mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 20,458
- 36,481
Lala salama mtumishi wa Mungu aliye hai.
Nilichojifunza kwako ni kwamba Mungu wetu hawekewi mipaka, yeye humpa karama amtakaye kwa sifa na utukufu wake.
Felician Venant Nkwera (alizaliwa Luilo, leo katika Wilaya ya Ludewa, mkoa wa Njombe[1], 28 Aprili 1936 (umri 89)) ni padri aliyetengwa na Kanisa Katoliki [2] na mwandishi nchini Tanzania.
Alipata upadirisho mwaka 1968 akaanza huduma ya maombezi akiwa bado padri kijana mkoani Tabora na baadaye kuhamia jijini Dar es Salaam. Ni huduma ambayo imemfanya awe kwenye mgogoro mkubwa na jimbo alilokuwa akilihudumia wakati huo; mgogoro huo ukafika makao makuu ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na baadaye Roma.
Ni huduma ambazo wenye imani wamekuwa wakikiri kwa kinywa na maandishi kwamba wameponywa huku rozari, maji ya baraka na sala vikiwa ndio msingi mkuu wa maombi yaliyopelekea kuponywa huko. Shuhuda za uponywaji wa wagonjwa zinaandikwa ama kusimuliwa na wahusika wenyewe.[3]
Muda mrefu umepita tangu Padri Nkwera asimamishwe kuhudumia Kanisa. Baadhi wanakosoa huduma hizi za maombezi, hasa wakiangazia namna sakata hili lilivyoanza. Baadhi wanaangalia sababu kuu ni ukaidi, huku wakiainisha bayana kwamba Padri Nkwera hakuwa mtii kwa aliyekuwa kiongozi wake kwa wakati huo alipokuwa akilihudumia Jimbo Katoliki la Njombe na zaidi hakutii maamuzi na maelekezo yaliyotolewa na viongozi wake wakubwa yaani maaskofu, Baraza la Maaskofu na hata Kardinali Polycarp Pengo kwa wakati huo.[4]
CC Sky Eclat
Mwamba amelala Huduma za Fr Felician Nkwera bado zinaendelea?
UPDATES
Mwili wa Padri Felician Nkwera unatarajiwa kuzikwa Jumamosi Mei 18, 2025 katika kituo chake cha Maombezi kilichopo Ubungo jijini Dar es Salaam
Nilichojifunza kwako ni kwamba Mungu wetu hawekewi mipaka, yeye humpa karama amtakaye kwa sifa na utukufu wake.
Felician V. M. Nkwera
Felician Venant Nkwera (alizaliwa Luilo, leo katika Wilaya ya Ludewa, mkoa wa Njombe[1], 28 Aprili 1936 (umri 89)) ni padri aliyetengwa na Kanisa Katoliki [2] na mwandishi nchini Tanzania.
| Felician V. M. Nkwera | |
| Amezaliwa | 28 Aprili 1936 (umri 89) Lwilo |
|---|---|
| Nchi | Tanzania |
| Makazi | Riverside, Dar es salaam |
| Anafahamika kwa | Padri Mwasisi wa Kituo Cha Maombezi cha mAma Bikira Maria |
Maisha yake
Wazazi wa Padri Nkwera walikuwa ni Venant Nkwera (baba) na Emmaculata Mhagama (mama).Alipata upadirisho mwaka 1968 akaanza huduma ya maombezi akiwa bado padri kijana mkoani Tabora na baadaye kuhamia jijini Dar es Salaam. Ni huduma ambayo imemfanya awe kwenye mgogoro mkubwa na jimbo alilokuwa akilihudumia wakati huo; mgogoro huo ukafika makao makuu ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na baadaye Roma.
Ni huduma ambazo wenye imani wamekuwa wakikiri kwa kinywa na maandishi kwamba wameponywa huku rozari, maji ya baraka na sala vikiwa ndio msingi mkuu wa maombi yaliyopelekea kuponywa huko. Shuhuda za uponywaji wa wagonjwa zinaandikwa ama kusimuliwa na wahusika wenyewe.[3]
Muda mrefu umepita tangu Padri Nkwera asimamishwe kuhudumia Kanisa. Baadhi wanakosoa huduma hizi za maombezi, hasa wakiangazia namna sakata hili lilivyoanza. Baadhi wanaangalia sababu kuu ni ukaidi, huku wakiainisha bayana kwamba Padri Nkwera hakuwa mtii kwa aliyekuwa kiongozi wake kwa wakati huo alipokuwa akilihudumia Jimbo Katoliki la Njombe na zaidi hakutii maamuzi na maelekezo yaliyotolewa na viongozi wake wakubwa yaani maaskofu, Baraza la Maaskofu na hata Kardinali Polycarp Pengo kwa wakati huo.[4]
Kesi mahakamani
Padri Felician V. Nkwera amekuwa na kesi nyingi mahakamani huku baadhi ya waumini au wafuasi wake pia wakiwa na kesi zenye sura tofautitofauti.Vitabu na machapisho yake
- Tumbuizo la jioni (1968)[5]
- Johari Ndogo (1979)
- Sarufi na Fasihi Sekondari na Vyuo (1979)[6]
- Kiswahili Sekondari na Vyuo (1979)
- Maana na Lengo la Adhabu ya Kifungo (1987)[7]
- Tamrin za Fasihi Simulizi, Secondary na Vyuo (1998) [8]