LAPF VS PPF: Mfuko upi una benefits nzuri?

Fanya ufanyalo lkn usije ukajiingiza lapf nenda nssf haraka. Lapf yenye makao makuu dodoma ni janga la taifa

Haupo sahihi Mkuu, LAPF ni moja kati ya mifuko bora ya hifadhi ya Jamii, ni member huko, nimebadili waajir kama watatu ila bado nachangia LAPF, nina kawaida ya kwenda ofisi zao kila miezi 6 (Iringa), statement naipata in a minute na inaendana kabisa na michango yangu, kulitokea ucheleweshaji Oct-Dec, 2012, walinipa maelezo ambayo yaliniridhisha, nilipoenda baadaye mzigo huo, nipo happy na LAPF. NSSF nilishakimbia na sirudi ng'o
 
mkuu hakuna cha nssf wala ppf, tena ppf usiiwaze hata kidogo utakufa kwa presha sikku utapotajiwa mafao yako

mfuko bora ni lapf, lapf wanatoa interest ya hela yako, hamna mfuko unaotoa interest hapa tz zaid na lapf.

Ukitaka kujua ubaya wa ppf watafte wazee wastaafu wakwambie live evidence, hata formula yao ni mbovu. Prof shivji ni shuhuda mzuri kwenye hilo swala.
 
Kwa tathmini yangu ya haraka, PPF, na NSSF ni majanga.
Naomba kujua juu ya mfuko upi bora kati ya LAPF, PSPF, na GEPF. Ni muhimu sana mtu akasema faida na hasara ya kila mfuko.
 
Wana JF.

Mifuko yote ni MAJANGA. Sababu kuu ni hizi zifuatazo:

1. Matumizi mabaya ya pesa za wanachama (expenditures are very high - running costs za majengo yao ni balaa, Ma investment ni janga lingine, ukioneshwa gharama za operations on administration utakufa kwa pressure, wanapeanamasafari kila kukicha Kama mbinu laini ya kula, hayo ma sabasaba, nane nane, Ma diaspora, member seminars, misaada chini ya kivuli cha Corporate social responsibility, n.k n.k n.k MAJAAANGAAAA!!!!

2. Viongozi ni miungu watu - wengine wamekaa kwenye hivyo vyeo muda mrefu mpaka WAMEKINAI. Hawana maono mapya tena, ukileta jambo jipya unapigwa BAN.

3. Siasa zimeingizwa kwenye mambo ya msingi, mfano actuarial reports zenye kuonyesha uwezo wa mifuko ni siri, pia kuna kauli tata za viongozi kuhusu uwezo wa mifuko n.k

4. Ongezea....

Queen Esther
 
Hata LAPF wanalo fao la matibabu, na formula Yao ya kukokotoa ni nzuri kuliko NSSF. Sema kiukweli PPF kwa sasa ni janga. Nasikia eti wana fight Regulator wao alazimishe mifuko yote iwe na formula moja. Huyo mama naye ni majanga
Ndugu yangu huyo mama wa SSRA ni janga kuliko majanga yote niliyopata kuyashuhudia katika maisha yangu, huu ni mwaka wasita kama sijakosea tangu taasisi hiyo ianze, sijakiona walichofanya zaidi ya kuanzisha zogo Bungeni juu ya Fao la kujitoa, naona hicho ndicho waliona ni changamoto kubwa, wakaacha mambo muhimu ya kustanderdise ffomula za Mafao ya wastaafu.

Mifuko yote ni noma isipokuwa PSPF pekee ndo wana fomula nzuri na inatekelezeka, ingawa nao wamewasahau wastaafu wa siku nyingi wenye vipensheni vya sh. 20,000.00 kwa mwezi.
 
Nssf bomba tena sana sana lile fao lao la matibbabu kwa wanachama wake.

Umeshawahi kuhudumiwa kwa fao hilo la matibabu au unafagilia kitu usichokijua? Mimi nimewahi mara moja halafu nikaachana nalo maana nilipewa hospitali mbili tu za kutibiwa, nikienda likizo kwetu Kamachum Bukoba imekula kwangu labda nisiugue. Siku hizi nimejiunga na Bima ya Afya (nhif) natibiwa popote ndani ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, kwa kweli huko nimepumua, maana juzijuzi nimelipiwa Kipimo cha Citiscan pale Regency bila mkwara wowote.
 
Ndugu yangu huyo mama wa SSRA ni janga kuliko majanga yote niliyopata kuyashuhudia katika maisha yangu, huu ni mwaka wasita kama sijakosea tangu taasisi hiyo ianze, sijakiona walichofanya zaidi ya kuanzisha zogo Bungeni juu ya Fao la kujitoa, naona hicho ndicho waliona ni changamoto kubwa, wakaacha mambo muhimu ya kustanderdise ffomula za Mafao ya wastaafu.

Mifuko yote ni noma isipokuwa PSPF pekee ndo wana fomula nzuri na inatekelezeka, ingawa nao wamewasahau wastaafu wa siku nyingi wenye vipensheni vya sh. 20,000.00 kwa mwezi.

Unataka kunishawishi kuwa PSPF ni bora kuliko LAPF? Kuna mdau kasema ana ushahidi kuwa LAPF wanalipa interest kwenye michango ya mfanyakazi. Vipi kwa hawa pspf?
 
Samahani kwa kuchelewa kukujibu. Sina uhakika sana lakini kama ni suala la Interest m,bona hata NSSF wanatoa interest kwenye michango. Suala la Msingi hap[a ni fomula wanayotumia kukokotoa mafao, PSPF kiboko bwana, mtu kuondoka na Lump sum ya miliono mia tatu, mbali na Pensheni ya kila mwezi wewe unaionaje??
 
Back
Top Bottom