Laiti Jakaya angekua anazingatia JF.......!!

Tumaini Jipya

JF-Expert Member
Jan 25, 2011
379
125
Nawasabahi wana JF katika Jina La Mageuzi!!
Mimi sina muda Mrefu tangu nijiunge na Jukwaa hili ambao Wanachama wake wengi(si wote) wanao uwezo wa kipekee kabisa wa Kufikiri,hawa ndiyo wale Watanzania wachache ambao NJAA na DHIKI iliyosababishwa na Ccm havijajeruhi uwezo wao Kufikiri!! Wana uwezo wa kukusikia na kukuelewa si tu kutoka kwenye maneno unayoyasema lakini zaidi sana kutoka katika maneno tusiyoyatamka!!
Katika kipindi kifupi nilichokuwa Mwanajamii wa Forum hii nimeshuhudia Michango ya Mawazo mizito na iliyosheheni nyama hasa katika Jukwaa hili la Siasa na Biashara!!
Nilichogundua tu hata waliowengi ambao huwa wanaandika "crap" hawasukumwi kufanya kutoka katika uwezo mdogo kichwani bali desturi tu ya kuchagua "the easy way" wakidhani kufanya hivyo kutawawezesha kuendelea kuweka "Sahani" mezani!!
I have been profoundly blessed by the contributions of many great thinkers in ths Forum,Big Up ladies and Gentleman!!

In light of ths,kama Jakaya angekuwa anafuatilia michango ya mawazo ya watu WanaJamvi hapa bila shaka angekuwa ana haja ya wale wanoitwa "washauri" wa Rais!! Jf ni zaidi ya Mshauri,unahitaji kuondoa "Pumba" chache zingine zote points tu!!!

Jakaya pay frequent Visits to ths Forum,hautotoka kapa,Ths is the home of people with Fine Minds!!
 
...*Nilichogundua tu hata waliowengi ambao huwa wanaandika "crap" hawasukumwi kufanya kutoka katika uwezo mdogo kichwani bali desturi tu ya kuchagua "the easy way" wakidhani kufanya hivyo kutawawezesha kuendelea kuweka "Sahani" mezani!! ...

Swali.. ! Unafikiri Watanzania asilimia ngapi hafanyi MATENDO ya hao wanaondika CRAP ? *Pili, Unafikiri KIONGOZI gani amepona huo ugonjwa wa hao wanaondika CRAP*

Swali la msingi zaidi ... Kweli Hapa Tanzania kwa sasa ..... the easy way .... HAILIPI? au tuseme Imeshamdhuru mtu yeyote?
 
Hujaeleweka,plz weka kiswahili muzuri!
 
Tumaini Jipya,
Karibu sana mkuu wangu, labda nikwambie tu kutoka upande wa pili ktk wigo la fikra huru!
Hivi wewe unafikiri kwa nini JK hazingatii ya JF? ni sababu zipi haswa maanake sisi wote hapa tumekuwa tukiandika mengi sana lakini kama ulivyosema hayafuatwi wala kuzingatiwa..

Binafsi yangu nimefikia kuamini kwamba pengine tunajaribu kutibu kisichotibika.. gonjwa la maambukizi na hautibiki na JK mwenye anajua fika kwamba ni muathirika hivyo unapozungumzia dawa ya tiba pamoja na kuwepo ukweli inatibu maradhi fulani lakini makosa ni pale mnapotegemea muathirika kutoa huduma hiyo ama kumpiga vita mgonjwa mwenyewe ambaye pia ni victim wa gonjwa hilo.

UFISADI kama UKIMWI - Mathlan JK ni muathirika ktk janga la Ufisadi, Je, inakuwaje sisi tunamhitaji yeye awe mstari wa mbele kupiga vita waathirika? Hivi kweli yawezekana mgonjwa wa HIV anaweza kusimama na kutangaza vita dhidi ya waathirika ilihali yeye mwenyewe ni muathirika!. Kama haiwezekani basi yawezekana nasi tunaelekeza mapambano yetu kusikofaa!

Kwa maana hiyo, hapa JF tumekuwa tukitazama upande wa kupambana na Mafisadi badala ya kuweka nguvu zetu kupambana na virusi vya Ufisadi..wananchi wenyewe wanaenezana gonjwa hili kila kona ya uzalishaji wakidai bora maisha mafupi matamu kuliko maisha marefu ya umaskini. Ni mawazo yaleyale tunayakuta ktk baadhi ya watu wasiojali maambukizi ya Ukimwi na wako radhi kutembea na bwana/Binti mwenye Ukimwi kwa ashiki zao za kimaisha. Na ngono sii haramu kwa wana ndoa isipokuwa haramu inakuja ktk maambukizi na tunapokosa trust baina yetu (uzinifu), vile vile Utajiri sii haramu isipokuwa pale tunapokiuka misnigi ya kujipatia utajiri kwa haki na sii njia za ulafi kama Ufisadi.

Mambo mengine makubwa tulozungumzia hapa ni jinsi ya kukuza uchumi wetu lakini jamani AFYA yetu kiuchumi mbovu sana na imetokana na gonjwa hili la Ufisadi. Kwa nini sisi wenyewe tusipige vita maambukizi, tusikubali kurubuniwa na tufanye shughuli zetu kwa kufuata sheria na kinga dhidi maambukizi ya gonjwa hili la Ufisadi..Na kama nilivyosema siku zote, hatuwezi kujaza maji ktk ndoo ilotoboka tutakesha miaka na miaka ndoo haitaweza kujaa..Huyo JK anaweza vipi yeye binafsi kuziba tobo hizi pasipo sisi wananchi wenyewe kuchukua jukumu la kupambana na Ufisadi.

Nijuavyo mimi vita ya Ukimwi haifanywi na muathirika bali hufanya na wananchi walio na afya bora kwa kujikinga wao wenyewe kwanza, kujihadhari na na vitendo vyovyote vya maambukizi halafu waathirika hupewa dawa zao na kuwekwa ktk sehemu wanazoweza kupata huduma na kwa wale wanaoambukiza kwa makusudi ndio tunawapeleka mbele ya sheria lakini hizi siasa za kupambana na Mafisadi hali tunauzsau Ufisadi wenyewe kama ndio adui yetu nadhani tunafanya makosa makubwa...

Hali halisi iliyopo leo Tanzania hata akija nani hatuwezi kufanikiwa bila sisi wenyewe kurekebisha mienendo yetu ktk kupambana na Ufisadi. Utamwamini nani Tanzania ya leo kwamba mzalendo hawezi kutoa ama kuchukua rushwa. Nilikuwa Bongo miezi tu ilopita nilishindwa kuishi ktk mazingira ya rushwa niloyakuta. Nilishindwa kufanya jambo hata moja la maana kutokana na watu walivyokuwa waongo, wanafiki na majambazi wa nafsi za watu. Hakuna mkweli, ndugu, rafiki wala ushirikiano na maajabu watu wanashangaa na Udini uloingia nchini lakini haya ndio matunda ya dhanaishi ya Watanzania ambao ni - IGNORANT, GREED and SELFISH..
 
alivyo mwoga na mvivu wa kusoma yule hawezi kuingia hapa..........kwani hujui kama tuna raisi mvivu wa kila kitu.......

hivi kwanza niulize kikwete alishawa wahi kuandika kitabu chake juu ya jambo lolote la maendeleo kama alivyokuwa mwalimu??

yule jamaa ni mvivu sana na ndio...
 
Mkuu Mkandara,

Sasa ni wakati wa kubadili mwelekeo wa Vita vya ufisadi. Kujikimbia na kuulekeza Vidole kwa waote isipokuwa mimi ..hiyo iwe impitwa na wakati. Nadhani Mkuu TJ atakuwa sasa ananielewa ni kisema ninani amabaye ni msafi ...asiyependa easy way ...ambao ndio nguzo na mbegu ya Ufisadi.

Na Mkuu , haya maneno .. IGNORANT, GREED and SELFISH ... yanatisha ...!!
 
Back
Top Bottom