La David Mattaka: Kwenye Hili simwelewi Kikwete! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

La David Mattaka: Kwenye Hili simwelewi Kikwete!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpaka Kieleweke, Feb 21, 2009.

 1. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Nimesoma taarifa ambayo ilitolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi Ndugu Philemon Luhanjo , ambayo inasema kuwa Rais Kikwete ameteua kikosi kazi kwa ajili ya kusimamia kazi ya kurekebisha shirika la Bima la Taifa (NIC).

  Kinachonifanya nishindwe kumuelewa ni kitendo cha kumteua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Nchini (ATCL) ndugu David Mtaka kuwa miongoni mwa wajumbe sita waliopewa jukumu la kusimamia kazi ya kurekebisha shirika la Bima wakati Mattaka ameshindwa kulisimamia shirika lake mwenyewe mpaka linajifia pamoja na serikali kumwaga mabilioni ya shilingi za walipa kodi kila wakati.

  Kikubwa zaidi kinachonifanya nishindwe kumwelewa Kikwete ni kazi za kikosi kazi hicho (Task Force) ambazo ni pamoja na kuandaa mpango wa kazi (NIC Bussiness Plan).

  Mataka aliyeshindwa kuandaa mpango kazi kwa ajili ya ATCL mpaka ikafilisika hivi ataweza kulinusuru shirika lingine wakati la kwake limemshinda?

  Hivi Mattaka , ambaye ameshindwa kabisa kuliokoa shirika lake anaweza kuokoa NIC?

  Kikwete na Mattaka wana mahusiano gani mengine tofauti na ya kikazi? kwani nashindwa kuamini kama Kikwete anashindwa kuona kuwa ATCL imeshindwa kufanya kazi na hata waziri wake wa Miundombinu ilimbidi naye akaunda kikosi kazi kwa ajili ya kulinusuru shirika hilo , huku mkurugenzi wake akiwa ameshazidiwa .

  Nashindwa kuzielewa akili za Kikwete kwani anachonionyesha hapa ni kuwa yeye hayaoni mapungufu ya Mattaka , na ndio maana anamtaka aende kuunda mpango kazi wa kufufua shirika lingine wakati la kwake linajifia.

  Nashindwa kumwelewa Kikwete anataka kulipeleka wapi shirika la NIC , ama anamtafutia Mattaka sababu ya kusema kuwa alikuwa na kazi nyingi na hivyo alishindwa kusimamia fedha zilizotolewa na serikali siku mahesabu yake yatakapokuwa hayako sawa.?
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  That reflects uwezo wa kuelewa na kupambanua mambo wa JK.
   
 3. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Wajumbe wengine ni pamoja na ,
  1.Balozi Charles Mutalemwa -Mwenyekiti.
  2.Agness Bukuku-katibu mkuu tume ya mipango na msajili wa hazina ,
  3.Kate Bandawe-Naibu Mkurugenzi Mkuu NSSF.
  4.Michael Mhando -kutoka Bima ya Afya.
  5.Justine P. Mwandu-kutoka idara ya usimamizi wa Bima.

  Hawa ndio wajumbe wa kikosi kazi na kimepewa miezi sita kuwasilisha taarifa yake Serikalini .

  Kama angetaka kupata mawazo mapya alipaswa kutafuta watu wengine kutoka sekta binafsi kwani hao wa serikalini ndio wamesababisha mashirika mengi kufilisika na kuwa na hali mbaya kama yalivyo leo , sasa wataweza kweli kumpa mawazo mapya?
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Labda anatakiwa mtu mwenye mawazo ya kiuwendawazimu kuelewa kinachofanyika
   
 5. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #5
  Feb 21, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Kwa jinsi tunavyoona hali ya ATC ingebidi Mattaka apambane hapo hadi hali ya hilo shirika liwe sawa kiutendaji.
  JK atakuwa amekosea sana kumpa jukumu lingine Mattaka wakati ATC kuna matatizo makubwa. Labda kama mkuu wa nchi ana nia nyingine ambayo hatuijui.
   
 6. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #6
  Feb 21, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli hii inaonesha uwezo wa mkulu kupambanua mambo ulivyo na walakini (hata washauri wake pia). ATCL haijatengemaa halafu mattaka huyu huyuy anateuliwa kwenye timu ya kusimamia urekebishwaji wa NIC (another shirika)!! Huyu jamaa vipi huyu???!!!!
   
 7. G

  Ghwakukajha Senior Member

  #7
  Feb 21, 2009
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Dont mess with 'wanamtandao'!!!But wahenga wanasema "mchawi,mpe mwanao akulelee" labda mkuu ndo alipotokea kwenye huu msemo ingawa huyu bwana tayari ashaiacha mahututi ATCL!!Pengine ilitumika ana-ana-doo....
   
 8. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #8
  Feb 21, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Kikwete amesoma Kibaha,one year ahead of Mataka. Kwa hiyo ni school mates.You can call it cronyism,Kiongozi anamchagua mtu ambaye ni loyal kwake,mtu ambaye anamfahamu.

  Indeed, Mataka ni school mate wangu pia Kibaha. Tulikuwa tunacheza sana ping pong.

  Jakaya Kikwete angeweza kuwa Rais badala ya Mkapa. It was just this cronyism that every one was worried about,ndio maana Kiwete ikabidi asubiri mpaka 2005.

  Sasa watu wanauliza,are we all in serious trouble. Should we be afraid? Itawezekana kuwathibiti mafisadi? Between you and me and the door post,nadhani itakuwa vigumu sana kuwathibiti mafisadi. There was plenty of time kuwakamata wote.

  Wanataka kutoa token punishment,but that is not enough. KABLA ya uchaguzi,mafisadi wote must be accounted for,CCM iende kwenye Uchaguzi na kusema," Mafisadi wote ,waliokuwa wanatajwatajwa, ni accounted for.''That is the way these things are done around the world.
   
 9. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #9
  Feb 21, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Nchi hii itaweza kweli kujiimarisha na kukua kiuchumi kama yule ambaye anashindwa ndio anaongezewa majukumu ya kwenda kutengeneza pengine?

  Inawezekana ndio maana alimwona Makamba kama mtu anayeweza kutengeneza dIra ya CCM , .
   
 10. kinetiq01

  kinetiq01 Member

  #10
  Feb 21, 2009
  Joined: Aug 25, 2006
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wajumbe wenzangu, hivi kwanini tunapoteza muda wetu kuhoji utendaji kazi wa mawaziri na maafisa wengine waandamizi serikalini, wakati mhusika mkuu anaendelea kupeta?

  Kwa kutathmini mfululizo wa high profile blunders zenye kugharimu taifa letu maendeleo, mimi naamini kabisa kuwa sasa ni wakati wa kugonga Ikulu.

  Hawa wote wanaofanya vituko si waliteuliwa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Jakaya Kikwete? Kama jibu ni ndiyo, basi huyu ndiye wa kumkosoa kwa uteuzi mbovu, utendaji wa ovyo na uzembe.

  The President is indeed responsible for the crazy deeds of his senior servants.People have been cautioning him right from the moment some of these appointments are made public, but as usual amekuwa akipuuza.

  Wanapokuja kufanya blunder, yeye hujiweka kando as if hawajui.Matatizo ya nchi yanasababishwa na uongozi wa rais kwa njia moja au nyingine.Kubali lawama Bw Kikwete.
   
 11. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #11
  Feb 21, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wasomi wetu ndio hao hao jamani...nyie wengine mpo UK na USA..!!
   
 12. D

  Dotori JF-Expert Member

  #12
  Feb 21, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 547
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sitarajii jipya toka kwa tume hii.
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Feb 21, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  You are a couple years behind playa....some of us figured out his abilities way back when before he even took the helm....so what's new?
   
 14. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #14
  Feb 21, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135


  1. I have no argument against this.

  2. There are about three reasons for this.

  2.1. The president is people pleaser to the core. He can and will never stand up for what is wrong in a person cause to him there is no God than the human beings. This is typically weakness human can no dare to carry on..

  2.2. The president has no firmness in him, has no true character to face and confront that which needs that treatment ...and this is either from the way he was brought up or cause he has the problem with the authority from the family he is coming from. He is too weak to face and overcome the really problem with authoritative nature...He can not come forward and do a 100% rebuke ...No No ...He has problem with his feelings...they are too painfully to do that...and the price the country is missing the really corrections from a true loving DAD!!!

  2.3 The President had a dream of becoming a president and he is enjoying that dream so comfortably...he just want to fulfill his long standing dream ...His dream of completing his first and second term is so important he doesn’t want to harm anybody in the way they will block him finish the coming term. To him is better to be passive and calculative to win the cheap popularity ...to place him in the second coming term...ili mzee akapumzike. He doesn’t to be firm and Hard on important issue cause that will ..make him go into conflict with the Chama and the government...

  13.0 All the ministers he elect very cleverly .... to make the above happen... No one with True character and bold enough to face the really issue for the people. No just there.... to make their dreams come true... that they have once become the ministers ... with or without any output...it doesn’t matter!! Walikaa Na Rais wao vizuri!! Passively and very feeble in their work no to harm any one especially the president even for the benefit of the wananchi.
   
 15. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #15
  Feb 21, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Mambo ya utapeli hutegemei kuyaona Serikalini. Haya ni mambo ya wahuni tu wa mitaani. Lakini inapokuwa Waziri Mkuu anahusishwa na mambo ya utapeli,na yule Waziri Mkuu inambidi ajiuzulu,ina maana Taifa lote limeingizwa mkenge.

  Kwa hiyo,ingawa credentials za Kikwete ni impeccable,Kikwete ni honest,wise,dedicated. Lakini hawa watendaji wake hawafanyi kazi vizuri.The Nation has come to a standstill. Lakini ukisema huna imani na Rais,inakuwa almost as if ungependa Rais ajiuzulu sasa hivi. Hilo ni jambo ambalo ni very drastic,and I must say,I have not thought of it that way. It seems a little bit imprudent to discuss this. Lakini ke time is wated wakati vingozi wakiwa incompetent. Rais Mkapa kila siku alikuwa hataki kusikia mtu yeyote anasema kasi ya maendeleo haitoshi. Lakini GDP ya China inakuwa 10 per cent every year. Why not us? Haina maana tutaendelea kama China in one year. It just means that we would be richer by an increase of one tenth every year.
   
 16. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #16
  Feb 21, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa RAIS anapekecha mwaka wake wa nne kama kiongozi mkuu wa TAIFA TANZANIA. Mwaka kesho atajisalimisha kwetu WANANCHI (kwa mujibu wa katiba) akiomba tumtunuku tena NAFASI HIYO ADHIMU bila shaka atadai kuwa amalizie kazi aliyoianza. WAUNGWANA tuna karibu miezi kumi na nane kabla tukio hilo UJUMBE WANGU KWA RAIS ni KUMALIZA KAZI ILIYOPO MBELE YAKE ATUHAKIKISHIE WATUHUMIWA WOTE WA UFISADI MASHAURI YAO YANAKUWA FIRST TRACK kelekea MAHAKAMANI. Katika kipindi hicho kabla ya uchaguzi. Kinyume cha hayo Mh AMEKOSA KURA yangu inadvance na nitajitahidi kuwashawishi wengi waungane nami.
   
 17. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #17
  Feb 21, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  bwana ganesh, uwezi kuchuma machungwa kwenye michongoma, yaani uwezi kuchagua baraza la mawaziri na nusu wakawa wabovu kama wewe sio mbovu, baraza la kwanza kabisa la mawaziri la kikwete liliprove failure just before end of year 1
  aka reshuffle baraza lake, lakini wajaka kutokea wakina chenge, karamagi, lowasa na wengineo, lakini pamoja na hayo yote badala ya kuchukua hatua anasimama mbele ya watu na kusema ni ajali ya kisiasa,
  mambo ya madini tunaweza tukasema yalifanyika wakati wa mkapa, na jk alipoingia madarakani alisema mikataba kama hiyo haiwezi kufanyika tena, lakini muda si mrefu karamagi akasaini buzwagi, na rais kakaa kimya tu sasa unataka tumtofautishe vipi na hao wenzie?
  Baada ya kufanya maendeleo anachokifanya sasa ni kuhakikisha kuwa kundi lake(mtandao) unakuwa hauitetereki, mtu kama magufuli ni potential sana na kuna wizara nyeti kabisa ambazo anastahili kupewa lakini kwa sababu yeye hayupo kwenye mtandao basi bora masha apewe, ni vigumu sana kwa mtu mwenye upeo safi kumtenganisha kikwete na hilo group
   
 18. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #18
  Feb 21, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Wakulu heshima mbele, nilikuwa nazungumza na watu waliofanya kazi na David Mattaka enzi hizo PPF ikiwa bado ni kitengo ndani ya shirika la bima na ambao wamemuelezea David Mattaka kama ni msomi na mjuvi sana katika mambo ya bima na hifadhi ya jamii ambaye alisomeshwa nchini marekani kwa miaka 4 na serikali yetu.Wanasema David Mattaka kwenye mambo ya Bima ni mahala pake na wangefurahi kama angekuwa Mkurugenzi wao mkuu badala ya huko walikomuweka ambako ni kama misallocation of resources na kushindwa kuitumia taaluma yake ipasavyo.

  Kwa kitendo cha Muungwana kumuweka katika kamati hiyo inaashiria kitu kimoja tu kwamba huenda ndiye atakayepewa mikoba ya kulifufua shirika la bima la Taifa.Mark my words hivyo ndivyo itakavyokuwa mara tu baada ya kukamilisha kazi waliyopewa.
   
 19. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #19
  Feb 21, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Mkulu never ceases to amaze me !! Ni vigezo gani vimetumika kumuingiza mtu huyu kwenye timu hii ?? kwa sababu imedhihirika wazi kwamba kazi siyo tu kwamba hajui kazi bali pia haiwezi. Si mkwe wa Mkulu alikwamishwa airport wakati Mataka huyu alipokodi ndege mbovu ya mahujaji? Si under his command ATCL ilisimamishwa ? i think first time in its history too !! Naona bongo ukitaka kupata ulaji zaidi wewe haribu tu... utaongezewa ulaji tena...this is the lesson our kids a learning from us.
   
 20. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #20
  Feb 21, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwani Mataka hajawahi kuwa kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii? Alifanya nini huko?
   
Loading...