Muswada wa kuunganisha mifuko unapunguza mafao; walio LAPF na PSPF kulipwa kiduchu kama NSSF ya sasa

kilambimkwidu

JF-Expert Member
Jul 21, 2017
6,052
7,057
WANABODI,

NIMEFUATILIA KWA KINA MUSWADA WAKUUNGANISHA MIFUKO NA KUANZISHA MFUKO MMOJA MPYA (PSSSF), NA HAYA NDIO MAJANGA YA MUSWADA

Muswada wa kuunganisha mifuko ya PPF, LAPF, GEPF na PSPF na kuunda mfuko wa (PSSSF) umebeba "misiba" mikubwa mitatu kwa watumishi na wanachama wa mifuko hiyo wakiwemo ndugu wabunge, majaji wa mahakama na watumishi (members) wa kawaida.

1. UNAPUNGUZA MAFAO NA WASTAAFU WOTE, HATA WA PSPF NA LAPF WATATAKIWA KULIPWA KAMA WASTAAFU WA SASA WA NSSF.

Muswada unapendekeza (kwa kificho) kwamba baada ya kuunganisha mifuko, kanuni itakayotumika kulipa mafao ya kustaafu ni kanuni ile iliyotungwa na SSRA mwaka 2014 (soma section 30 ya muswada). Ifahamike kwamba kanuni ya SSRA ndiyo inatumika mpaka sasa na mifuko ya PPF, NSSF na GEPF wakati LAPF na PSPF wanaendelea kutumia kanuni zao (kwa wanachama waliokuwepo kwenye mfuko kabla ya kuanza kanuni hiyo ya SSRA). Hapa ni muhimu kufahamu kwamba, kanuni ya SSRA haikuwa inawahusu PSPF na LAPF kwasababu ya principles za pension duniani kwamba kwenye mifuko ya DEFINED BENEFIT hapatakiwi kutunga kanuni itakayopunguza mafao ya mwanachama ambaye tayari alishajiunga na mfuko kwakua "mkataba umeshafungwa". Huu ndio utaratibu unatumika ulimwengu mzima kwa mifuko ya pension (ya Defined Benefit). Principles hizo zinaongeza kwamba mamlaka za usimamizi (kama hii SSRA yetu) zitatakiwa kumlinda na kutetea maslahi ya mwanachama na kama kuna mabadiliko ya sheria basi sheria hizo ziongeze wingi (ujazi) fao lakini SIYO kupunguza.

NINI KINAPASWA KUFANYIKA?

(a) mfuko mpya ulipe mafao ya kustaafu kwa kutumia kanuni ya PSPF au LAPF na sio kanuni ya SSRA kwakua inapunja mafao na inawapunja hata wale ambao watastaafu kesho na keshokutwa na wangelipwa kwa kanuni za mifuko yao ya LAPF au PSPF.

(b) Sheria ilitakiwa kutaja moja kwa moja kanuni itakayotumika kulipa mafao ili wabunge na wanachi wajue. Muswada usiigiche kanuni (hata sheria za mifuko zilikua zinataja moja kwa moja). Kinyume chake, kuruhusu mafao kulipwa kwa mujibu wa Guidelines za SSRA ni kuleta mtikisiko kwenye mafao kwakua hata hiyo kanuni ya SSRA utungaji wake haushirikishi wabunge hivyo inaweza kubadilishwa tena na tena kinyemela muda wowote kwakua anaesaini kuidhinisha kanuni hiyo kubadilika na kuanza kutumika moja kwa moja ni Mkurugenzi Mtendaji wa SSRA tu. Ndugu wanabodi, kanuni ya kulipa mafao ndio moyo wa sheria ya mafao na ni jambo lenye maslahi mapana ya wanachama na ingefaa iwekwe kwenye sheria na ili wakati wowote inapotakiwa kufanyiwa mabadiliko, wabunge/wawakilishi wa wanachi wahusishwe na wajadili kwa upana ili kulinda maslahi ya wanachama.

(c) Au angalau sheria iwalinde wanachama kwa kusema kwamba "wanachama waliokua wakinufaika na sheria za PSPF na LAPF (na GEPF coz nao walikua wanahamisha wastaafu PSPF) Mfuko mpya utaendelee kuwalipa mafao ya kustaafu kwa kanuni za mifuko waliyokua wakichangia kabla ya sheria hii ya kuunganisha mifuko.
305c731dfd8c2e85818fcc2653673f38.jpg


2. FAO LA KUJITOA "HALITATOLEWA", HIYO "UNEMPLOYMENT BENEFIT" SIO FAO LA KUJITOA.

Hiyo wanayoita "unemployment benefit" (soma section 29(1) (e) ya muswada) sio fao la kujitoa ispokua ni malipo flani tu ambayo serikali italipa kwa watu WOTE ambao hawajaajiriwa (kama selikali itaamua na kama fedha zitakuwepo. kumbuka hata wazee na wataanza kulipwa pensheni serikali ilisema). Tena ukisoma zaidi ile section 29(2) muswada unasisitiza kwamba fao hilo litatolewa na mfuko huu mpya "kama waziri ataliwekea utaratibu/regulations"! Ikumbukwe kwamba withdraw (yaani fao la kujitoa) halina kanuni ispokua ni michango ya mtu tu basi.

Sheria hii ingetaja "withdraw benefit" inamana wanachama wanaaoachishwa kazi wangeweza kuchukua michango yao na kujitoa kama ilivyokua kwa NSSF na PPF kabla hawajaanza ubabaishaji mwaka jana. Bila kuwepo kwa fao la kujitoa, waajiri (serikali) inaweza kutumia hicho kibano kama fimbo kwa watumishi kwakua mwajiri akiamua kukufukuza kazi haupati chochote (kama ilivyokua miaka ya '90) na au usubiri pensheni ukifika miaka 55 (kama utakuwa hai). Na ikumbukwe kwamba ili ulipwe pesheni lazima uwe ulifanya kazi na kuchangia kwa miaka 15, kwahiyo ukigukuzwa na miaka yako 3 au 4 hupewi michango yako na utasubiri hadi miaka 55 na bado hautalipwa pensheni, utarudishiwa hela yako ileile (zingatia kushuka thamani)

3. MUSWADA HAULIPI "Deffered Pension" KWA WATU AMBAO WAMESHAFIKISHA MIAKA 15 YA KUCHANGIA ILA HAWAJAFIKISHA UMRI WA KUSTAAFU

Kwa kawaida, hua kanuni za ulipaji pensheni zinaruhusu mwanachama aliyefukuzwa/achishwa kazi huku akiwa tayari amechangia kipindi kinachokubalika kulipa pensheni (miaka 15 au michango 180), mwanachama huyo hata kama hajafikisha miaka 55 (tuseme awe na miaka 40) anaweza kukokotolewa malipo ya mkupuo (ile lumpsum) na analipwa halafu anasubir afikishe miaka ya kustaafu ili aanze kulipwa ya kila mwezi. SABABU NI HII: moja; hata akisema asichukue ile lumpsum mpaka atakapo staafu bado atalipwa hela sawa na anavolipwa leo akiwa na miaka 40 na amechangia michango 180. Sabau ya pili ni kwamba mtu ambaye ameshafanya kazi na kuchangia kwa miaka 15 (tuseme alizna kazi na miaka 25) tayar atakua kafikisha miaka 40 ambayo inawezekana asiweze kuajiriwa kabisa na akawa kakaa bure tu.

HIVYO BASI, shime wabunge wetu na wadau mzingayie mambo hayo makubwa matatu (hasa la kwanza na la tatu) kwakua muswada unapendekeza mumnyonya mwanachama kwa (hata yule ambaye alishaingia mkataba na PSPF na LAPF) kwamba atalipwa kwa kanuni inayolipa zaidi ya hii ya SSRA ambayo tayari NSSF wanaitumia hadi sasa na bado wastaafu wanalia sana. Kwa utafiti niliofanya, watumishi wawili wa RAHCO walioajiriwa pamoja na kufanya kazi kitengo kimoja wakati mmoja anachangia NSSF mwingine PSPF hadi kustaafu, mwanachama wa PSPF atalipwa mafao yaliyozidi ya wa NSSF kwa 40% ( yaani atapata NSSF+ 40 ya NSSF tena). Ushahidi huu unaweza kuupata kwa kuulizia wastaafu au hata ukitengeneza scenario kwa kanuni ya SSRA na ya PSPF.

Ni wazi kwamba kama kanuni ya SSRA ndo italipa wote kama muswada unavopendekeza mzigo wa PSPF iliyofilisika utakua umepungua (kwasababu wastaafu wote watalipwa kwa hela za ppf, lapf na gepf ambazo bado ziko vizuri kifedha) lakini maumivu ya kufilisika pspf yatabebwa sasa na watumishi wa umma kwenye mfuko wao mpya kupitia kanuni ya ssra inayonyonya mafao.

SSRA hua wanasema "kujitoa SIO fao", sisi tuseme kwamba by whatever name, watumishi wanataka hela zao pale wanapoachishwa kazi kwakua kupata kazi na kuendeleza uchangiaji ni majaliwa magumu kwa jinsi hali ilivo!
8f5a5ceaaa5b4b54876ef4f42d1bb8d5.jpg


Mamlaka hii ya Usimamizi Mifuko ya Kijamii itekeleze wajibu wake wa kuishauri serikali ili kutetea maslahi ya mwanachama na sio kuleta miswada inayonyonya mwanachama huku ikitoa ufafanuzi kwa hoja mufilisi!

KILAMBIMKWIDU
 
Aiseee withdraw benefit ilikuwa msaada sana. Hii mifuko sasa imekuwa ya kinyonyaji sana
 
Ni kweli mkuu,

Mimi nafikiri wahusika wanaliona hilo ila it's like mswada upo hivyo makusudi (bila kujali kuwa watumishi wananyonywa kiasi gani) ili kupunguza mzunguko wa fedha hizi baina ya mifuko na watumishi lakini pia ili waweze kuzitumia fedha za mifuko kama itakavyowapendeza.
 
Mambo matatu muhimu ambayo yataleta shida sana kwenye jamii..

Muajiri atakuwa na kiburi cha kunyanyasa mfanyakazi, mfanyakazi itambidi atafute kazi akiwa kazini ili aweze kujikimu huku akiwa hana raha wala faraja maana kukaa mtaani na kutafuta ajira kutakufanya usiwe na pesa yakujikimu kwa muda huo usiojulikana.

Vijana wengi watakosa fursa za kwenda shule na kujiajiri.. Fao hili lilitumika sana na vijana kujiajiri na kwenda shule kuongeza Elimu maana walikuwa na uhakika na hii fedha..

Serikali lazima ijue watu wake wengi ni masikini hivyo huishi kiujanjanja na akili nyingi ili kupambana na huu umasikini, Fao la kujitoa husaidia watu kujitibu au kutibu ndugu zao wa karibu pale ugonjwa unapomkumbuka mhusika mwenyewe au ndugu wa karibu, Gharama za matibabu ni ghali kiasi cha matibabu mengine kupatikana nje ya nchi...
 
SERIKALI IJARIBU KUTENGENEZA VITU VITATU RAHISI, FAO LA KUJITOA, PAYE NA PENSION FUND.

PAYE NA SOCIAL SECURITY FUND VIPUNGUZWE KWA ASILIMIA FULANI NA JUMLA YAKE IINGIE KWENYE FAO LA KUJITOA, PIA IHAKIKISHE HUO MCHANGO WA FAO LA KUJITOA KWA MWEZI UNAKUWA MKUBWA KULIKO SOCIAL SECURITY FUND YA SASA YA MTU BILA KUINGILIA MSHAHARA WA SASA.

HIVYO KWENYE MAKATO MAPYA NDANI YA SALARY SLIP ISOMEKE ; PAYE, PENSION FUND NA FAO LA KUJITOA.
HILI FAO LA KUJITOA IKITOKEA MTU AKIACHA AU KUACHISHWA KAZI ANACHUKUA AU LA AKIAMUA LIBAKI MPAKA ANAFIKA HIYO 60 ANALIPWA HELA YAKE NA HIYO PENSIO FUND NDIO ANAPEWA KIDOGO KIDOGO.

 
Je kwa sasa hivi kwa wale waliofukuzwa mika 5 iliyopita na wanapigwa danadana na NSSF watapataje hela zao?
 
Serikali ya ccm imeifilisi kabisa hii mifuko kwa kuikopa bila kulipa, sasa inaamua kutunga sheria kandamizi na za kinyonyaji kwenye fedha za wanachama ili kuifavour/kuilipa fadhila mifuko hii maana uwezo wa kulipa hawana! KUAJIRIWA TENA MIMI BASI!
 
KAMA IMEFUTWA.....naomba niusemee moyo maana kwenye usimnwage mchele kwenye kuku wengi.

Inauma , inauma, inauma, kuna haja gani hela za mtu ikatwe ikifika wakati wa kutaka eti wafanye uchunguzi kama ana ajira???
 
Back
Top Bottom