Ladies ndani ya ndoa piteni hapa

Ladies ndani ya ndoa piteni hapa

Moyo wa mtu ni fumbo kwa wengine!!

kuna jirani yangu hapa alikuwa anamsifia sana mumewe yuko hivi mara yuko vile, wao wanamiliki Lodge picha linaanza wafanyakazi wa lodge wanagombana wao kwa wao kisa huyo mume kumbe kawapitia wote,

Mke kapewa taarifa kawatimua wote sasa hivi hadi anaona aibu sababu mtaa mzima umejua yuko kimyaaa!!

Haina maana yoyote kumsifia mume labda pale panapostahili na inategemea mko kwenye mazingira gani na watu wa aina gani!!

Angalizo angalia aina ya marafiki ulionao wakoje, wana muelekeo gani! si kila mtu anafaa kuwa rafiki na kuna saloon zingine hazifai kbsa kwenda kwa mtu anayejitambua!!
 
Poleni na majukumu ya kila leo mashostito pale tunapokuwa na jambo lazima kushare pamoja

Leo nina jambo kidogo la kushare kwa sisi ambao tunashikilia Gurudumu la ndoa mambo machache ya kukumbushana na kuelekezana,

Kumekuwa na kasumba ya kina mama wakiwa saloon au popote kwenye mikusanyiko ya kina mama ,kina dada wengi utamsikia mtu ooh mme wangu ni mwaminifu ooh mme wangu saa kumi na mbili tu yuko ndani , ananipenda na hacheat na mengineyo mengi wakati wenzio ukigeuza tu kisogo wanakucheka na kusema things happen.
Cha msingi kama unaona hilo na kujua hivyo piga goti na umshukuru mungu kwa hilo,wala usifungue mdomo kujisifia Mbele za watu .
Mifano hai,

1.Kuna dada mmewe akiwa nyumbani kwake anajali watoto ,anamjali mke,Kusoma neno la mungu na kuongoza misa ya family ni mtu ambae ukimuona utasema yes mme ninae hasa hata kumdolishia kwa watu,Lakini upande mwingine wa shilingi ambao mkewe hajui na ni mke ambae mambo ya outing ,socialization kwake hayapo ,michepuko kwa mmewe ile ya underground ni namba 1,so mkewe akiwa sehemu kwenye vikao vya kparty au walipo wanawake anajisifia watu wanasikiliza tu kwa vile walioko nje wanamjua huyu shemeji sema wanashindwa kumwambia na hawawezi kuhofia kuleta hitilafu kwenye ndoa .INATISHA

2. Jmos nikiwa Saloon kuna warembo fulani walikuwa wanapiga story zao eti ooh huyu dada akija hapa nikujisifia mme wangu mme wangu hajui kama mmewe tunakula nae sahani moja,Kumbe mmoja wa wale akina dada anatoka na huyo jamaa yuko Bank moja,na ili kuthibitisha hilo akamcall jamaa wakaahidiana akitoka saloon atapita pale amchukue waende wanapojua..VERY BAD

3.Kubwa kuliko hii niliikuta duka la nguo za kina mama kuna wadada wamepeana kazi ya kumtafuta mme wa dada mmoja kwa udi na uvumba wanasema lazima wampate hii wamepeana task kabisa mmoja akishindwa kumpata lazima mwingine ampate ,hivyo wameweka mbinu na mikakati ya kumpata huyo jamaa ,
Ni jamaa ambae eti wanadai lazima aende hapo dukani kumfanyia mkewe shopping ya nguo na sokoni sometimez anaenda yeye kufanya manunuzi ya ndani
wanadai pia mke wake ni mzuri lakini mshamba,
Pia wanadai jamaa ni Handsome na ana mshiko wa uhakika-lazima waende nae sambamba

Duh tunaenda wapi kumbe waume zetu wanatafutwa :A S 11:

Haya kina mama tunaopenda kusifia waume zetu mbele za mabinti /kinadadaa mara ooh nikiwa mjamzito ananipikia anapapasa kitumbo ananiogesha - wapo wanaowapigia speed huko

Kina mama mnaotoa siri za ndani hizo ndio silaha za kutumaliza :flame:

Mwisho kabisa wanasema sie wachoyo kwanini kula peke yetu - Tukumbuke kuziombea ndoa zetu majaribu ni meeeengi sana.

Muwe na Ijumaa njema:couch2:

Very mature advice
 
Moyo wa mtu ni sawa na kichaka huwezi jua ndani yake kunani, nyoka, chatu ama nini tena masalon ndo wamama wenye ndoa wanapo ongea mambo ya ndoa zao .
What the hell it's better to shut your bowl off maana waweza kuwa wajichoresha tu
hizi salon na makundi makundi haya yana mambo kwa kweli
 
ni mbaya sana kumsifiaa au kumponda mume kwa maana dunia ya sasa sio

tuwe na kifua cha kutunza siri
 
Rule no 1: ndoa ni wawili marufuku kusimulia kuhusu mume wangu si saluni, si kwenye biashara wala popote

Rule no 2: maswala ya mahaba kati yangu na mume ni marufuku kusimulia

Rule no 3: weka mbali mumeo na mashosti

Rule no 4: know your husband

Nitarudi acha nikapike
 
Siwezi kujisifu nina mume bora au bf bora ... hawa viumbe hubadilika mara ... kama kama kuchanganya maji na rangi nyekundu acha kabisa....... akiwa mzuri tumia hiyo nafasi vizuri jua ubaya unakuja...

Ukiolewa utajisifu tu kwa kuwa mume... hata kama uwa tunabadlika ila mke ni mke tu anaheshma yake special
 
Ni kweli, si kila jambo la kusema hadharani, lakini mi naona nyumba ndogo tumezipa umuhimu kuliko zilizo nao.

Huyo dada kama anamsifia mumewe kutoka rohoni ni haki yake, sasa aogope kisa mwizi wake yuko pale, tena wala hamjui? Bora hata mume angekuwa ameitambulisha nyumba ndogo yake kwa mkewe, ningesema ana uzito fulani kwa muwe.

Anyway, ni mtizamo tu(he he he, japo huwa si mtu wa kujisifia iwe ninacho ama sina), but ningekuwa mtu wa matangazo na masifa, ningesifia hata kama najua ni kit.ombi. Binadamu anaweza kuwa na baya 1, akawa na mazuri 9, ya nini niyazike mazuri 9 kwa baya 1?

Labda kweli huyo dada mumewe anamsaidia kukata vitunguu, wangapi hapa tunasaidiwa vitunguu? Akiingia jikoni ni aidha kwa maelekezo ya mganga ama mke uko kwenye ambulensi. Sometimes if you have it, brag it, kama haikusumbui.

Asante
Ndo maana nakupendaga...
Nasisitiza wanaume sio wote wabaya kitabia, kuna wengine ukiwa nao burudani tu japo maudhui ya hapa na pale yapo..
Mi kiukweli namsifia tu bt sio kila kitu cha kuongea pia ni kuangalia Place n Time....sio eti naenda kupiga story saluni ndo ndoa za watu zinaharibika huko.... nina uhakika hanicheat...maombi yangu kwa Mungu yanamlinda
 
Hivi mimi NK kabisa nikapige story na wadada salon...?
Kunangwa kwingine ni kwa kujitakia...
(Know your class)

Na ukute hata mumewe hawamjui...
Ila kwa kuwa kajisifia wanataka kumrusha roho tu...

Mimi huwa sitaki hata zile service za kufuatana home...

Nyumbani kwangu si pa kila mtu kuingia na kutoka kama chooni...
 
Mmenikumbusha mama mmoja mumewe anafanya kazi TRA...
Basi ni gumzo la salon ninayotumia...

Wakianza kumsifia wanajua hata mshahara anaompa house girl wake...
Wanajua shule wanayosoma watoto wake...

Kazi kweli kweli...

Imagine mwenye kazi ni mumewe si yeye...

Lakini ana mapozi ya kujikweza na kutafuta wapambe...

Mengi yanachangia kwa wamama kuongea ongea na kila mtu mambo binafsi...
Kubwa ni elimu...

Hao ndio wanaofukuzisha waume zao kazi...maana TRA wengi mishe mishe...
 
Mie kwa kwa kweli kelele za chura hazitanizuia kumsifia zombie, niibe nijifiche kusifia, mume naye niogope kumsifia kisa kuna pyschos wanataka kumkwiba kwa kunikomoa nisijisifie? Wamkwibe tu, tena akiwa zuzu wambebe mazima.

As long as mume anarudi home, am at peace na nitamsifia hadi nitakapoona otherwise.

Kuna workmate wangu pia alinishangaza, anaishi Sinza. Alinisimulia jinsi wanavyopanga kumwibia shost yao mume kisa anajisifia sana. Nikamuuliza, mkishamuiba mnapanga na kuivunja hiyo ndoa, wakasema hapana, tunamkomesha tu afunge mdogo. Kweli nilimuona ni pyscho tu. Kumkoa mke wa ndoa wa mtu mtu ni sawa na kuikomoa serikali, haikomoleki. Sema tu hili gonjwa ndio balaa.

Kwanza ukiona wanawake wanafuata mumeo, jua ulichagua aliyenona, na inafanya ndoa kuwa more exciting.

Simply brilliant.kongosho
 
"Kizuri kula na mwenzio"?!!,...that's the dumbest thing I've ever heard!

Lakini sisi KE nao sometimes mh!, huko kwenye vijiwe vyetu Hakunaga vingine vya kuongea zaidi ya kuwaongelea hawa wanaojifanyaga miungu wadogo?!

And then kuna sifa na sifa jamani, yaani unamtangaza mmeo kisa kakusaidia kukata nyanya, sijui kitungulu...really people?!, I think that's supposed to come with a package?!, kwa nini usimfie vitu vya maana kama kuwa promoted kazini, au kama ame seal deal moja nziito, kimaendeleo zaidi tena kwa watu wa karibu cause I think it's more persona. Lakini haya mambo ya kuwaweka KE wenzetu chini na kuanza kuwahadithi mara oh!, mume wangu ananifikisha kitonga!, halafu ananipeleka kilimanjaro, halafu anarudi kinyumenyume, halafu anakatika mpaka chini!....seriously Ladies?!
 
Hivi mimi NK kabisa nikapige story na wadada salon...?
Kunangwa kwingine ni kwa kujitakia...
(Know your class)

Na ukute hata mumewe hawamjui...
Ila kwa kuwa kajisifia wanataka kumrusha roho tu...

Mimi huwa sitaki hata zile service za kufuatana home...

Nyumbani kwangu si pa kila mtu kuingia na kutoka kama chooni...

I am.sure u know your class
I love yo mind
 
Poleni na majukumu ya kila leo mashostito pale tunapokuwa na jambo lazima kushare pamoja

Leo nina jambo kidogo la kushare kwa sisi ambao tunashikilia Gurudumu la ndoa mambo machache ya kukumbushana na kuelekezana,

Kumekuwa na kasumba ya kina mama wakiwa saloon au popote kwenye mikusanyiko ya kina mama ,kina dada wengi utamsikia mtu ooh mme wangu ni mwaminifu ooh mme wangu saa kumi na mbili tu yuko ndani , ananipenda na hacheat na mengineyo mengi wakati wenzio ukigeuza tu kisogo wanakucheka na kusema things happen.
Cha msingi kama unaona hilo na kujua hivyo piga goti na umshukuru mungu kwa hilo,wala usifungue mdomo kujisifia Mbele za watu .
Mifano hai,

1.Kuna dada mmewe akiwa nyumbani kwake anajali watoto ,anamjali mke,Kusoma neno la mungu na kuongoza misa ya family ni mtu ambae ukimuona utasema yes mme ninae hasa hata kumdolishia kwa watu,Lakini upande mwingine wa shilingi ambao mkewe hajui na ni mke ambae mambo ya outing ,socialization kwake hayapo ,michepuko kwa mmewe ile ya underground ni namba 1,so mkewe akiwa sehemu kwenye vikao vya kparty au walipo wanawake anajisifia watu wanasikiliza tu kwa vile walioko nje wanamjua huyu shemeji sema wanashindwa kumwambia na hawawezi kuhofia kuleta hitilafu kwenye ndoa .INATISHA

2. Jmos nikiwa Saloon kuna warembo fulani walikuwa wanapiga story zao eti ooh huyu dada akija hapa nikujisifia mme wangu mme wangu hajui kama mmewe tunakula nae sahani moja,Kumbe mmoja wa wale akina dada anatoka na huyo jamaa yuko Bank moja,na ili kuthibitisha hilo akamcall jamaa wakaahidiana akitoka saloon atapita pale amchukue waende wanapojua..VERY BAD

3.Kubwa kuliko hii niliikuta duka la nguo za kina mama kuna wadada wamepeana kazi ya kumtafuta mme wa dada mmoja kwa udi na uvumba wanasema lazima wampate hii wamepeana task kabisa mmoja akishindwa kumpata lazima mwingine ampate ,hivyo wameweka mbinu na mikakati ya kumpata huyo jamaa ,
Ni jamaa ambae eti wanadai lazima aende hapo dukani kumfanyia mkewe shopping ya nguo na sokoni sometimez anaenda yeye kufanya manunuzi ya ndani
wanadai pia mke wake ni mzuri lakini mshamba,
Pia wanadai jamaa ni Handsome na ana mshiko wa uhakika-lazima waende nae sambamba

Duh tunaenda wapi kumbe waume zetu wanatafutwa :A S 11:

Haya kina mama tunaopenda kusifia waume zetu mbele za mabinti /kinadadaa mara ooh nikiwa mjamzito ananipikia anapapasa kitumbo ananiogesha - wapo wanaowapigia speed huko

Kina mama mnaotoa siri za ndani hizo ndio silaha za kutumaliza :flame:

Mwisho kabisa wanasema sie wachoyo kwanini kula peke yetu - Tukumbuke kuziombea ndoa zetu majaribu ni meeeengi sana.

Muwe na Ijumaa njema:couch2:

he... kumbe umeolewa, hongera!!:third:
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom