Kanuni mpya ya mafao kwa wastaafu kupata 25% inayobaki 75 kuunganishwa katika pension ya mwezi

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Hebu fikiria. Umefanya kazi kwa miaka 32 ukiwa mtumishi mwaminifu, na ulipofika miaka 60 ukastaafu kwa mujibu wa sheria. Unalipwa pensheni yako kwanza mkupuo wa 25% halafu asilimia 75 inayobaki unaambiwa utalipwa kila mwezi hadi ufe.

Lakini bila kutarajia, mara tu baada ya kustaafu, kwa kuwa mwili haujishughulishi sana, afya yako inadhoofika kwa kasi. Baada ya miaka mitatu toka kustaafu unapatwa na kifo.

Ndugu zako wanaambiwa wasihofu, wataendelea kupata pensheni yako kwa miaka mitatu tangu ufe, baada ya hapo ndio basi tena. Waambiwa hakuna kitu tena.

Kwa hiyo baada ya kustaafu, ile 75% ya pensheni serikali iliyosema italipwa hadi ufe, imelipwa kwa miaka sita tu. Tena wewe ulikuwa na bahati, angalau uliishi miaka mitatu baada ya kustaafu. Kuna waliokufa mwaka huo huo wa kustaafu!

Sasa jiulize, serikali inakutendea haki kweli, wewe na familia yako?

Serikali inajua wazi kwamba wastani wa umri wa kuishi kwa Watanzania ni miaka 65, na juzi hapa tu ndio walisema inaweza kuwa 66 (Life expectancy in Tanzania rises to 66.7 years) Hiyo ni rekodi ya kisayansi. Sasa iweje serikali inatunga sheria hii kwa kusema eti inategemea watu wataishi miaka 25 baada ya kustaafu, yaani kuwa pensioners kwa wastani wanakufa wakiwa na miaka 85?

Hivyo ni wazi serikali inajua wazi kwamba watanzania wengi wakisha staafu sana sana wataishi miaka mitano tu na kisha kufa, na hivyo sehemu kubwa ya ile 75% uliyoambiwa utaipata kwa maisha yako yote unakuwa umeichangia serikali!

Ni jambo la kushangaza. Uovu na uonevu kama huo hufanywa na serikali isiyojali watu wake pekee, kuwa umri wa kustaafu ni miaka 60, rekodi ya kitaifa ya wastani wa maisha kuwa miaka 65, halafu serikali inatunga sheria inayosema ukistaafu ukiwa na miaka 60 utalipwa 25% ya pensheni yako na 75% utalipwa kila mwezi maisha yako yote. Maisha yako yote yepi wakati serikali inajua wastani wa maisha ya Mtanzania ni miaka 65? Kurekebisha hili, serikali inabidi iweke kipengele cha pensiner aliyekufa kabla ya miaka 12.5 ya ukokotoaji haijaisha, la sivyo hii ni pata potea ya serikali kujipatia mapato toka wastaafu wanaokufa mapema, ambao ni wengi zaidi ya wale watakaoishi miaka 12.5 baada ya kustaafu.

Ukweli ni kwamba serikali imewapiga Watanzania dongo la macho, na inawaibia kwa kucheza pata potea ambapo inajua wazi kwamba katika wastaafu wote, huenda ni 25% tu wataishi zaidi ya miaka 70! Kwa hiyo ni wazi kwamba hapa mwenye kufaidika na pesheni yako sio wewe au familia yako, ni serikali!

NB: Katika kuhalalisha serikali kuchukua mafao ya mfanyakazi ikiwa atakufa mwezi mmoja baada ya kustaafu, Mkurugenzi wa Sheria wa Mifuko ya Jamii, Onorius Njole, amesema kwamba mfuko wa jamii ni kama BIma, kuna wanaopata na wanaokosa. Lakini hii si kweli, kwa kuwa katika Bima ulipwaji hufanywa kufaidisha warithi kifo kinapotokea, sio bima kufaidika kifo kinapotokea. Kama mfko wa jamii unataka kujiendesha ki-bima hilo ni suala jingne kabisa, ambapo uchangiaji wa mifuko ya jamii unaweza kufanywa kama malipo ya kila mwezi ambapo bima itaiva (maturity) mfanyakazi akifika miaka 60, na kuwa na haki ya kulipwa fedha zote za bima au yeye kuamua alipwe kidogo kidogo. Na pia tungependa ufafanuzi wa malipo kwa warithi ikiwa mchangiaji wa mfuko atakufa tuseme mwezi mmoja kabla ya kustaafu.


=======

Hivi ndivyo mafao yatakavyokuwa

SHERIA mpya ya sekta ya hifadhi ya jamii imeweka utaratibu wa kulipa mafao kwa mkupuo kwa asilimia 25 na asilimia 75 inayobaki italipwa kama mshahara kwa mstaafu kwa miaka 12.5.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, umri wa kustaafu ni miaka 55 kwa hiyari na miaka 60 kwa lazima, lakini kwa kada maalum kama vile madaktari na maprofesa, umri wa kustaafu ni miaka 60 kwa hiari na miaka 65 kwa lazima.

Sheria hiyo imeunganisha mifuko ya PPF, PSPF, LAPF na GEPF kuunda mfuko wa PSSSF unaohudumia watumishi wa umma na mfuko wa NSSF unaohudumia watumishi wa sekta binafsi.

Kanuni za sheria hiyo zinabainisha kuwa pensheni nzima inakokotolewa kwa kuangalia moja ya 580 (1/580) ikizidishwa mara miezi ya uchangiaji na mara mishahara mizuri ya miaka mitatu.

Kwa upande wa malipo ya mkupuo, kanuni hizo zinaeleza kuwa yatakuwa moja ya 580 (1/580) mara jumla ya miezi ya uchangiaji na mishahara ikizidishwa na miaka 12.5 ambayo ndiyo muda ambao mstaafu atalipwa pensheni yake ikizidishwa na asilimia 25 ambayo ndiyo malipo ya mkupuo.

Kwa mujibu wa kanuni hizo, kikokotoo cha pensheni ya mwezi ni moja ya 580 mara jumla ya miezi ya uchangiaji ikizidishwa na mishahara minono ya miaka mitatu mara asilimia 75 ambayo mwanachama atalipwa kama mshahara kwa kipindi cha miaka 12.5 ikizidishwa na moja ya 12 (1/12).

Ofisa Sheria wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Innocent Kyara, katika ufafanuzi wake kwa Nipashe kuhusu kikokotoo hicho, alisema mwanachama aliyeanza kazi na mashahara wa Sh. milioni moja, akiwa na kiwango cha uchangiaji cha asilimia 20 kwa muda wa miezi 420 (miaka 35) atakuwa na jumla ya michango yenye thamani ya Sh. milioni 84.

Kwa mujibu wa kikokotoo cha zamani, malipo ya mkupuo kwa mtu mwenye mshahara wa aina hiyo, yangekuwa Sh. milioni 71.6, lakini kwa kikokotoo kipya atalipwa Sh. milioni 35.8, huku pensheni ya mwezi kwa zamani ikiwa Sh. 371,800 na ya sasa ni Sh. 557,800, ikiwa ni ongezeko la asilimia 15.

Kyara alisema kwa mwanachama huyo, jumla ya pensheni ya mwezi ni Sh. milioni 69.2 kwa kikokotoo cha zamani, lakini sasa atalipwa Sh. milioni 103.7, huku mafao yote yakiwa ni Sh. milioni 140.8 kwa kikokotoo cha zamani na Sh. milioni 139.6 kwa kikokotoo kipya.

Alisema mafao yameongezwa kwa asilimia 50 ya mfumuko wa bei ambao ni kati ya asilimia moja hadi 10 na kwamba mfumuko ukizidi asilimia 10, uthaminishaji wa mafao utakuwa asilimia tano na ukiwa chini ya asilimia moja kutakuwa hakuna uthaminishaji na kwamba utafanyika kila baada ya miaka mitatu.

Sheria hiyo ilipitishwa Oktoba 20, mwaka jana ikiunganisha mifuko ya pensheni na kuunda mfuko wa PSSF na kufanya marekebisho kwenye Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), ili uwe mahususi kwa ajili ya wafanyakazi wa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.

Sheria hiyo ilianza kazi Agosti Mosi, mwaka huu na kanuni zake zilishatangazwa kwenye gazeti la serikali.

Nipashe
 
Hii inayolipwa 25% ni pencheni (pension) au kiinua mgongo (gratuity)? Kwa vyovyote iwavyo, hapa kuna udhaifu. Sijui sheria yenyewe inasemaje. Wajuzi watusaidie kwani wengine tunaelekea huko huko.
 
Tatizo watu ambao wanapeleka haya mapendekezo utafili sio wafanyakazi wao. Angalia wabunge wanavyo jipitishia maslai yao. Just utumishi wa 5 years tena pengine usio tukuka unakula kifuta jasho cha haja.

Hapa nakataa wanasiasa kuhusishwa, ni uzwazwa wa watunga sera wetu ambao wao pia ni watumishi. Ndio maana watu wana kuwa wezi na wapiga deal/rushwa kama mtu unaona mbele giza kwa nini usibutue kombe mwana haramu apite!

Arafu tunalalamika hii nchi ilikuwa imefika pabaya. Boresheni maslahi ya watumishi ya sasa na badae uone kama mtu ataangaika na virushwa vya chai au kubrashia viatu.

Miaka pia ipunguzwe mpka 55 kuwapisha vijana kuchukua nafasi na wazee kusaidia kulea wajukuu.
 
Hii inayolipwa 25% ni pencheni (pension) au kiinua mgongo (gratuity)? Kwa vyovyote iwavyo, hapa kuna udhaifu. Sijui sheria yenyewe inasemaje. Wajuzi watusaidie kwani wengine tunaelekea huko huko.
Mkuu, sheria inasema ukistaafu unapewa 25% ya pensheni yako. Asilimia ile nyingine 75, utakuwa unalipwa kila mwezi hadi ufe. Ukifa, iwe ni mwezi mmoja au miak 25 baada ya kustaafu, familia yako itaendelea kupata pensheni yako kwa miaka mitatu tu. Baada ya hapo hakuna kitu tena.

Serikali inasema imefanya hivi ikitegemea watu kuishi miaka 25 baada ya kustaafu!
 
Mimi naomba kujua hii ni mafao ya UZEE watumishi wa umma au ni zile dunduliza za NSSF, PSPF, Sijui wapi na wapi please naombeni kulijua hili
Hizo ni pesa unazowekewa NSSF, PSPF Mkuu, mchango wako na wa mwajiri. Ndizo hizo utalipwa 25% na nyingine 75% kila mwezi hadi ufe, serikali ikisema imefanya hesabu utaishi miaka 25 baada ya kustaafu. Ila ukifa imekula kwako. Familia yako italipwa kwa miaka mitatu tu.

Itafikia mahali familia zitafanya siri pensioner akifa serikali isijue! Ila sasa kupata yale malipo ya kila mwezi, kila baada ya muda fulani unataiwa uende wakuone kujihakikishia hujafa bado!
 
Hizo ni pesa unazowekewa NSSF, PSPF Mkuu, mchango wako na wa mwajiri. Ndizo hizo utalipwa 25% na nyingine 75% kila mwezi hadi ufe, serikali ikisema imefanya hesabu utaishi miaka 25 baada ya kustaafu. Ila ukifa imekula kwako. Familia yako italipwa kwa miaka mitatu tu.

Itafikia mahali familia zitafanya siri pensioner akifa serikali isijue! Ila sasa kupata yale malipo ya kila mwezi, kila baada ya muda fulani unataiwa uende wakuone kujihakikishia hujafa bado!


Mmmh HOPE HII SHERIA BADO HAIJAPITA..... Sitaki kuzeesha ubongo kwa kuifikiria jamani................ Mungu atuondolee huu mkosi/janga
 
Mmmh HOPE HII SHERIA BADO HAIJAPITA..... Sitaki kuzeesha ubongo kwa kuifikiria jamani................ Mungu atuondolee huu mkosi/janga

Sadly and unfortunatedly, imeshapitishwa

1542187341289.png
 
Mkuu, sheria inasema ukistaafu unapewa 25% ya peshini yako. Asilimia ile nyingine 75, utakuwa unalipwa kila mwezi hadi ufe. Ukifa, iwe ni mwezi mmoja au miak 25 baada ya kustaafu, familia yako itaendelea kupata pesheni yako kwa miaka mitatu tu. Baada ya hapo hakuna kitu tena.

Serikali inasema imefanya hivyi ikitegemea watu kuishi miaka 25 baada ya kustaafu!
Sasa huu si ujambazi, sikatai ni namna nzuri ya ku control matumizi mabaya maana kuna wastaafu wengine wanakuwaga vimwaga, na mbwembwe za kuongeza wake halafu baada ya mwaka mtu toka 70 millions hana hata mia anaanza kutia huruma kwa mke mkubwa!

Wanalofanya ni sahihi ila swala la ku cease funds za mstaafu miaka mitatu baada ya kufa badala ya kuwapa yote kama lumpsum wanufaika wake pesa iliobaki kwenye mfuko sio sawa!
 
Back
Top Bottom