Poleni na majukumu ya kila leo mashostito pale tunapokuwa na jambo lazima kushare pamoja
Leo nina jambo kidogo la kushare kwa sisi ambao tunashikilia Gurudumu la ndoa mambo machache ya kukumbushana na kuelekezana,
Kumekuwa na kasumba ya kina mama wakiwa saloon au popote kwenye mikusanyiko ya kina mama ,kina dada wengi utamsikia mtu ooh mme wangu ni mwaminifu ooh mme wangu saa kumi na mbili tu yuko ndani , ananipenda na hacheat na mengineyo mengi wakati wenzio ukigeuza tu kisogo wanakucheka na kusema things happen.
Cha msingi kama unaona hilo na kujua hivyo piga goti na umshukuru mungu kwa hilo,wala usifungue mdomo kujisifia Mbele za watu .
Mifano hai,
1.Kuna dada mmewe akiwa nyumbani kwake anajali watoto ,anamjali mke,Kusoma neno la mungu na kuongoza misa ya family ni mtu ambae ukimuona utasema yes mme ninae hasa hata kumdolishia kwa watu,Lakini upande mwingine wa shilingi ambao mkewe hajui na ni mke ambae mambo ya outing ,socialization kwake hayapo ,michepuko kwa mmewe ile ya underground ni namba 1,so mkewe akiwa sehemu kwenye vikao vya kparty au walipo wanawake anajisifia watu wanasikiliza tu kwa vile walioko nje wanamjua huyu shemeji sema wanashindwa kumwambia na hawawezi kuhofia kuleta hitilafu kwenye ndoa .INATISHA
2. Jmos nikiwa Saloon kuna warembo fulani walikuwa wanapiga story zao eti ooh huyu dada akija hapa nikujisifia mme wangu mme wangu hajui kama mmewe tunakula nae sahani moja,Kumbe mmoja wa wale akina dada anatoka na huyo jamaa yuko Bank moja,na ili kuthibitisha hilo akamcall jamaa wakaahidiana akitoka saloon atapita pale amchukue waende wanapojua..VERY BAD
3.Kubwa kuliko hii niliikuta duka la nguo za kina mama kuna wadada wamepeana kazi ya kumtafuta mme wa dada mmoja kwa udi na uvumba wanasema lazima wampate hii wamepeana task kabisa mmoja akishindwa kumpata lazima mwingine ampate ,hivyo wameweka mbinu na mikakati ya kumpata huyo jamaa ,
Ni jamaa ambae eti wanadai lazima aende hapo dukani kumfanyia mkewe shopping ya nguo na sokoni sometimez anaenda yeye kufanya manunuzi ya ndani
wanadai pia mke wake ni mzuri lakini mshamba,
Pia wanadai jamaa ni Handsome na ana mshiko wa uhakika-lazima waende nae sambamba
Duh tunaenda wapi kumbe waume zetu wanatafutwa :A S 11:
Haya kina mama tunaopenda kusifia waume zetu mbele za mabinti /kinadadaa mara ooh nikiwa mjamzito ananipikia anapapasa kitumbo ananiogesha - wapo wanaowapigia speed huko
Kina mama mnaotoa siri za ndani hizo ndio silaha za kutumaliza :flame:
Mwisho kabisa wanasema sie wachoyo kwanini kula peke yetu - Tukumbuke kuziombea ndoa zetu majaribu ni meeeengi sana.
Muwe na Ijumaa njema:couch2:
Haya ngoja wenye ndoa waje kwanza
hakika tuwe tunaombea familia
sasa unasubiri nini kuolewa ??
Siwezi kujisifu nina mume bora au bf bora ... hawa viumbe hubadilika mara ... kama kama kuchanganya maji na rangi nyekundu acha kabisa....... akiwa mzuri tumia hiyo nafasi vizuri jua ubaya unakuja...
Ni kweli, si kila jambo la kusema hadharani, lakini mi naona nyumba ndogo tumezipa umuhimu kuliko zilizo nao.
Huyo dada kama anamsifia mumewe kutoka rohoni ni haki yake, sasa aogope kisa mwizi wake yuko pale, tena wala hamjui? Bora hata mume angekuwa ameitambulisha nyumba ndogo yake kwa mkewe, ningesema ana uzito fulani kwa muwe.
Anyway, ni mtizamo tu(he he he, japo huwa si mtu wa kujisifia iwe ninacho ama sina), but ningekuwa mtu wa matangazo na masifa, ningesifia hata kama najua ni kit.ombi. Binadamu anaweza kuwa na baya 1, akawa na mazuri 9, ya nini niyazike mazuri 9 kwa baya 1?
Labda kweli huyo dada mumewe anamsaidia kukata vitunguu, wangapi hapa tunasaidiwa vitunguu? Akiingia jikoni ni aidha kwa maelekezo ya mganga ama mke uko kwenye ambulensi. Sometimes if you have it, brag it, kama haikusumbui.
Mie kwa kwa kweli kelele za chura hazitanizuia kumsifia zombie, niibe nijifiche kusifia, mume naye niogope kumsifia kisa kuna pyschos wanataka kumkwiba kwa kunikomoa nisijisifie? Wamkwibe tu, tena akiwa zuzu wambebe mazima.
As long as mume anarudi home, am at peace na nitamsifia hadi nitakapoona otherwise.
Kuna workmate wangu pia alinishangaza, anaishi Sinza. Alinisimulia jinsi wanavyopanga kumwibia shost yao mume kisa anajisifia sana. Nikamuuliza, mkishamuiba mnapanga na kuivunja hiyo ndoa, wakasema hapana, tunamkomesha tu afunge mdogo. Kweli nilimuona ni pyscho tu. Kumkoa mke wa ndoa wa mtu mtu ni sawa na kuikomoa serikali, haikomoleki. Sema tu hili gonjwa ndio balaa.
Kwanza ukiona wanawake wanafuata mumeo, jua ulichagua aliyenona, na inafanya ndoa kuwa more exciting.
Hahahaa
Bado miezi michache tu na mi niingie humo ndani
Hivi mimi NK kabisa nikapige story na wadada salon...?
Kunangwa kwingine ni kwa kujitakia...
(Know your class)
Na ukute hata mumewe hawamjui...
Ila kwa kuwa kajisifia wanataka kumrusha roho tu...
Mimi huwa sitaki hata zile service za kufuatana home...
Nyumbani kwangu si pa kila mtu kuingia na kutoka kama chooni...
Poleni na majukumu ya kila leo mashostito pale tunapokuwa na jambo lazima kushare pamoja
Leo nina jambo kidogo la kushare kwa sisi ambao tunashikilia Gurudumu la ndoa mambo machache ya kukumbushana na kuelekezana,
Kumekuwa na kasumba ya kina mama wakiwa saloon au popote kwenye mikusanyiko ya kina mama ,kina dada wengi utamsikia mtu ooh mme wangu ni mwaminifu ooh mme wangu saa kumi na mbili tu yuko ndani , ananipenda na hacheat na mengineyo mengi wakati wenzio ukigeuza tu kisogo wanakucheka na kusema things happen.
Cha msingi kama unaona hilo na kujua hivyo piga goti na umshukuru mungu kwa hilo,wala usifungue mdomo kujisifia Mbele za watu .
Mifano hai,
1.Kuna dada mmewe akiwa nyumbani kwake anajali watoto ,anamjali mke,Kusoma neno la mungu na kuongoza misa ya family ni mtu ambae ukimuona utasema yes mme ninae hasa hata kumdolishia kwa watu,Lakini upande mwingine wa shilingi ambao mkewe hajui na ni mke ambae mambo ya outing ,socialization kwake hayapo ,michepuko kwa mmewe ile ya underground ni namba 1,so mkewe akiwa sehemu kwenye vikao vya kparty au walipo wanawake anajisifia watu wanasikiliza tu kwa vile walioko nje wanamjua huyu shemeji sema wanashindwa kumwambia na hawawezi kuhofia kuleta hitilafu kwenye ndoa .INATISHA
2. Jmos nikiwa Saloon kuna warembo fulani walikuwa wanapiga story zao eti ooh huyu dada akija hapa nikujisifia mme wangu mme wangu hajui kama mmewe tunakula nae sahani moja,Kumbe mmoja wa wale akina dada anatoka na huyo jamaa yuko Bank moja,na ili kuthibitisha hilo akamcall jamaa wakaahidiana akitoka saloon atapita pale amchukue waende wanapojua..VERY BAD
3.Kubwa kuliko hii niliikuta duka la nguo za kina mama kuna wadada wamepeana kazi ya kumtafuta mme wa dada mmoja kwa udi na uvumba wanasema lazima wampate hii wamepeana task kabisa mmoja akishindwa kumpata lazima mwingine ampate ,hivyo wameweka mbinu na mikakati ya kumpata huyo jamaa ,
Ni jamaa ambae eti wanadai lazima aende hapo dukani kumfanyia mkewe shopping ya nguo na sokoni sometimez anaenda yeye kufanya manunuzi ya ndani
wanadai pia mke wake ni mzuri lakini mshamba,
Pia wanadai jamaa ni Handsome na ana mshiko wa uhakika-lazima waende nae sambamba
Duh tunaenda wapi kumbe waume zetu wanatafutwa :A S 11:
Haya kina mama tunaopenda kusifia waume zetu mbele za mabinti /kinadadaa mara ooh nikiwa mjamzito ananipikia anapapasa kitumbo ananiogesha - wapo wanaowapigia speed huko
Kina mama mnaotoa siri za ndani hizo ndio silaha za kutumaliza :flame:
Mwisho kabisa wanasema sie wachoyo kwanini kula peke yetu - Tukumbuke kuziombea ndoa zetu majaribu ni meeeengi sana.
Muwe na Ijumaa njema:couch2:
mie mbona siwaonag waingie 18 zangu? mpenz/mume wangu majidai naee kwa raha zng mtu ajilete atantambua