Lady Jaydee: Naamka tena baada ya siku 30

warumi

R I P
May 6, 2013
16,273
18,422
Mkongwe wa muziki wa bongo fleva Lady Jaydee ametangaza rasmi kurudi tena kwenye muziki baada ya ukimya wa muda kidogo kwenye muziki. Lady Jaydee ameweka wazi ujio wake mpya kwenye muziki baada ya siku 30 kuanzia leo.

Wiki kadhaa zilizopita Lady Jaydee aliwahi kuwaomba wapenzi wa muziki wake kuwa wavumilivu na kuwataka wasubiri kwani kwa kipindi hicho alikiri wazi kuwa hana kitu cha kuimba wala hakuwa na mizuka ya kuimba, kutokana na mambo yake ya hapa na pale na kuwataka wapenzi wake kwenye muziki kudumisha amani.

“Karibu tu lakini sina lolote kwa sasa, sina kabisa na sitakuwa nalo kwa kipindi kirefu sana, yaani sina, sina, sina. wapenzi huvuta subira mashabiki huhama hama. Wapenzi vuteni subira na dumisheni amani” Aliandika Lady Jaydee.

Baada ya ukimya na mashabiki kuanza kuhoji juu ya ukimya wake kwenye muziki, mwanadada Lady Jaydee alikuja na kuweka wazi kuwa amekuwa kimya lakini hawezi kufanya lolote sababu hakuwa na jambo la kusema au kuimba kwa wakati huo na kuwataka tena mashabiki na wapenzi wa muziki wake kuwa wavumilivu.

“Ni kweli sijasema ,ni kweli nimekaa kimya lakini siwezi sema tu endapo sina cha kusema mnaweza kuvumilia? Kama ninavyo vumilia? Napumzika tu sina cha kufanya mvumilie nitarudi sema sina cha kusema na siko tayari kusema, nitasema nikiwa tayari kusema” Alimaliza Lady Jaydee.

Lady Jaydee sasa amepata cha kusema na amepata ya kuzungumza na ndio maana ametangaza rasmi ujio wake mpya kwenye muziki wa bongo fleva, Jide amesema kuwa baada ya siku 30 kuanzia leo atasimama tena.
 
Attachments

  • 1455894991977.jpg
    1455894991977.jpg
    70 KB · Views: 49
Ajipange muziki umevua nguo haumueshimu mtu tu ni msobemsobe mbwa kamla mbwa ni mwendo wa fitina usije ukaanza vilio tu na watu wanajua kutofautisha kwaya na R n' B naona majabali wenzako wako pembeni wanapima kina kwa vijiti maana wadogo zenu hawana adabu,karibu Judith kipimo cha ubora siku hizi ni video uka-shoot SA,video ichezwe Trace,MTV,Sound City and the like.
 
Uzuri wa jay Dee watu wala huwa hawahitaji video ili wakubali kazi zake. . Trust me, hata asipotoa video atahit sana tu......Jay Dee ni mashine nyingine kwa Tz hakuna
 
Ajipange muziki umevua nguo haumueshimu mtu tu ni msobemsobe mbwa kamla mbwa ni mwendo wa fitina usije ukaanza vilio tu na watu wanajua kutofautisha kwaya na R n' B naona majabali wenzako wako pembeni wanapima kina kwa vijiti maana wadogo zenu hawana adabu,karibu Judith kipimo cha ubora siku hizi ni video uka-shoot SA,video ichezwe Trace,MTV,Sound City and the like.

jide na Ay walishaanza kushoot video south kabla ya diamond na video zao zilishapigwa vituo vya nje sana , hata ngoma yake ya mwisho na DJ mazet sijui niliona video inapigwa MTV base
Nakuunga mkono akaze zaidi lakini kwenye video na kushoot SA anauzoefu wa kutosha
 
Back
Top Bottom