CHADEMA wasibembelezwe katika meza ya mazungumzo maana ni vigeugeu na waliyokosa msimamo

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,187
9,633
Ndugu zangu, ukifuata akili za CHADEMA na wana CHADEMA na viongozi wao lazima upotee, upoteze dira, muelekeo na kuchanganyikiwa. CHADEMA ni chama kisicho na msimamo, dira aala muelekeo, hakina misingi inayokiongoza na kusimamia.

Ni chama ambacho huwezi ukajua baada ya mwaka kitakuwa wapi na kitakuwa kinasimamia nini. Hakina ajenda ya kudumu na kueleweka, hakieleweki msimamo wake ni upi.

Ni chama kinachoruka na matukio kama kimbunga, ni chama kilichokosa viongozi wa kukipa muelekeo, hakina viongozi wa kuweka msimamo ambao ukaeleweka ndiyo msimamo wa chama juu ya Jambo fulani.

Ndani ya CHADEMA kila kiongozi anao msimamo wake kulingana na maslahi yake, na jinsi mambo yake yatakavyo kwenda ndivyo atakavyotaka uwe muelekeo wa wote. Hakuna msimamo wa pamoja ndani ya CHADEMA, ndiyo sababu utaona kila mtu akikurupuka kivyake na kuongea kivyake juu ya jambo fulani na kutaka kuwa ndiyo msimamo wa chama.

CHADEMA siku zote wana damu ya usaliti, ukigeugeu na kukosa msimamo ndiyo sababu leo wanaweza mnanga fulani ni fisadi lakini kesho wakampamba kuwa ndiye malaika aliyekuja kuwakomboa akili zao na kuwapeleka nchi ya ahadi. Ndiyo maana unaona hawaaminiani wala kusimama pamoja.

Ndio sababu ya kuona vijana wengi wamepoteza ndoto zao, malengo yao, maisha yao, kwa sababu ya ubabaishaji na ulaghai wa kisiasa kwa vijana. CHADEMA wanaweza kukujaza upepo kichwani na ukishajaa na kupasuka wanakuacha ulipo na kusambaratika kila mtu na njia yake.

Rais wetu na Mwenyekiti wa CCM Mama Samia ameonyesha dhamira ya kuhitaji kutaka kuona kila mmoja wetu anashiriki katika ujenzi wa taifa letu. Amefungua milango yote ya maridhiano, amenyoosha mkono wa amani na upendo kwa kila mtu, amefuta mstari wa uchama na kuweka uwanja wa maridhiano na mshikamano, amefungua milango ya kidemokrasia na siasa za kirafiki na kiungwana ili kila mtu ajione na afurahie kuwa Tanzania.

Ndiyo sababu ya kuona kauli zake na matendo yake Rais wetu yamekuwa ni ya upendo na kuhubiri mshikamano na umoja wa kitaifa, amekuwa akitoa kauli za kujenga na siyo kubomoa.

Lakini licha ya juhudi hizi zote za Rais bado CHADEMA wanaendelea na tabia zao za ukigeugeu, kujiona wao ni wakipekee, wanaotakiwa kupewa uangalizi wa kipekee, kusikilizwa kipekeee na kudekezwa kama mtoto mdogo kwa bibi yake.

Rais anahubiri amani lakini wao wanahubiri vita vya kisiasa, kutunishiana misuli, ubabe wasiyouweza, matamshi ya kuvuruga mazungumzo na mengine mengi yenye vurugu za kuharibu maridhiano

Hii yote ni kwa kuwa CHADEMA kimekosa safu ya kiuongozi yenye nguvu ya kusikilizwa, kutoa muongoza njia, muelekeo, dira na msimamo wa pamoja. Viongozi ndani ya CHADEMA hawaheshimiki kwa wanachama wao. Ndiyo sababu chama kinaendeshwa na vijana na wanaharakati wa mitandaoni.

Ndiyo sababu kunakuwa na mvurugano wa kimsimamo na kiajenda. Viongozi ndani ya CHADEMA wanafanya vitu kuwafurahisha wafuasi wao ambao kwa bahati mbaya ni kuwa wengi wao uwezo wao ni mdogo sana.

Viongozi wao wanafanya vitu kwa msukumo wa kupata ufuasi wa mtu binafsi badala ya chama, ndiyo sababu kule CHADEMA ili uwe mgombea na kuitwa Kamanda basi wewe tukana sana matusi, hata ikibidi nenda kituo cha polisi na kuwatukana sana, hakika hapo lazima CHADEMA wakupe uongozi hata kama huna sifa wala vigezo vyovyote vile vya kiuongozi.

Hivyo rai yangu kwa serikali yangu na chama changu cha CCM ni kuwa wasiwabembeleze CHADEMA, kama hawataki maridhiano au kukaa katika meza ya mazungumzo kwa sababu zisizo na mashiko. Watanzania wameshaelewa dhamira njema ya Rais na hivyo wapo naye bega kwa bega na wala hawawezi kuwaelewa hao CHADEMA hata wakitamka maneno ya kichochezi.

Kikubwa ni kuwa ni lazima waongozwe tu kwa mujibu wa sheria zetu, wasilete maneno ya vitisho au uchochezi wala kuvuruga amani, utulivu, mshikamano na upendo uliyotamalaki kwa sasa miongoni mwa Watanzania.

Kazi iendeleee, Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasiyo na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu: 0742-676627
 
Unaongea Kama Nani?. Mwenyekiti wa CCM kakutana na Mbowe ikulu na Lissu ubelgiji. Wewe mpiga kelele una lipi la kusema?
Mh Rais anahitaji maridhiano na kila mtu na kila chama lakini chadema wanataka mavurugu na kutunishiana misuri
 
Mh Rais anahitaji maridhiano na kila mtu na kila chama lakini chadema wanataka mavurugu na kutunishiana misuri
Wewe ni simbilisi tu hata kukaribia wanapokaa mabosi wa ccm huwezi unaishia kujidhalilisha kila siku hapa JF kwa mada zako za kipumbavu, kama kuna anayekusoma anakudharau sana. CCM ina wenyewe na wao hawahitaji kujichora humu na kuweka namba za simu, wacha uchawa wa bei ya chini wewe dogo.
 
Chadema chama kubwa. Jiwe alipambana kuiua chadema lkn badala yake akafa yeye. Mwambieni mama aepuke mapambano na chadema
Unatumia vigezo gani kusema chadema Ni chama kikubwa wakati hakina uwezo wa kuandaa hata mgombea Urais? Ukiwa na pesa zako hata Leo ukienda chadema lazima wakupe uongozi na kukupigia magoti hata Kama huna sifa za kiuongozi
 
Chadema chama kubwa. Jiwe alipambana kuiua chadema lkn badala yake akafa yeye. Mwambieni mama aepuke mapambano na chadema
Unatumia vigezo gani kusema chadema Ni chama kikubwa wakati hakina uwezo wa kuandaa hata mgombea Urais? Ukiwa na pesa zako hata Leo ukienda chadema lazima wakupe uongozi na kukupigia magoti hata Kama huna sifa za kiuongozi
 
Mh Rais anahitaji maridhiano na kila mtu na kila chama lakini chadema wanataka mavurugu na kutunishiana misuri

Jiangalie Sana. Mwenyekiti anataka maridhiano wewe unatak Nini?. Wewe na mwenyekiti Nani wa kumsikiliza?. Punguza kelele.
 
Jiangalie Sana. Mwenyekiti anataka maridhiano wewe unatak Nini?. Wewe na mwenyekiti Nani wa kumsikiliza?. Punguza kelele.
Mwenyekiti wetu mh Rais Samia anahitaji maridhiano Sana. Je kwa uelewa wako wa kibinadamu unaona chadema wanahitaji na kuwa Tayari kwa maridhiano? Huoni kila Siku wanazungumza maneno yasiyo na Afya katika muafaka wa mazungumzo? Huoni wakiweka masharti yasiyopaswa kuzungumza hadharani wakati mazungumzo yanaendelea? Una Ina Ni sahihi hiyo?
 
Kama mtanzania

Semaa unaongea kama chawa. Nilikishauri kwenye platform Kama hii usipende kuweka namba zako wazi na huku ukibeza harakati za mwenyekiti wa CCM . Shauri yako, ndio nimekuambia. Usipende kurukia mambo yaliyokuzidi upeo yatakushinda.
 
Mwenyekiti wetu mh Rais Samia anahitaji maridhiano Sana. Je kwa uelewa wako wa kibinadamu unaona chadema wanahitaji na kuwa Tayari kwa maridhiano? Huoni kila Siku wanazungumza maneno yasiyo na Afya katika muafaka wa mazungumzo? Huoni wakiweka masharti yasiyopaswa kuzungumza hadharani wakati mazungumzo yanaendelea? Una Ina Ni sahihi hiyo?

Do Tulia alivyotoa matamshi ya vurugu uliona sahihi? Majadiliano ya ajenda nyingi na mambo mengi, sio matamko tu ya kisiasa hata maendeleo ya kiuchumi.
 
Boot licker akiwa kazini
IMG_20221101_154222.jpg
 
Wewe unazo pesa au ni mlamba viatu wa Lumumba? Sasa sijui baada ya kulamba biatu na kuvitakatisha utalamba nn tena? Au utalamba nnya??
Wewe akili yako ilishagotia katika matusi tu ,nje na hapo huwezi ukajenga hoja yoyote Ile maana umeuzoesha ubongo wako kutukana tu muda wote
 
Tueleze unachotaka tukielewe na tukuunge mkono, naona unalalama tu kwa hasira kiasi umesahau ulichonuia kutufahamisha kuhusu uovu wa Chadema, kunywa maji tulia na uandike upya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom