Laana kuu Ubungo mataa!

Laana gani hiyo mkuu? Huo ni ujinga wenu wenyewe,. Kwanini ukubali kukaa kwa muda wote huo hapo mataa?

Kwako wewe ujanja ni upi, kutoka kwenye gari lako na utembee kwa miguu huku ukiliacha gari kwenye foleni barabarani?
 

Huyu anayepinga kujengwa daraja Ubungo kweli hajawahi kufika Dar
 
Mawazo yangu mimi kwa hili ni kuimalisha usafiri wa public.watu wapaki magari yao nyumbani sote tupande public transport kwenda na kurudi ma kazini..nadhn hii itasaidia..

public transport ndio kero kabisa wizi pia mtajazwa ka magunia
 
Teh teh umenikumbusha ile " Anayeona miambili ni ghali apige mbizi mpaka Kigamboni" dah! Hawa watu wanajisahau mno, nchi za watu huezi jibu upuuzi kama ule. Tena utajuta kwenye siasa uliingilia nini.
 

Pale panaudhi aisee. Kuna rafiki yangu aliwahi kusema eti ni heri uwe kwenye foleni nyuma kuliko mbele. Ukiwa mbele eti husogei! Nilicheka sana.

Nafikiri tuwe wabunifu maana situation yenyewe haionekani ku-improve siku za usoni. Muwe mnatembea na audio books msikize huko kwenye magari yenu...au msikize kwa simu etc. Acheni kuchokonoa simu kutwa...ukiwa kazini wewe na simu; ukiwa out baada ya kazi wewe na simu; kwenye usafiri wakati wa kurudi nyumbani vivyohivyo. Ni kuchat tu na kutafuta charger muda wote! Kama mnabisha fanyeni utafiti mdogo kesho kuangaoia abiria wa daladala au wadau waliojaliwa usafiri wao. Kama hawasikizi nyimbo basi wanashangaa nje. Tutumie muda ule unaokaa folenini kwa kulisha ubongo na mambo mapya.

Kila lakheri wadau
 
...loh siku moja nilikuwa huko nikaa kwenye foleni mchana mpaka usiku,kuanzia mida ya kumi na moja mpaka moja na kitu....
 
Daraja!!!!!! mhhhh hilo daraja la ubungo ..Mheshimiwa JK alisema tukimchagua yeye atajenga toka 2005 nipo school had leo kabakisha 2014.. labda ni mipango endelevu!

WaTZ tunahuziwa huduma zetu za msingi kwa kupiga KURA
 
Daraja!!!!!! mhhhh hilo daraja la ubungo ..Mheshimiwa JK alisema tukimchagua yeye atajenga toka 2005 nipo school had leo kabakisha 2014.. labda ni mipango endelevu!!
WaTZ tunahuziwa huduma zetu za msingi kwa kupiga KURA

Hakyanani litajengwa tuu mwaka huu.., wa-Japan wameshamwaga mihela nasikia..
 

Huu ni woga wa maendeleo. Hizi pesa walizochezea kujenga hizo njia za DART na hasara ya kutoa lami iliyokuwepo na kuweka nyingine katika barabara nyembamba zaidi ndio zingetumika kujenga fly overs na junctions nyingine kuchimba.
 
Hizo greda unakodisha wewe au..?!
Unawaza kukodisha?

Kipimdi fulani karibu na uchaguzi, serikali ilifanya uzinduzi wa magreda matatu brand new kwa kila wilaya ya DSM na hilo lilienda sambamba na malori matatu ya tani 10 kwa kila wilaya.

Magreda haya utayaona yakiwa bize kwenye majimbo yenye wabunge wa CCM au yakifanya kazi za binafsi. Sisi tuliochagua wapinzani, tunakomolewa kwa barabara zetu kutokarabatiwa.
 
mkuu njoo uishi huku machame baridi safi chakula safi...
hakuna foleni wala nini

Sote tukihamia machame unadhani hiyo baridi na chakula safi vitakuwepo tena? Na foleni kubwa sana itahamia huko! Kumbuka hata dar es salaam zamani haikuwa na matatizo mengi kama haya ya sasa yaliyoletwa na over population
 

Tatizo ni kwamba moja ya sababu inayotufanya tuendelee kuwa Masikini huwa tunakimbilia kufanya jambo jipya kabla ya kuhahakikisha tumetatua tatizo tulilonalo kwanza.
Kwa Mfano Raisi mzima anaongelea kujenga Reli mpya mpaka Burundi na nyingine mpaka Musoma wakati iliyopo ina Miaka 100 na haitumiki sasa kwa nini tusihakikishe kwanza iliyopo inatumika kwa 100% halafu baade ndio tuanze kujenga nyingine?

Sijapinga kabisa kujengwa kwa Madaraja, ila kabla ya kufanya hivyo tuhakikishe kwanza tumeshafanya kila kitu kujaribu kukabiliana na foleni ili haya Madaraja yawe hatua ya mwisho, na hili ni pamoja na kuhakikisha kwanza br. zinazoungana na br. kuu zinapitika bila shida ili madereva wasizunguke kwa mf. Mtu anaishi Kimara anataka kwenda Airport hana haja ya kuja mpaka Ubungo kuna br. inaanzia Mbezi kupitia Kinyerezi mpaka Ukonga ipitike kwa Uraisi huo ni Mfano tu, pia Foleni nyingi zinasababishwa na Daladala hivyo kuhakikisha hilo linaondoka na dala dala zote zisimame vituoni na sio barabarani, kuna uzembe wa madereva pia kutokuheshimu taa wengi wetu taa nyekundu ikiwaka hatusimami matokeo yake wale wa upande mwingine walioruhusiwa nao wanapita tunakutana ktktk na mwishowe hakuna anayekwenda mbele wala kurudi nyuma tukabiliane pia na Hilo kwanza.

Madereva wengi wanatanua matokeo yake wanaziba wale wanaokuja upande wa Pili mwisho wake hakuna anayeweza kwenda haya yoote yako ndani ya uwezo wetu na tuyatatue kwanza tukishamaliza hapo ndio tuanze mambo ya Kufikiria kujenga Madaraja...

Kuhusu Magreda ni kazi rahisi sana kwanza kila Kata inaweza kufanya Mfano hai ni Kata yangu huwa tunafanya sana tu na inasaidia sana kupunguza Foleni, usisahau kila kata ina Fungu la fedha...


 
Michepuko sio dili kwanza watu wenyewe wamejenga kiholela michepuko si utawavunjia wote kipnde kinachotenganishwa na barabara za mandela na sam nujoma kuelea mbezi ndo vipande hovyo kabisa nadhan ndo maeneo yake mengi hayakupimwa sa utajenga bara bara wapi,walau upande wa pili shekilango sinza manzese pana nafuu. Halafu mnaopinga flyover sijui mna takwimu za wapi kuna zile kuinua barabara kwenye junction wakat kulia na kushoto zinatengenezwa barbra zenye miteremko kuungana junction simple,ctaki kuamini kua nchi zoote waliojenga hivi hawakuona michepuko,tatizo tz w2wakishakariri kitu hawataki kubadilika na wengine humu jf ndo wale wale waliopanga mipango mibovu so hapa wanaspoil hoja tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…