye nini CCM haikwepi lawama na haisafishiki hata kwa kupiga rangi iache itajifia yenyewe kama WaTZ hawajataka kuiadabisha!!!! Huwezi kuwalaumu akina Zitto na Lipumba hawa jamaa si nao mabwege tu wanaganga njaa ya ruzuku they are all birds of the same colour !!


 
;;;;;;;;;;;;;;;

Kwa hiyo Exaud na wenzako hata mfanye nini CCM haikwepi lawama na haisafishiki hata kwa kupiga rangi iache itajifia yenyewe kama WaTZ hawajataka kuiadabisha!!!! Huwezi kuwalaumu akina Zitto na Lipumba hawa jamaa si nao mabwege tu wanaganga njaa ya ruzuku they are all birds of the same colour !!

MKEREME,
Mimi sipendekezi CCM ikwepeshwe lawama.
Lakini ni wao tu?
Asante kwa hoja matata.
 
wa kulaumiwa ni sisiem chama kimeongoza dola for more than forty years na kuifisadi nji hii bila huruma kwa nini tusiwalaumu ni mema yapi wamefanya ? watoto wetu wanakufa hakuna dawa na madaktari wao viongozi wa chama wanatibiwa ulaya.
 
Mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa kwa sasa.

Nimefuatilia sana lawama zinazotolewa kwa viongozi mbali mbali wa nchi yetu Tanzania.

Kinachonipa wasi wasi ni kuona kuwa lawama hizo zinaelekezwa tu kwa wale viongozi ambao ni wana CCM.

Najiuliza haya:-
1. Ni kweli kwamba hakuna la maana wanalilifanya viongozi wana- ccm?
2. Je viongozi, Wabunge, nk. wa Itikadi nyingine za siasa hwana lawama?
Wako safi tu?
3. Viongozi wa taifa letu hawana lolote la kusifiwa?
Mbona lawama ndo nyingi zaidi? Na ni kwa wana- CCM tu?

Mimi nashauri mema yasemwe na mabaya pia .
Yasemwe hayo mema na mabaya bila kujali itikadi ya siasa ya mhusika.

Kwanza eleza lawama hizo ni zipi?.

Mimi ninachojua kuwa CCM ni chama tawala, yaani wao sera zao ndiyo zinanafasi ya kutekelezwa kwa mandate waliyoipata katika uchaguzi (sijui kama ulikuwa halali au la).

Sasa kama wewe umepewa dhamana ya kuboresha hali za maisha ya wananchi kwa kuwa na rungu la mwisho la kuamua nini kifanyike kwa wakati gani na madhumuni gani halafu ukaboronga unatarajiwe alaumiwe nani?.

Mazuri uliyoyafanya ni sehemu ya wajibu wako ulioumba mwenyewe bila kulazimishwa na mtu. Hivyo huhitaji kuomba kusifiwa na mtu ila waliokupa dhamana ndiyo watapima kama unawafaa au vipi ili wakupatie mandate nyingine. Sasa kama unalazimisha watu "kinyesi wakiite choo" kwa kuwa tu kuna tafisida katika neno choo basi unakuwa unakosea kabisa.

Huwezi kulazimisha wananchi walaumu vyama vingine wakati hata nafasi ya kuvipima kama CCM havijaipata. Hebu 2010 CCM itoke madarakani kishike chama kingine uone kama CCM italaumiwa, tena huenda wakati huo watu wataikumbuka CCM au kuisahau kabisa kutokana na utendaji wa Chama tawala wakati huo.

Huu utamaduni wa CCM wa kung'ang'ania madaraka kwa vyovyote ndiyo unawafanya watu wakilaumu kwa kuwa wanaona kuwa baadhi ya maeneo kimeshindwa wajibu wake. Baba hahitaji credit kwa kulisha familia yake ila anapata lawama pale anaposhindwa kuihudumia familia hata kwa siku moja tu, sasa huwezi sema mbona familia ya jirani hailaumiwi wakati baba wa familia ile anawalisha kila siku ugali dagaa, mi nawapa wali nyama ila nimeshindwa leo tu mnanilaumu. haiingii akilini!
 
Mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa kwa sasa.

Sidhani kama unasema kweli - yawezekana si mwananachma kwa maana ya kuwa na kadi lakini kwa post zako ni wazi u mpenzi wa CCM. Unaumia unapoona chama chako kipenzi kinapata lawama lakini hujiulizi kwa nini lawama hizo zisiwe halali yao. CCM imepewa dhamana ya kulinda na kusimamia maslahi ya taifa, sasa hayo maslahi yanapohujumiwa Exaud J. Makyao unataka tumtafute mchawi nje ya CCM, kwa nini ?

Viongozi wa taifa letu hawana lolote la kusifiwa?

Taifa limepiga kambi kwenye bonde la kashfa na umasikini na CCM kikaomba ridhaa ya wananchi kulikwamua taifa na wakapewa. Miaka karibu hamsini baadaye bado tumejaa tele humo humo na hakuna dalili ya kuhama. Wakati hao waliopewa dhamana wanakula mabilioni kulinda nyadhifa zao, masikini Watanzanaia wanazidi kudidimia, Exaud J. Makyao hilo halioni - anauliza kwa nini CCM inalaumiwa !

Mbona lawama ndo nyingi zaidi? Na ni kwa wana- CCM tu?

Raisi na makamu wake ni CCM, Mawaziri wote wa jamhuri ni CCM, Wakuu wa mikoa wote ni CCM, Wakuu wa wilaya zote ni CCM, Wakuu wa idara na taasisi zote nyeti za serikali ni CCM, Wawakilishi wa wananchi kwenye baraza la taifa (Bunge) zaidi ya asilimia 80% yao ni CCM - sasa ndugu yangu Exaud J. Makyao unataka tumlaumu nani ?

Mimi nashauri mema yasemwe na mabaya pia .

Unachanganya mambo hapa, tunayolilia ni wao kutimiza wajibu, ndivyo inavyotakiwa na hapa hawana haki kudai sifa kwa kuwa wanatimiza wajibu. Kwa kuwa wanakusanya kodi kama watajenga barabara huo ni wajibu - ndio maana waliomba kura. Kufanya hivyo si hatimiliki ya CCM kuhusu utawala bora - good has never been enough where better is possible. Lakini wakiboronga kama wanavyoendelea kufanya je, Exaud J. Makyao unatwambia tusiwalaumu kweli ?

Yasemwe hayo mema na mabaya bila kujali itikadi ya siasa ya mhusika.

Bahati mbaya ni kuwa ni itikadi moja tu ndiyo imekuwa madarakani na kila siku wanajizatiti kunga'ng'ania madarakani. Wamefunga milango yote ya kuingiza hewa safi na wako tayari sote tufie humo humo kwenye uozo. Exaud J. Makyao yawezekana hii hewa chafu imekuathiri kiasi cha kushindwa kutambua kuwa huko nje ya CCM kuna hewa safi. Balaa ilioje kuwa watu wa aina yako mko wengi na itachukua zaidi ya mapinduzi kuwazindua usingizini.

Ustaarabu unatwambia kwamba kama wajibu unakushinda, kubali ukae pembeni, mwachie mwingine ajaribu. Lakini hivi sasa tunashuhudia CCM isivyokuwa tayari kupisha wengine na wanatumia hadi nguvu isiyo ya kawaida kung'ang'ania huku uwezo hawana. Exaud J. Makyao, haya huyaoni ? Matokeo yake kila kukicha wanazidi kuharibu huku ustaarabu wa kuwajibika hawana. Kalaghabaho !
 
Viongozi waliopo madarakani ni taswira ya wananchi waliowachagua.

Sio lazima kwa sababu:
1)inawezekana viongozi 'wamejichagua' wenyewe na wakawatumia wananchi kama mhuri fulani hivi.
2) inawezekana wananchi waliingizwa mkenge wakati wa kampeni wakadanganywa na wapiga debe kwamba basi inayoenda Dodoma ni X kumbe basi lenyewe linaelekea Ntwara. Sasa kila wakiangalia wanaona hawafiki Mtwara, na haielekei kabisa kama njia inaelekea Mtwara. Madamu wananchi walikosea kupanda basi, utatuzi ni kwamba lazima wafike mahala washuke kwenye hilo basi wachukue lingine linaelekea wanapokwenda.

Kwa hiyo mkuu sio lazima viongozi wetu wawe wanafanana na wananchi; inawezekana kabisa hawa ndugu ni 'species' ingine kabisa na wale wanaowaongoza!
 
Kwa hiyo mkuu sio lazima viongozi wetu wawe wanafanana na wananchi; inawezekana kabisa hawa ndugu ni 'species' ingine kabisa na wale wanaowaongoza!

Kitila bana..eti inawezekana viongozi wetu ni species nyingine lol..

Halafu bao uko Ntwara ukila samaki nchanga au usharudi? Manake wewe nawe bana...kwanza bado una unfinished business kuhusu yule shori wa Kinyiramba...kwikwikwikwiiii
 
..........................
Ustaarabu unatwambia kwamba kama wajibu unakushinda, kubali ukae pembeni, mwachie mwingine ajaribu. Lakini hivi sasa tunashuhudia CCM isivyokuwa tayari kupisha wengine na wanatumia hadi nguvu isiyo ya kawaida kung'ang'ania huku uwezo hawana. Exaud J. Makyao, haya huyaoni ? Matokeo yake kila kukicha wanazidi kuharibu ..........!

Mag3,
Hongera kwa presentation yako nzuri na ya kiufundi japo ni changamoto.
Ukweli ni kwamba mimi si mwanachama wa chama chochote na wala sikitetei CCM.
Lengo langu kutoa mada hii ni
1. kuamsha ari ya watu ili wasielemee kuitazama ccm tu halafu tukasahau kuwa nje ya CCM kuna binadamu wengine pia.
Na huko nje ya CCM kuna hewa nyingine kama ulivyosema.
2. Kuwashtua wale walioko nje ya CCM ili wasije wakajisahau na kujihesabu wasafi kisha wakaacho kujitakasa.

Tena nasema asante tena kwa mawazo yakinifu.bwana MAG3.
 
Mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa kwa sasa.

Nimefuatilia sana lawama zinazotolewa kwa viongozi mbali mbali wa nchi yetu Tanzania.

Kinachonipa wasi wasi ni kuona kuwa lawama hizo zinaelekezwa tu kwa wale viongozi ambao ni wana CCM.

Najiuliza haya:-
1. Ni kweli kwamba hakuna la maana wanalilifanya viongozi wana- ccm?
2. Je viongozi, Wabunge, nk. wa Itikadi nyingine za siasa hwana lawama?
Wako safi tu?
3. Viongozi wa taifa letu hawana lolote la kusifiwa?
Mbona lawama ndo nyingi zaidi? Na ni kwa wana- CCM tu?

Mimi nashauri mema yasemwe na mabaya pia .
Yasemwe hayo mema na mabaya bila kujali itikadi ya siasa ya mhusika.

Unataka vyama vingine vilaumiwa kwa namna gani na mkataba gani?

ni nani anaesimamia na kuendesha uchumi wetu(ccm)

ni nani anaepanga bajeti yetu (ccm)

ni nani anaesimamia maendeleo yetu (ccm)

kwa kifupi serikali ina responsibillity zote za tanzania na watu wake, CCM ndio head na controller of every responsibility ya tanzania sasa umlaumu chadema sijui na kwa barabara mbovu nadahani unataka kuitwa mkichaa kwani wao ndio wapanga mikakati ya tanzania, ebu acha vituko Mh., alafu una chama???????
 
Unataka vyama vingine vilaumiwa kwa namna gani na mkataba gani?

ni nani anaesimamia na kuendesha uchumi wetu(ccm)

ni nani anaepanga bajeti yetu (ccm)

ni nani anaesimamia maendeleo yetu (ccm)

kwa kifupi serikali ina responsibillity zote za tanzania na watu wake, CCM ndio head na controller of every responsibility ya tanzania sasa umlaumu chadema sijui na kwa barabara mbovu nadahani unataka kuitwa mkichaa kwani wao ndio wapanga mikakati ya tanzania, ebu acha vituko Mh., alafu una chama???????

Kwani upinzani si uko bungeni?
Bajeti hupitishwa na CCM tu?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom