Lady Jaydee: Clouds FM ni wanafiki, wanataka wahongwe ili wapige nyimbo za wasanii

Hawa wasanii wakubwa tabu sana na wanajiua wenyewe! Kipindi Sugu anapambana walimtenga akaishia kuungana na vijana wadogo kama Dan Msimamo na wengine kama sisi tukasimama kidete kupitia hapa JF hadi kubadili upepo na chuki dhidi ya Mawingu kuhamia mtaani kwa kasi!!!
Clouds wakigombana na wewe wanamtafuta msanii kama wewe wanahakikisha anarudi kwenye chati na anatumika kutukana wenzake!!
Wasanii kwa upumbavu wenu na dharau ngoja cha moto mkione ndio mjifunze kuwa wamoja.
 
Ah kumbe hayo yapo

Huenda kuna bifu kati yao, wanataka kujumuisha na wengine

Yetu macho bana, let us wait and see
 
Hawa wasanii wa bongo mi nawaita wajinga kwa sababu wao ndio wanafiki na wataendelea kuburuzwa na hao clouds mpaka mwisho wa dunia, unafiki wa kwanza ni kutoziamini/kudharau redio nyingine na kuona kuwa nyimbo zao haziwezi ku hit mpaka zipigwe na clouds. Na unafiki wa wao kwa wao wasanii ambao wanatukuzwa na kupambwa kijinga na clouds kwa nia ya kuibiwa wanawatenga wasanii wengine wanajiona wao ndio wao lakini wakibwagwa ndio wanalalamika na kutaka msaada(ndio yaliyomkuta jay dee) ushauri wangu kwa wasanii jikazeni lenu liwe 1 unganeni kiukweli sio kinafiki, mtakuwa matajiri wa kubwa na hamtolalamika ovyo. Maana kwa unafiki wao ndio unawasumbua

Alikuwa wapi enzi vinega wanakinukisha? Aanzishe kinega yake pia.

Afterall Clouds FM sio public radio, ni private.
 
jide achana na clouds fm kwani wasipopiga nyimbo zako unapoteza nini? halafu ondoeno imani potofu iliyo mioyoni mwenu kuwa wimbo hauwezi kuhit mpaka uwe unapigwa clouds? wapotezeeni bhanaa
 
LADY JAY DEE: CLOUDS FM NI WANAFIKI, WANATAKA WAHONGWE ILI WAPIGE NYIMBO ZA WASANII

Mwanamziki nguli wa Bongofleva, Lady Jay Dee ameamua kuwapa madongo Clouds FM kupitia Twitter leo kutokana na wimbo wake mpya uliotoka hivi karibuni Joto hasira kutopigwa katika radio hiyo. Jay Dee ameandika kuwa radio ya watu isiyopiga nyimbo za wasanii wa watu ila wasanii wao tu.
>> Angalia tweet za Queen of Bongofleva huyo pichani
Jay Dee pia anaonekana kujizatiti na kujiamini kuonyesha kuwa yupo kwa lolote yeye kama Komandoo Binti Machozi aliandika tena "Kill me if u can. Am on Fire, siogopi ng'oooooo Jipangeni, Ni kweli nimelamba sumu, lakini hainidhulu. Nakunywa maziwa daily, I will survive".

Hata hivyo si Jay Dee pekee kuanza kulaumu kwani wapo wanamuziki wengine wanaolaumu nyimbo zao kutokupigwa hasa Mr II aka Sugu

578053_452019121541333_147761534_n.png

Alikuwa Wapi wkt kina Sugu, Inspektah wanalalamika? Leo kimegeuka u want us to sympathize with u...? U reap what u sow mommy!
 
Jay dee amefulia alikuwa zamani nyimbo yake haina ubora hata chembe inapigwa sababu ya ukongwe wake tu
 
Si katangaza pale pale na mume akampata... na ndio walikuwa wanamganda kwa zamu leo anakuja nakutubania pua nyooooooooo.... Kijinga sana hiki kidem..
 
East African popular musician Lady Jay Dee ameamua kuwapa modongo Clouds fm kupitia Twitter leo kutokana na wimbo wake mpya uliotoka hivi karibuni Joto hasira kutopigwa katika radio hiyo. Jay dee ameandika kuwa radio ya watu isiyopiga nyimbo za wasanii wa watu ila wasanii wao tu. Angalia tweet za Queen of Bongofleva huyo.
“Radio ya watu isiopiga nyimbo za wasanii wa watu ila za wasanii wao tu, wasiopendwa na watu. #JotoHasira ”

” Anaedai kuianzisha bongoflava aliapa kuiua bongo flava. Sasa hata wasioijua Hiphop nao wana beef na Bongo flava! Damn !!”
Jay Dee pia anaonekana kujizatiti na kujiamini kuonyesha kuwa yupo kwa lolote yeye kama Komandoo Binti Machozi aliandika tena “Kill me if u can. Am on Fire, siogopi ng’oooooo Jipangeni, Ni kweli nimelamba sumu, lakini hainidhulu. Nakunywa maziwa daily, I will survive”…….more info please follow the link: FAHARI YA KUSINI MWA TANZANIA: JAY DEE AWAVULIA UVIVU REDIO YA WATU "CLOUDS FM"

Lady JayDee @JideJaydee Radio ya watu isiopiga nyimbo za wasanii wa watu ila za wasanii wao tu, wasiopendwa na watu. #JotoHasira
12:53 AM - 30 Mar 13
 
Hivi haijawahi kusemekana kwamba aliwahi kumpa Ruge kule South Africa?
 
Sasa zile kwaya anazoimba nani anataka kusikia...???? Watu wamejipanga wamemkalia juu anahaha kutafuta mlango wa kutokea heheheheeeee.... jitahidi kuomba mungu akupe mtoto walau mmoja ulee mama.. huu muziki unaung'ang'ania ila wenyewe haukutaki... nilikukubali way back not now adayz hata ningekuwa mimi dj au presenter nisingecheza ngoma zako.. hauvutii kusikilizwa Mama.
Ni lazima utakuwa miongoni mwa wale wanaotafutwa na dr Manyau nyau!Unatema nyongo as if wewe ndo clouds!


Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Jay dee amefulia alikuwa zamani nyimbo yake haina ubora hata chembe inapigwa sababu ya ukongwe wake tu
Walewale wapenzi wa nataka kulewa. Jaydee ni Mwanamuziki halisi kwa sababu anatumbuiza na Live band na siyo hao masharobaro wenu wanaoweka CD na kuimba playback. (Computer artist ).
 
Hawapigi tena track redioni, na hata kwenye TV hamnioni, na jina haliendi chini.

Najua mnashangaa hata mi Sijui kwa nini?

Mabitozi na mark ii mikwara tu hawana kitu kiwese geji ipo chini ndio maana vioo chini
 
Back
Top Bottom