Last night at KFC mikocheni

Last night at KFC mikocheni

Salaam waungwana vipi ma saga ya serikali mnayaelewa!! ? Hahaha msivunjike mioyo ishu ni kufocus kwenye mambo yetu muhimu

Well Jana usiku nilitoka kumeet na one of my family friend alipatwa na matatizo sasa wakat narudi kwangu Mke Wangu akashauri tupitie KFC pale mikocheni ili tupate dinner ndio turudi sikumpinga nilipofika nikaingia kushoto tukaenda kula pale

Wakati tuko pale nakula chakula sababu Mimi nilikaa yeye akaenda kutoa order alivyo rudi ndio akawa ananiambia kuna mdada yuko pale ananiuliza kua yule mkaka ni Mume wako wife akashangaa akamwambia ndio vipi unamfahamu? yule binti akamwambia nahisi namfananisha.

Sasa kumbe Mke Wangu hakutaka mengi akamwambia njoo unaweza kuja kumsalimia kama unfahamu basi yule binti akaja pale.

At first nikawa namkumbuka ila sio kivile akaja yuko ulisoma mlimani UDBS? nikamwambia ndio akanikumbusha tukakumbukana tukawa tunacheka nikamwambia karibu tukae hapa Niko nimekuja Mara moja tuu huyu ni Mke Wangu akaniambia nimehisi hata hivyo hongera kwa Mke mzuri huku akamwambia Mke Wangu hongera kwa mume mzuri basi tukawa tunaongea tunakumbushana miaka hiyo huyu yuko wapi yule nani yah it was funny

Sasa wakati tunaendelea kula baada ya dakika kama kumi akaingia jamaa amemshika binti was kidar es salaam kuanzia mavazi mpaka muonekano wale mabinti mimi huwa nawaitaga mapython yani wezi wa wame za watu nikiwa nastaajabu huku naangalia hee yule binti tuliye kuwa nae akawa haelewi anajisemesha nimemkosea nini Mungu!? Mke wangu akamuuliza vipi uko sawa kama amejawa na hasira ghafla nikawa namuita vipi unatatzo lolote?

Yuko yule ni Mme Wangu mi na Mke Wangu tukawa tunaangaliana tunashangaa sabu ilikua kama filamu nikataka kumuuliza sasa unafanyaje akanyanyuka anataka kuwafata walipokaa nikamwambia ngoja hiyo sio njia sahihi kua muungwana uobserve angalia what is he into wanaweza kua marafiki japo walivyoingia wameshikana ilikua ni wazi wapenzi lengo langu ilikua kumpunguza jazba japo sikufanikiwa.

Alisogea mpaka pale akwamwagia vitu sasa cha ajabu yule Python yaani mchepuko akawa anaongea maneno ya kishenzi kwa mwenye Mme wake mpka nikajisikia vibaya yule binti akawa anasema sitaki maneno mengi tuachane niache na maisha yangu ata kama sijajaaliwa mtoto na wewe lakini not to this extent umenikosea sana we mwanaume .

Ikabidi nimzuie nimtoe nje nikamwambia Mke Wangu kaa nae kurudi ndani nakuta lijamaa limebaki linagombezwa na mchepuko nikajisikia vibya nikamfata yule binti nikamwambia hapa ni sehemu ya biashara after all yule ni mke wake jaribu kustaarabika huku nikimuonesha ishara ya kucalm japo hakuelewa kabisa nikamgeukia jamaa namwambia kaka mambo kama haya yanapotokea tunakua upande wa wake zetu sio hawa wakuokoteza hata hivyo pole na samahani sijui what is in yo marriage lakini nashauri mfate Mke wako muzungumze

Yule binti nikaona ametoka anaondoka jamaa nae akatoka anamuita yule binti aliekua amekaribia getini akampakia wakaondoka, yani sikuelewa sasa yule rafiki angu akawa Analia kwa uchungu mpaka unaona hii sio kawaida ameumia saaana nikamwambia twende tukupeleke nyumbani kama haukuja na usafiri akasema hataki tena kulala home anaitaji kuwa in a hotel apumzike mi nilipinga wazo lake nikasema nenda nyumbani piga simu ukweni eleza kilichotokea

Mke Wangu akajitahidi kumbembeleza sana akawa sasa at list namuona yuko kimya lakini Kwi Kwi haziish tukamsindikiza mpaka kwake tukamtia moyo hatukuingia ndani tukamuacha getini tukaondoka na Mke Wangu tunashangaa uku tumeguswa na kilichotokea

Sina mda mrefu nimeoa ila yesterday heart break ilikua touching sana nishauri tu guys tuwe makini tunapochagua wake tusiwatese watoto za watu hivi sio sawa kabisa sio sawa fikiria we we ndio umefanyiwa hivi na Mke wako wa ndoa pengine alafu yeye ndio chanzo cha tatizo lakini bado anakufanyia mambo ya ajabu. Ufike wakati tuheshimu wake zetu.
Tunajidanganya tu kuwa sisi ni watu poa, waungwana na wenye upendo. Ila hakuna watu wabinafsi, wanafiki na wazushi kama watanzania hasa linapokuja suala la kuwatendea wenzao. Dah huyo jamaa ni mbinafsi wa hali ya juu. unaweza kusababisha uhai wa mtu ukakoma.
 
Hao wataelewana tu, mambo ya ndoa ni makubwa, niliwahi kusuluhisha migogoro ya ndoa za ndugu zang na marafiki pia ingawa sijaoa lkn yafaa wawili wakae pamoja waamue na mara nyingi sana mwishoni huwa ni kurudiana
 
I wishi i kuldi bi braza yake jamaa hasingekuwa salama mpka mda huu..
 
Kumamayo mke unikute na mchepuko uanze kunikoromea utanijua mi nani hakiamungu walai nisubiri nyumbani ndio unikoromee
Tuwe fair ila mimi ukinikuta hapo hapo unaniadabisha,Usichopenda kufanyiwa usimfanyie mwenzako.Sisi ni wavumilivu sana sana so usimchukulie poa mkeo mheshimu tu hata kama unamakandokando
 
Heeee
Kumbe Urban Gentlemen Umeooooaa? !
Du
Na kunisumbua kote kule mpaka nikaku block, kweli leo nimekamata mwizi!

Shame on u!
[HASHTAG]#PYTHONWAKIUMEAU?![/HASHTAG]
Are you matured?
Haya ni mambo ya kuyaongea humu so unataka kumchafulia na yeye aonekane ni mbaya au vipi ..aise sijawah ona hii, unakuja kwenye hadhira kama hii kumsema mtu ambaye yumo humu humu na zaidi kwemye uzi wake kwamba alikutongoza , ..sasa perioud ya yeye ameoa na mda ambao aliku approach ni mda gani?
mtu ameku approach ..umemkataa hadi umemblock si basi...
yan wanawake wa aina yako ni wasiostaarabika na haujafundwa ukafundika. Huna staha ya maneno.
 
Back
Top Bottom