Laiti kama kweli Mungu hayupo... Nini itakuwa hatma ya viumbe wanyonge?

Ph-25

JF-Expert Member
Nov 19, 2012
1,159
537
Habari za mida wakuu...

Ni muda sasa tangu mabishano juu ya uwepo wa mungu kuzuka humu ndani na kutokea kwa makundi moja linaamini juu ya uwepo wa kiumbe huyo... Na lingne halisadiki hamadani juu ya uwepo wake...

Binafsi sielewi kabisa nini hasa itakua hatma ya viumbe ambao wana nyanyaswa,kuu wawa na kudhurumiwa haki zao ktk jamii even mahakamani pia hawapati haki zao...

Abortion,mauaji ya imani za shirki, haya yote kweli ndo yanaishia hapa duniani bure bure kweli.?

Kama mungu hayuko kweli basi inamana hata hata siku ya ukumu haiko.? Je.? Hawa wasio amini uwepo wa mungu wanaamini kama duniani kuna zambi.?

Wadau embu tuingie dipu ktk hoja hii bna ili tuelewe haya mambo kwaundani...

Tunaitaji refference za vitabu mbali mbali ktk hili wadau.

Cc Kiranga Eiyer Mshinga Nyani Ngabu na wadau wengine pia.
 
Last edited by a moderator:

Mungu sio kiumbe,kiumbe ni kilichoumbwa,binadamu,wanyama,majini,nk ndio viumbe kwasababu vimeunbwa.Mungu anaitwa Mungu tu, sio kiumbe.
 
Last edited by a moderator:
Habari za mida wakuu...

Ni muda sasa tangu mabishano juu ya uwepo wa mungu kuzuka humu ndani na kutokea kwa makundi moja linaamini juu ya uwepo wa kiumbe huyo... Na lingne halisadiki hamadani juu ya uwepo wake...
Kwanza Mungu ninaemjua mimi sio kiumbe!
Hivyo nakuomba urekebishe kauli!
Binafsi sielewi kabisa nini hasa itakua hatma ya viumbe ambao wana nyanyaswa,kuu wawa na kudhurumiwa haki zao ktk jamii even mahakamani pia hawapati haki zao...
Abortion,mauaji ya imani za shirki, haya yote kweli ndo yanaishia hapa duniani bure bure kweli.?
Kama mungu hayuko kweli basi inamana hata hata siku ya ukumu haiko.? Je.? Hawa wasio amini uwepo wa mungu wanaamini kama duniani kuna zambi.?
Wadau embu tuingie dipu ktk hoja hii bna ili tuelewe haya mambo kwaundani...
Tunaitaji refference za vitabu mbali mbali ktk hili wadau.
Cc Kiranga Eiyer Mshinga Nyani Ngabu na wadau wengine pia.
Unaturudisha kulekule tu
Hatujakubaliana kama Mungu huyo yupo
Kama tukikubaliana yuo itabidi tujadili ni Mungu yupi huyo
Halafu ndipo tujadili kuhusiana na haya uliyosema hapa

Sdhani kama kutakuwa na jipya hapa!
 
Ehee baba mungu uliye juu nakuja mbele zako baba. Naomba uwasamehe wote wanaoshuku kama haupo, baba hao si akili zao wanaoshuku uwepo wako bali ni mapepo machafu.

Baba naomba ufukuze hao pepo wachafu wanashuku uwepo wako. Tazama baba awajui walitendalo kwa sababu roho chafu na pepo wachafu wamewaandama.

mungu naomba uwabadilishe na watambue uwepo wako .ASante Baba kwa kusikiliza maombi yangu.

Amen
 
Mimi nishaweka "the problem of evil" hapa kama swali, na sijajibiwa.

Kuwapo kwa maovu duniani ni moja kati ya shahidi za kutokuwapo kwa mungu mwenye upendo mkuu na uwezo mkuu.

Kama mungu ana uwezo mkuu, uwezo wa kuumba ulimwengu wa aina yoyote, hata usio na maovu (usiowezekanika kufanyika maovu kama vile wewe usivyoweza kupaa angani bila msaada wa vifaa) kwa nini hakuuumba ulimwengu wetu uwe hivyo?

Kama alikuwa na uwezo nini kilimzuia? Alikuwa hajali tu?

Lakini tunaambiwa na upendo usio kifani, kwa hiyo alitupenda waja wake.

Sasa kilichomzuia kuumba ulimwengu ambao hauna njaa, matetemeko ya ardhi, magonjwa, dhoruba, kifo, watoto kuzaliwa na vilema etc ni nini?

Ina maana alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu usio na maovu lakini hakutaka tu?

Kama kafanya hivyo tutasemaje kwamba ana mapenzi makuu?

Hata baba wa kibinadamu akiwa na uwezo wa kuwapa good time wanawe halafu akawaacha waugue, wapate njaa tutamuona mbaya, hatutasema ana upendo.

Si zaidi kwa mungu ambaye anatakiwa kuwa muweza wa vyote na mwenye mapenzi yasiyo kifani?

Kweli huyu mungu yupo au stories tu?

Kama yupo mbona kaumba ulimwengu wenye maovu kibao?

Hili ndilo swali hapa.

Maana hata daktari wa kibinadamu tu akiwa na ujuzi kwamba mama mjamzito akinywa dawa hii wakati ana mimba itamsababishia azae mtoto mwenye kilema, halafu asipozuia mama kunywa dawa ile, tutamuona huyu daktari ni kama mnyama.

Sasa inakuwaje mungu mwenye uwezo wote na upendo wote aachie watoto wadogo wasio na hatia wazaliwe na vilema halafu tuendelee kumtukuza kwamba ana mapenzi makuu?

Mungu gani huyu ambaye hana hata ethics ndogo tu za kibinadamu?
 
Shauri yako ukienda huko ukamkuta sijui utamjibu nini
 
kama unaamini upepo upo pasipo kuuona...unashindwa nini kuamini kuwa mungu yupo pasipo kumuona?

Upepo unapimika kwa mwendokasi wake, muelekeo wake etc.

Mungu hata haelezeki, achilia mbali kupimika.

Kama kuna mungu muweza yote na mwenye mapenzi ya juu kabisa, kwa nini kaumba ulimwengu ambao uovu na ubaya unawezekana?
 
Shauri yako ukienda huko ukamkuta sijui utamjibu nini

Wewe ushaenda huko na kumkuta?

Na kama unataka kuamini tu ili ku satisfy "Pascal's wager" utajuaje kwamba utakayemchagua wewe ndiye mungu sahihi wakati kuna mamilioni ya miungu?
 
upepo hauonekani lakini ni kitu unachoweza kuhisi na kusikia ila uwepo wa mungu ni jambo la kufikirika zaidi

hata mungu unaweza kuhisi uwepo wake ziadi hata ilivyo upepo nenda kasome vitabu vya dini kama utoona unatembea na mungu popote ulipo...najua sayansi inawadanganya kuwa tulikuwa nyani
 
Wewe ushaenda huko na kumkuta?

Na kama unataka kuamini tu ili ku satisfy "Pascal's wager" utajuaje kwamba utakayemchagua wewe ndiye mungu sahihi wakati kuna mamilioni ya miungu?

kumbe wewe ushaenda hukumkuta?wewe muabudu mungu yoyote maana mungu ni mmoja tu
 
Mimi nishaweka "the problem of evil" hapa kama swali, na sijajibiwa.

Kuwapo kwa maovu duniani ni moja kati ya shahidi za kutokuwapo kwa mungu mwenye upendo mkuu na uwezo mkuu.

Una maana Mungu yupo ila hana upendo wala upendo??

Kama mungu ana uwezo mkuu, uwezo wa kuumba ulimwengu wa aina yoyote, hata usio na maovu (usiowezekanika kufanyika maovu kama vile wewe usivyoweza kupaa angani bila msaada wa vifaa) kwa nini hakuuumba ulimwengu wetu uwe hivyo?

Mungu kampa kila mtu uhuru wa kuamua
ili mwisho mje kusadiki kuwa hukumu zake ni za kweli na haki

Kama alikuwa na uwezo nini kilimzuia? Alikuwa hajali tu?

Uwezo anao bali kampa binadamu uhuru wa kuamua
kwani binadamu anajua mema na mabaya

Lakini tunaambiwa na upendo usio kifani, kwa hiyo alitupenda waja wake.

John 3:16
Sasa kilichomzuia kuumba ulimwengu ambao hauna njaa, matetemeko ya ardhi, magonjwa, dhoruba, kifo, watoto kuzaliwa na vilema etc ni nini?

Hayo yote ni matokeo ya zambi

Ina maana alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu usio na maovu lakini hakutaka tu?

Kabla ya dhambi ulimwengu ulikuwa hauna ovu lolote

Kama kafanya hivyo tutasemaje kwamba ana mapenzi makuu?

John 3:16

Hata baba wa kibinadamu akiwa na uwezo wa kuwapa good time wanawe halafu akawaacha waugue, wapate njaa tutamuona mbaya, hatutasema ana upendo.

John 3:16

Si zaidi kwa mungu ambaye anatakiwa kuwa muweza wa vyote na mwenye mapenzi yasiyo kifani?

Kweli huyu mungu yupo au stories tu?

Kuwepo kwa uovu ni dhahiri shahiri kuwa Mungu ana upendo wa Agape

Kama yupo mbona kaumba ulimwengu wenye maovu kibao?

Unarudia rudia swali hilo hilo huna jingine?

Hili ndilo swali hapa.

Maana hata daktari wa kibinadamu tu akiwa na ujuzi kwamba mama mjamzito akinywa dawa hii wakati ana mimba itamsababishia azae mtoto mwenye kilema, halafu asipozuia mama kunywa dawa ile, tutamuona huyu daktari ni kama mnyama.

Sasa inakuwaje mungu mwenye uwezo wote na upendo wote aachie watoto wadogo wasio na hatia wazaliwe na vilema halafu tuendelee kumtukuza kwamba ana mapenzi makuu?

Mungu ni Upendo

Mungu gani huyu ambaye hana hata ethics ndogo tu za kibinadamu?

unataka kumlinganisha Mungu na binadamu?
 
inaonekana uoga wako ndio mungu wako.

Very well put. Wengine wanaamini mungu kwa sababu ya uoga tu.

Ni kama wale watu waliokuwa wanaamini dunia ni bapa, na ukienda mbali sana baharini na meli utaanguka nje ya dunia.

Wakaja kina Columbus na Magellan kutuonesha kwamba dunia ni duara.

Kama na wao wangeogopa mpaka leo watu wa Afrika na Ulaya wangekuwa hawajafika Marekani.
 
Back
Top Bottom